Bibi Titi Mohammed, mwanamke aliyeitikisa Tanzania na Dunia

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,030
Habari wanajamvi

Wakati tukimkumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere naomba pia tujikumbushe pia matatizo ambayo mwalimu amewahi kupitia.

Moja ya tatizo ambalo Mwalimu alipitia nikutaka kuuwawa na kupinduliwa kwa mara ya pili. Njama ambazo pia zilimhusisha mwanamama BIBI TITI MOHAMMED. Bibi Titi alizaliwa mwaka 1926.

Tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka 1969 na mwanzoni mwa mwaka 1970.

Baada ya uchunguzi kesi ilianza kunguruma Juni 8, 1970 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar.

Bibi Titi Mohammed (45) aliwashangaza Watanzania na Dunia kwa ujumla.

Aliwashangaza kwa sababu;

1. Enzi hizo mwanamke kujihusisha na kitu kizito kama hicho ilikuwa ni ndoto, lakini yeye alifanya na alimwaga fedha kwa kazi hiyo.

2. Bibi Titi aliwahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT).

3. Alishirikiana na Mwalimu wakati wa kudai uhuru na hata baada ya taifa kuwa huru. 1954 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa chama cha TANU.

Kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine ( Majina yao hayajawekwa hapa ) Bibi Titi Mohammed alitumia majina bandia ya kazi. Mama huyo alitumia majina kama Mama Mkuu, Mwamba au Anti wakati wa mipango yao ya mauaji na kuipindua serikali ya Nyerere.

Biti Titi alikamatwa na polisi Oktoba 1969 akiwa na waziri wa zamani wa kazi, Michael Kamaliza pamoja na maofisa wanne wa JWTZ na wote wakafunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua na kumpindua Nyerere.

Nawasilisha.

TAARIFA HIZI HAZIPO WAZI SANA NDIYO SABABU WATU WENGI HAWAFAHAMU KUWA MWALIMU NYERERE ALINUSURIKA KUPINDULIWA MARA3.

NAOMBA KUUNGANISHA NA MCHANGO WA MWANA JF MWENZETU AMBAYE ALIEZEA JUU YA MAJARIBIO HAYA MATATU YA MWALIMU KUPINDULIWA.

Yericko NyerereVerified

[HASHTAG]#5Nov[/HASHTAG] 3, 2012Joined: Dec 22, 2010Messages: 15,128 Likes Received: 1,229 Trophy Points: 280

Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
 
Dunia, maana kwa wakati ule kwa bara la Afrika ni wanawake wachache sana waliothubutu kushiriki katika mapinduzi.

india na pakista majina yao nimeyasahau hao wanawake watata
 
Dinia ilishtuka, ilikuwa taarifa nyeti sana ya ki-intelijensia iliyomuhusisha mwanamke hasa kwa bara la Afrika.
 
Hua tunaambiwa sifa tu za nyerere je upande wa pili wa maisha yake nae alikuaje?
 
Nimestuka sana Ndg.
Watu wengi hawafahamu kuwa Mwalimu alinusurika kupinduliwa mara 3. Mmoja kati ya viongozi wa jaribio la mapinduzi ya mwisho aliuwawa na mwingine alipotelea kusipo julikana maana hakukamatwa
 
Habari wanajamvi

Wakati tukimkumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere naomba pia tujikumbushe pia matatizo ambayo mwalimu amewahi kupitia.

Moja ya tatizo ambalo Mwalimu alipitia nikutaka kuuwawa na kupinduliwa kwa mara ya pili. Njama ambazo pia zilimhusisha mwanamama BIBI TITI MOHAMMED. Bibi Titi alizaliwa mwaka 1926.

Tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka 1969 na mwanzoni mwa mwaka 1970.

Baada ya uchunguzi kesi ilianza kunguruma Juni 8, 1970 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar.

Bibi Titi Mohammed (45) aliwashangaza Watanzania na Dunia kwa ujumla.

Aliwashangaza kwa sababu;

1. Enzi hizo mwanamke kujihusisha na kitu kizito kama hicho ilikuwa ni ndoto, lakini yeye alifanya na alimwaga fedha kwa kazi hiyo.

2. Bibi Titi aliwahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT).

3. Alishirikiana na Mwalimu wakati wa kudai uhuru na hata baada ya taifa kuwa huru. 1954 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa chama cha TANU.

Kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine ( Majina yao hayajawekwa hapa ) Bibi Titi Mohammed alitumia majina bandia ya kazi. Mama huyo alitumia majina kama Mama Mkuu, Mwamba au Anti wakati wa mipango yao ya mauaji na kuipindua serikali ya Nyerere.

Biti Titi alikamatwa na polisi Oktoba 1969 akiwa na waziri wa zamani wa kazi, Michael Kamaliza pamoja na maofisa wanne wa JWTZ na wote wakafunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua na kumpindua Nyerere.

Nawasilisha.

TAARIFA HIZI HAZIPO WAZI SANA NDIYO SABABU WATU WENGI HAWAFAHAMU KUWA MWALIMU NYERERE ALINUSURIKA KUPINDULIWA MARA TATU.

SOURCE: GLOBAL PUBLISHER

NAOMBA KUUNGANISHA NA MCHANGO WA MWANA JF MWENZETU AMBAYE ALIEZEA JUU YA MAJARIBIO HAYA MATATU YA MWALIMU KUPINDULIWA.

Yericko NyerereVerified User

[HASHTAG]#5Nov[/HASHTAG] 3, 2012Joined: Dec 22, 2010Messages: 15,128 Likes Received: 1,229 Trophy Points: 280

Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
Hv kassim hanga nae kifo chake kilikuaje vile
 
Ungeondoa neno "kutikisa"
Maana inaleta picha ya chura.
 
Hicho kibibi cha kariakoo kinwaweza kutikisa labda Tandamti lakini si Dar wala Tanganyika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom