Bibi wa Miaka 107 Anatafuta Mume wa 23

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Bibi wa Miaka 107 Anatafuta Mume wa 23

EBC49B12-E76D-4810-8B76-4F0459AAE8A8.jpeg


Bibi Wook Kundor

Tuesday, September 15, 2009 7:32 AM

Bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia ambaye alishaolewa na kuachika mara 21 amesema yuko tayari kuolewa na mwanaume mwingine kwa mara ya 23 kwasababu anahofia kuwa mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine mwenye umri mdogo.
Baada ya kuolewa na wanaume 21 na kuachika, bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia amesema kuwa anahofia kukimbiwa na mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa ambaye miezi miwili iliyopita alikamatwa akitumia madawa ya kulevya.

Bibi Wook Kundor alipata umaarufu duniani baada ya kuolewa kwa mara ya 22 na mwanaume ambaye amemzidi jumla ya miaka 70.

Hivi sasa bibi Wook hana imani kabisa na mumewe Muhammad Noor Che Musa mwenye umri wa miaka 37 ambaye hivi sasa yuko kwenye kituo cha kurekebisha tabia akipatiwa matibabu ya kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya.

Bibi Wook ameishaanza kusaka mume wa 23 kwani anahofia Muhammad akishatoka kwenye kituo hicho na kuacha tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine wa rika lake.

"Katika siku za hivi karibuni kuna hofu imeniingia" alisema bibi Wook huku akiwa ameshikilia picha yake.

"Najua kwamba mimi ni mwanamke niliyezeeka. Sina umbile la kuvutia tena na kwa umri wangu siwezi kumvutia mwanaume yoyote"

"Nia yangu ya kuolewa tena ni kuepuka upweke na si kwa sababu yoyote ile" alisema Wook na kuongeza kuwa anajihisi mpweke sana wakati huu ambao mumewe yuko mbali.

Bibi Wook alisema kuwa angependa kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr wiki ijayo akiwa pamoja na mumewe.

Wook alisema kuwa ana mpango wa kumtembelea Muhammad kwenye kituo chake cha kurekebisha tabia jijini Kuala Lampur iwapo majirani zake watampeleka huko kwa gari.

Muhhamad alifunga ndoa na bibi Wook miaka mitatu iliyopita akisema kuwa urafiki wa karibu na heshima uligeuka kuwa mapenzi ya kweli.

UPDATE:

Bibi huyu alifariki Juni 2016 akiwa na umri wa miaka 114
 
Back
Top Bottom