Bibi wa Miaka 72 Azaa na Mjukuu Wake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
4414158.jpg


Bibi Pearl akiwa na mpenzi wake ambaye pia ni mjukuu wake

Bibi mwenye umri wa miaka 72 wa nchini Marekani amewashangaza marafiki zake na familia yake baada ya kutoboa siri kuwa anatarajia kuzaa mtoto na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 26.

Bibi Pearl Carter, 72, anasema kuwa hajawahi kuwa mwenye furaha kama wakati ambao amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake Phil Bailey mwenye umri wa miaka 26.

Bibi huyo wa Indiana, Marekani anatumia pesa zake za pensheni kumlipa mwanamke atakayejitolea kuibeba mimba yake na mjukuu wake.


Bibi Pearl alisema kuwa hajali maneno ya watu kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi na mjukuu wake na anasubiria kwa hamu kuzaa naye mtoto.


Phil ni mjukuu wa bibi Pearl kwa mtoto wake wa kike Lynette Bailey ambaye alipelekwa kwenye nyumba ya kulea yatima alipokuwa na umri wa miaka 18.


Wakati mama yake alipofariki, Phil alimtafuta bibi yake ambaye alikuwa hana mawasiliano naye kwa muda mrefu na ghafla walianza uhusiano wa kimapenzi.


"Ilikuwa ni wiki ya pili pamoja baada ya chakula na mvinyo nilipomuita Phil chumbani kwangu, nilimkalisha kitandani na kuanza kumbusu", alisema bibi Pearl.


"Nilitarajia angenikatalia lakini naye alianza kunibusu" Pearl alisema akielezea mwanzo wa uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake.


"Kwa mara ya kwanza nilijihisi kwenye msisimuko mkubwa wa kimapenzi", alisema bibi Pearl.


Phil naye kwa upande wake anasema kuwa anampenda sana bibi yake na kwakuwa tangia zamani alikuwa akiwapenda wanawake wazee anadhani bibi yake ni mrembo sana.


Phil na bibi yake wametumia dola 54,000 kumlipa mwanamke atakayebeba ujauzito wao.


"Ni kweli tunachekwa na kutukwana wakati tunapobusiana mbele za watu lakini hatujali kitu", alisema Phil.


"Sitamuomba radhi mtu yoyote kwani naamini Mungu amenipa nafasi ya pili", alimalizia kusema bibi Pearl.
 
Mwisho wa dunia sasa, matukio na machukizo kwa Muumba yatajitokeza. Huku ni kukosa heshima kusikoelezeka!!
 
FUNDISHO:
BINADAMU YU TOFAUTI NA MNYAMA....
BINADAMU AWEZA KUWA MBAYA KULIKO HAYAWANI WA MWITUNI.
BINADAMU MUME NA MKE NI HALALI KUTENGANISHWA - HUJUI NI SAA NGAPI MVUTANO WA SUMAKU UTATOKEA!

Haijalishi umri, rangi, sura, undugu, wala kigezo chochote hasa kama wahusika wamejivua haya/soni.
MUNGU ATUSAMEHE MAANA ANAONA MACHUKIZO MENGI MNO NA KUTUVUMILIA KWA KIWANGO KISICHOFIKIRIKA.
 
Huyo dogo naye ana matatizo kabisa. Kukimega hicho kibibi ni wehu wa hatari kabisa. Ah! Lakini hii mizungu huwa na mambo ya ajabu siku zote!!
 
- kama wote wameridhia kuwa wapenzi, let them enjoy jamani.

- kwani penzi halichagui
 
Jamani hilo tusilishangae sana hao wameamua kuwa wa wazi, hebu wazia mtu anayetembea na mtoto wake!! Na haya yanatokea hata kwetu Tz yapo sana
 
mi nafikirifunzo kubwa ni tabia ya kupenda kuishi mbali na familia zetu inavyoweza weza punguza social distance btn the two. psycologically they dont care bloodrelationship btn them, lkn suala la umri majuu hamnazo. may God 4giv them.
 
Tunaomba source ya hii habari..... Please!!!!
Usituwekee link ya picha isiyo na maandishi!!!!
 
Back
Top Bottom