Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

We mleta thread umeanza udini wako! Huna lolote

Huo ndio upumbvu mlionao, mkiambiwa kweli mnajidai tunaleta udini, yaani nyinyi siku zote mnakuwa kama vile serikali ya marekani "mkisema nyinyi nisawa lakini wengine inakuwa noma" Huo uliolezwa ni ukweli mtupu lakini kwa vile alotajwa ni muislamu inkuwa hana uzito hata kama anastahiki kupewa haki yake.
Na ukweli ni kwamba Nyerere bila ya watu kama Bi Titi bint Mohammad asingeweza kufanya chochote. Hiyi Historia yenu mlipewa ya kughushi hayo ndio madhara yake mjomba JIFUNZE UELEWE ASILI YA TANGANYIKA.

Soma historia kaka ujifunze kuujua uhuru wa Tanganyika ulipatikana vp na ni akina nani walishiriki usiropoke na ujinga wako huo. Kama huko Tanganyika mnashindwa kuijua historia yenu vizuri basi njoo Zenji tukufunze mjomba.
 
Kuna mtu mmoja ningependa sana kuipata historia yake naye ni Cecil Matola....kuna kipande hiki kuonyesha harakati za Uhuru zilivyoanza...kinasema:- Prospects in Tanganyika were not much better than other territories, as the example of Tanganyia African Association (TAA) reveils. The TAA was founded in Dar-es Salaam in 1929. Under the leadership of Cecil Matola, Kleise Sykes, Mzee Bin Sudi and Ramadan 'Ali, the Association stated its aims as being 'to safeguard the interests of Africans, not only in this territory but in the whole of Africa...
Source:- Bofya

Je, kuna mtu mwenye habari kamili huyu Cecil na hawa waasisi wa Uhuru wetu ambao wamesahaulika baada ya kizazi kipya cha kina Nyerere kuingia..

Mkandara,
Hili swali ungeliekeleza kwa mwanahistoria wetu Mohammed Said. Yeye amejikita zaidi kuandika juu ya waanzilishi wa harakati za uhuru ambao historia ya kawaida imewasahau. Nina hakika atakuwa na habari za bwana Matola.
 
butiama%2520288.jpg


Wanajamii forums kuna mwanamke mmoja shupavu enzi za kupigania uhuru ambaye alikuwa bega kwa bega na Nyerere na kudiriki kuwanyooshea viledole vibosile waingereza kama Halima Mdee anavyowanyoshea vidole vibosile wa serikali na CCM wanaowanyang'anya ardhi wananchi na kujilimbikizia bila kuziendeleza.
  • Kwenye picha anaonekana nani anamfahamu?
  • Je, ni nyadhifa gani alishawahi kuzishika na alionyesha uwezo sawa kama alivyokuwa kipindi cha kupigania uhuru?
 
Mbona mnatudharau wazee na vijimaswali kama hivi? Ni wazi ulikuwa hujazaliwa enzi hizo! Haya, umeshajibiwa.
 
Mambo kama haya ndio yanawafanya watu wahoji mtu kutangazwa mwenye rehema. Ni vigumu sana mwanasiasa kuitwa mwenye rehema kama hutaki nitajie unayemjua.
 
http://4.bp.blogspot.com/-ViPKGxfvt...v5rjQdg/s1600/BIBI_TITI_MOHAMMED-1%5B1%5D.JPG Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa ni mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania.
Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua Serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na Rais Julius Kambarage Nyerere.

Baada ya kutolewa Jela, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wakisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani na kumtenga.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya Uhuru, Bibi Titi alionekana katika makaratasi ya chamatawalaCCM kama"Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 novemba 2000 Bibi Titi alifariki kwenye hospitali ya 'Net Care Hospital' ya mjini Johannesburg ambako alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya barabara kubwa za jijini Dar es salaam imepewa jina la Bibi Titi kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.mia
 
Mbona huwa hatajwi kwenye list iliyo husika kuleta uhuru, au wanamhujumu?
 
Uhuru wetu tulioupata umechangiwa na watu mbali mbali, lakn mbona taarifa za weng wao n ngumu kupata?? Wadau kuna mwenye taarifa za harakati za Bibi titi mohamedi ktk kupigania uhuru?? Tujuzane!
 
Bwana mkubwa, barabara haiwezi kuitwa Bibi Titi sreet. Huo ulioutaja ni mtaa. Ile barabara inayoanzia pale CBE hadi Serena (sheraton ya zamani) inaitwa Bibi Titi road.
 
hv ni hatua gani zichukuliwe ktk soma la historia la nchi hii ili tuweze kuwatambua hawa wengine mana ktk kosoma kwangu kote kuhusu historia ya nchi hii nilimjua nyerere ktk kila jambo kumbe kuna wengine kibao hatuwafahamu na walijitoa kupigania uhuru wa nchi hii
 


Hii ni kamba, mwongo mkubwa!

Kwanza, Bibi Titi hakumleta Nyerere TAA, na wala si Kawawa. Pia, Waislam na Wakristo ni wote walishiri kwenye harakati za Uhuru.

Bibi Titi hakuwepo kwenye picha wakati wa TAA, wala TANU ya mwanzo.
Bibi Titi ndio aliletwa kukutana na Nyerere, 1955, na dereva Taxi aliyejuana na shemeji wa Bibi Titi. Baadae, shemeji wa Bibi Titi akawa anamsukuma Bibi Tibi ahudhurie mikutano ya Nyerere, na baadae akavutiwa nae, akapewa kadi namba 16. Nyerere alikuwa na kadi namba moja.

Na Kawawa alikuja TANU akitokea vyama vya wafanyakazi mwaka 1958, four years behind the curve!


Na madai yako mengine ya Wakristo vs Waislam ni uwongo wa kuchomwa moto. Wakristo na Waislam walishiri bega kwa bega katika harakati. Walionzisha TANU wako 17, wa dini zote:

(1)Mwalimu J.K. Nyerere – Mwenyekiti
(2)Geremano Pacha
(3)Joseph Kimalando
(4)Japhet Kirilo
(5)C.O. Milinga
(6)Abubakari llanga
(7)L.B. Makaranga
(Saadani A. Kandoro
(9)Suleman M. Kitwara
(10)Kisung’uta Gabara
(11)Tewa Said Tewa
(12)Dossa A. Aziz
(13)Abdu Sykes
(14)Patrick Kunambi
(15)Joseph K. Bantu
(16)Ally Sykes
(17)John Rupia

Na ukienda nyumba zaidi, hata viongozi wa Kitaifa wa TAA walioanza kutuma madai ya kimaandishi ikulu ya Sir Edward Twinning kudai chama kitambulike kwa uwakilishi Bungeni walikuwa ni Mwenyekiti na Katibu Mkuu, TAA Taifa, Abdulwahid Sykes na Vedastus Kyaruzi respectively.

Hiyo ni kabla na wakati wa uundwaji wa TANU. Baada ya kuundwa, TANU ili recruit viongozi wa harakati kutoka viongozi wa vyama vya ushirika, Nsilo Swai, Sir George Kahama, Jeremiah Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile, na wengine.

Kwa hiyo, kusema TANU ilikuwa ya Waislam waliokaribisha Wakristo ( or vice versa ) ni urongo, uzandiki.

Wangapi wapo hai hapo?
 
ukumbi wa wawa nazi kutaja wazee kibao..km Tambaza na wengine ambao in reality wameshakula kuliko hata wanajeshi wetu ktk vita ya kagera, kuliko hata akina Nyerere....

Mnayo kazi ndugu zangu....
 
Jamani kutumia nguvu na mali kujenga chama si hoja hasa pale unaposaliti malengo ya chama, chama ni kikundi cha watu wenye lengo moja, kwa chadema ni kuingia ikulu, mtu anapokiuka malengo si mwanachama,msaliti
 
Hebu tueleze kambona na bibi tti walisaliti nini siasa za TANU, Tatizo kubwa viongozi wa kiafrika hawa taki challenge. Sio, titi wala kambona tu, kwa taarifa yako wapo viongozi wengi wakati wa siasa za chama kimoja na wakati wa utawala wa mwl. nyerere walipinga siasa za chama kimoja na wakashauri mfumo wa vyama vingi ulo kuwepo kabla ya uhuru. hapo ndipo mwl. akaanza kuwaweka vizuizini viongozi waaandamizi miongoni mwao ni balozi kasaga tumbo. sasa tueleze bibi titi na kambona walikosea nini? siku zote ukiwa kiongozi usiogope changamoto
 
Usaliti ni usaliti tu, hata ukitumwa sokoni kufata chakula, hela ukazinywa bia, kambona na bibi titi walisaliti imani ya chama chao, mfumo wa chama kimoja,mazingira yaliruhusu kuitwa wasaliti
 
Back
Top Bottom