Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Niliwahi kuuliza hivi - Mukasa/Rwegasira - One and the same ? na nikauliza kulikoni ? Rekodi zote za nyuma zinaonyesha kuwa mhusika amejulikana kwa maisha yake toka utotoni kama Oscar Mukasa. Hata hivyo baada ya kuteuliwa tu, ghafla jina lilibadilishwa na kuwa Oscar Rwegasira baada ya majadiliano makali ndani ya CCM. Jina Mukasa linajulikana kama jina la Kiganda - yanikumbusha jamaa moja kwa jina la Omari kutoka Kenya alivyoweza kujipenyeza hadi kufikia uongozi wa juu kwenye Chama cha kandanda Tanzania, FAT. Wakati huo, enzi za chama kimoja, wagombea walikuwa wanapitishwa na vikao vilivyojumuisha CCM.Mukasa aliyezaliwa Julai 1970, ni mtoto wa tano kati ya 10 katika familia ya Mzee William Mukasa na Mama Apolonia Mukasa. Alizaliwa katika kijiji cha Rukaragata kilichopo takriban kilometa tatu kutoka mji Biharamulo, barabara ya kwenda wilayani Ngara.
Baba yake ni mtumishi wa umma mstaafu ambaye amewahi kuwa Ofisa Afya wa wilaya ya Biharamulo kati ya mwaka 1977 na mwaka 1987 kabla ya kuwa Ofisa Afya wa mkoa wa Kagera kati ya mwaka 1987 na 1992 alipostaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa mtumishi wa umma sehemu mbalimbali nchini.
Tarehe 6/6/2009 nilikuwa na haya ya kusema -
Hata hivyo nauliza kitu kimoja, inaonekana kuna jitihada za kulizika jina Mukasa ingawaje mwanzoni tuliambiwa na washikaji wake kuwa anaitwa Oscar Mukasa na sasa ni Oscar Rwegasira. Je kuna kitu kinafichwa ?
Jaji Makame hata hili atalifumbia macho- ndio maana yuko pale.