Biblia ilivyookoa maisha ya mchezaji wa Chapecoense “Neto” kwenye ajali ya Ndege

Sasa Kiranga anaingiaje hapa?...au ndiye aliyeyatawala mawazo yako?
Kama mtu una uwezo wa kuwa mfuasi wa usichokijua kama kipo, utashindwa kuwa mfuasi wa kilichopo?
Sasa hivi unaniambia ni mfuasi wa kisichokuwepo halafu baadaye utaniambia ni Agnostic.
 
Unaweza kuthibitisha kwamba nimekashifu imani ya watu?......au una amini nimekashifu maana wewe kuamini inahitaji kuambiwa na siyo kureason?
Nithibitishe nini na wakati kufutwa kwa post zako ni uthibitisho tosha.

We unaeamini hakuna mungu hutaki imani yako hiyo ihojiwe.
 
Kwahiyo una amini aliyefuta hiyo post ni standard reference ya uelewa?
Siami kutokuwepo kwa Mungu bali nahitaji ushahidi wa uwepo wa Mungu toka kwa wanaodai yupo....Kama Mungu angekuwepo, mijadala ya namna hii isingekuwepo.
 
Amen! Ila watoto wa mamdogo wanajitahidi kupinga.Jaman Mungu huyu ni wetu sote,huyo kijana inawezekana kabisa kuwa alimwomba Mungu hata kabla ya safari.Leo hii kuna watu hata kuomba kabla ya safari wanapinga.Mungu si mjinga hata aseme ombeni! Hata kama siku yake bado but hii inatuonyesha sisi kumtafuta Mungu wa kweli wakati wote.
Kweli kabisa mkuu Mungu yupo na anatenda miujiza kila siku ila tumekua wagumu sana kuukubali ukweli ndio maana hata hapa kuna wakuu wanachangia kwa kukebehi au kuonesha hali ya kukashifu niwaombe tu ndugu zangu tuwe tuna mtanguliza Mungu katika kila tunalolifanya kwa sababu Mungu yupo na anatenda kazi zake Mungu amjalie afya njema huyo mchezaji alietumika kufanikisha kazi hii ya Mungu
 
Kwahiyo una amini aliyefuta hiyo post ni standard reference ya uelewa?
Siami kutokuwepo kwa Mungu bali nahitaji ushahidi wa uwepo wa Mungu toka kwa wanaodai yupo....Kama Mungu angekuwepo, mijadala ya namna hii isingekuwepo.
Kusema hakuna mungu ni imani na ndiyo unaiamini wewe,kama isingekuwa imani ungekuwa na ushahidi na kuonyesha kweli hakuna mungu,maana si hayupo.

Unajua hadi watu wanapokuja kuwaambia mthibitishe kuwa hakuna mungu ni kwa sababu kila mkielezwa kuhusu dalili za uwepo wa mungu mnakataa kwa kusema hamtaki kuamini,suala la mungu ni la imani sasa mnapokuja kupinga kuwa hayupo na wala hamtaki kusikiliza maelezo ya imani..ina maana mtakuwa ushahidi wenu wa kuwa hakuna mungu.
 
Wewe hujui useme lipi kati ya Mungu yupo ama hayupo.
Nisingekuwa nabishana na nyie mnaosema hakuna mungu,mbona hujawahi kuona kubishana na wanaoamini mungu?

Hivyo msimamo wangu ni mungu yupo,ila tatizo lako wewe unavyoona nasema wakristo wengi wanakuwa ma atheists na ndipo unaona sieleweki, na hivi ndivyo mlivyo atheists wengi kuwa na vichembe chembe vya ukristo.
 
Kusema hakuna mungu ni imani na ndiyo unaiamini wewe,kama isingekuwa imani ungekuwa na ushahidi na kuonyesha kweli hakuna mungu,maana si hayupo.

Unajua hadi watu wanapokuja kuwaambia mthibitishe kuwa hakuna mungu ni kwa sababu kila mkielezwa kuhusu dalili za uwepo wa mungu mnakataa kwa kusema hamtaki kuamini,suala la mungu ni la imani sasa mnapokuja kupinga kuwa hayupo na wala hamtaki kusikiliza maelezo ya imani..ina maana mtakuwa ushahidi wenu wa kuwa hakuna mungu.
Idea ya uwepo wa Mungu ina contradictions nyingi sana.
Sifa anazopewa Mungu na uhalisia haviendani hata kidogo.Unaposema Mungu ni mwenye huruma, ujuzi, upendo, na uwezo usio na ukomo halafu maovu na mateso yamekithiri duniani, hiyo ni clear contradiction.

Sasa kama swala ya kuamini uwepo wa Mungu ni la kiroho, hii idea ya uwepo wa Mungu iliingiaje kwenye physical world?
 
Biblia zipo hadi guest but watu wanapata ukimwi cku yake ilikuwa haijafika period
 
Idea ya uwepo wa Mungu ina contradictions nyingi sana.
Sifa anazopewa Mungu na uhalisia haviendani hata kidogo.Unaposema Mungu ni mwenye huruma, ujuzi, upendo, na uwezo usio na ukomo halafu maovu na mateso yamekithiri duniani, hiyo ni clear contradiction.

Sasa kama swala ya kuamini uwepo wa Mungu ni la kiroho, hii idea ya uwepo wa Mungu iliingiaje kwenye physical world?
Hata uwepo wa mwanadamu sio halisi !!
 
Na hao wengine wote siku yao ilikuwa imefika??
Je hao wengine watano walionusurika walikutwa wanasoma biblia pia? Halafu mtu akisoma biblia ukimkata kichwa je hafi? Na je mtu akisoma biblia na kutembea na biblia hatokufa kamwe?
 
NETO-CHAPECOENSE.jpg

Wiki moja baada kutokea ajali mbaya ya ndege iliyokuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil na kuua abiria 71 wakiwemo wachezaji wa timu hiyo, waandishi wa habari, makocha na wafanyakazi wa ndege hiyo, imetoka ripoti kuwa mchezaji Helio Neto aliyenusurika alikuwa akisoma Biblia kabla ya kutokea ajali.
nintchdbpict000285630805.jpg

nintchdbpict000285577557.jpg
undefined

Kwenye kipande kifupi cha Video kilichoonekana kwenye camera za ndege hiyo kimeonesha kuwa mchezaji huyo alikuwa akisoma Biblia muda mwingi akiwa kwenye ndege na hata baada ya ajali bado Biblia ilikutwa kwenye siti yake pamoja na yeye Neto kuwa kwenye hali mbaya.

Ukurasa ulioonekana kwenye Bibla ilikuwa ni kutoka kwenye kitabu cha Zaburi 63:6-8. Ambayo ina maneno haya;

“Wakati ninapokukumbuka kitandani mwangu, wakati wa makesha ya usiku natafakari juu yako. Kwa maana umenisaidia na katika kivuli cha mabawa yako napiga vigelegele kwa shangwe, nafsi yangu imekufuata karibu, mkono wako wa kuume unanishika sana.”

zz.jpg
Baada ya kutokea ajali hiyo, Biblia ya mchezaji huyo ilikabidhiwa kwa mke wake ambaye alikiri wazi kuwa mume wake amekuwa mtu wa dini sana na huwa anatembea na Biblia yake popote anapokwenda.

Jumla ya watu 71 walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege aina ya Avro RJ85 iliyotengenezwa nchini Uingereza baada ya kuanguka kwenye milima ya Medellin nchini Colombia, ambako timu ya Chapecoense ilikuwa inaenda kucheza fainali za Copa Sudamericana.
Naamini Mungu ni Mungu tu, lakini kurasa nzima ina hiyo mistari miwili tu?
 
Wahooo! m so in love with God,what a might God.
 
Back
Top Bottom