Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

..binafsi nadhani ni upotoshaji kudai harakati za Uhuru wa Tanganyika zilianzishwa na Waislamu.

..waasisi wa harakati zile hawakusukumwa na imani za madhehebu yao kudai Uhuru. kilichowasukumu kudai uhuru ni uzalendo wao kama WATANGANYIKA.

..harakati za kudai uhuru wa Tanganyika zilikuwa za ki-secular na KITAIFA ndiyo maana kila Mtanganyika bila kujali imani yake ya kidini alijiunga nazo.

..Wachagga na Wameru walishaanzisha harakati zao za self determination na walikuwa mbali zaidi ya Tanu. lakini kwasababu Tanu ilikuwa chama cha kitaifa Wachaga na Wameru walikuja kuungana na Tanu.

..kuna taarifa za kufanyika matambiko ya jadi wakati wa harakati za uhuru. matambiko hayo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Kiislamu na Kikristo. kama harakati za kudai uhuru zilikuwa za kidini-dini kama wengi wanavyojaribu kulazimisha basi matambiko yale yasingefanyika.

..pia zipo taarifa za Mwalimu Nyerere kupewa msaada wa kifedha na mashirika ya Kidini kama Maryknoll wakati wa harakati za kudai uhuru. sasa sidhani kama Mwalimu angepata msaada toka kwa wamisheni kama majority ya washirika wake walikuwa na mtizamo wa Ki-Ayatollah.
 
Hakuwa lulu tena, bali mhaini. Alihusika njama za kuipindua serikali mwishoni mwa miaka ya 1960s na kuhukumiwa jela miaka 10. Alitumika jela miaka michache tu na akasamehewa na Nyerere. Kutokana na hilo Mtaa wa Titi Street ulibadilishwa na ukawa UWT Street.

Hakusikika tena kisiasa kwa miaka 20 baadaye -- hadi vilipoingia vyama vingi, ndipo CCM waliona wako hatarini kupoteza nchi hivyo walim-habilitate haini huyo ili kuhamasisha wanawake. Mtaa ule ukarudishwa kuwa Titi Mohgamed Street tena!

Hiyo ndiyo CCM -- kwa kuhaha ndiye wenyewe. Wako taytari kumtumia shetani iwapo atasaidia waendelee kukaa madarakani. Utasemaje kwa hawa mafisadi walioiba hela za wananchi na bado wamo katika vyombo vya juu vya chama tawala?

Kujihusisha kuipindua nchi, bibi Titi alikuwa tayari kuona damu nyingi ya wanannchi kumwagika, endapo kungetokea machafuko kutoaka na mapinduzi.

Mimi nadhani kufufuliwe zile harakati zilizokuwapo huko nyuma za kupinga mtaa huo kupewa tena jina la ibi Titi -- mhaini aliyethibitika.
 
Bila shaka Kafiribangi anazungumzia kesi ile ya uhaini ya akina Kambona na Chipaka. Ni hakika alihukumiwa jela na rufaa yake katika Court of Appeal for Eastern Africa (iliyokuwa chini ya EA Community ya zamani) ilishindwa. mazuri yote aliyofanya wakati wa kudai uhuru yaliharibika kwa tamaa yake hii.

Nyerere alimsamehe tu baada ya kubeba mimba mle ndani. Hata hivyo Kafiribangi hakumtendea haki -- alipaswa kusema Mungu Mwenyezi amlaze mama huyo mahala pema peponi.
 
Huyu bibi alikuwa mkosoaji mkubwa wa siasa mbovu za Nyerere (yes call me anti Nyerereism if you please) na aligombana na Nyerere baada ya kumlaumu sana na hatua yake ya kutaifisha mali za wananchi (wajasiriamali wa siku hizo) na kilichomuudhi sana bibi Titi ni kule kuwadhulumu waislamu kwa kuwanyan'ganya mali zao na kuuwa jumuiya zao za kimaendeleo. Nyerere alipovyomshughulikia bibi huyu ni hadithi ambayo haipaswi kusimuliwa mbele ya mtu wa chini ya miaka 18, ni aibu na udhalilishaji wa hali ya juu kuwahi kufanyiwa mwanamke mtu mzima na heshima yake kama yeye ndani ya Jamhuri hii ya Muungano tena na mtu aliyemsukuma kwa nguvu na mali yake kuwa rais wa nchi.

Bibi Titi kama alivyokuwa Kasella Bantu na Eli Anangisye, walikuwa ni miongoni mwa watanzania wachache wa siku hizo waliokuwa na uthubutu wa kukosowa uozo wa serikali ya Nyerere, ingawa Nyerere alitumia ubabe kuwashughulikia, bado walibaki katika haki na kusimamia ukweli wa kile walichokiamini, ni historia baadae ilikuja kutoa hukumu kuwa walikuwa sahihi na Nyerere alikuwa wrong kushabikia siasa za kijambazi na unyan'ganyi, alizoziita "ujamaa na kujitegemea", ambazo zilishindwa.

Bibi Titi anabaki kuwa ni alama ya harakati za wanawake waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano ya uhuru wa kweli na haki za wananchi, mawazo ambayo alikuwa aki share na mwanasiasa machachari wa Kenya siku hizo, Jaramog Oginga Odinga (baba yake Raila Odinga), ambaye hakupendezwa kabisa na uhuni wa watawala wa Kiafrika baada ya uhuru waliojifanya "wakoloni weusi", katika maandishi yake yaliyokuja kuwa kitabu "Not Yet Uhuru", anabainisha wazi kuwa Afrika haijapata kile ilichokipigania kwa jasho na damu kwa kuwa "ukoloni wa mtu mweusi" umechukuwa nafasi yake.

Oginga, kama Bibi Titi, waliona viongozi waliopewa dhamana za kuyaongoza mataifa machanga baada ya uhuru,wanageuka wabinafsi, wachoyo, makatili na wasiopenda kusikiliza bali kusikilizwa na kukataa kata kata kukosolewa kwa namna yoyote ile, wamekuwa wabaya zaidi ya wakoloni weupe, kwao wao (Bibi Titi na Oginga) uhuru ulikuwa bado kwa watu weusi kutoka na siasa chafu za kidikteta za Kenyatta na Nyerere,Nkurumah n.k.
 
Junius - huwezi kamwe kumlinganisha Bibi Titi na Kasela Bantu na wengine. Bibi Titi alikuwa yes-woman wa Nyerere hadi mwisho. Ndo maana wakati wa ujio wa vyama vingi hakwenda upinzani, alibakia CCM, chama chake na kuikampenia kikamilifu (pamoja na Nyerere) ili kishinde. Uhasimu wake na Nyere uko wapi? Wapinzani hasa wa Nyerere -- huyo Kaselabantu, Kasanga Tumbo, Lifa Chipaka, Wilfrem Mwakitwange nk waliingia upinzani, lakini siyo mama huyu.

Hayo masuala ya uisilamu nk ni ya kwako tu -- ili kujenga hoja yako. Suala ni: Jee hakuhuisika kutaka kupindua nchi, kosa la uhaini na akapatikana na hatia?

Mimi nadhani mjadala uishie hapo.
 
Hayo masuala ya uisilamu nk ni ya kwako tu -- ili kujenga hoja yako. Suala ni: Jee hakuhuisika kutaka kupindua nchi, kosa la uhaini na akapatikana na hatia?

Mimi nadhani mjadala uishie hapo.
You got it all wrong ZM!
Kuwa hakwenda upinzani hakumaanishi alikuwa Yes woman wa Nyerere...huyu mama baada ya kutoka jela hakuwa na hamu ya siasa hasa, alichagua ku keep low profile in politics kwa kuwa yaliyomfika kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe "...namwachia Mungu...", yalimtosha na afya nayo ilikuwa shida tupu.
Vipi abaki mwema kwa Nyerere? natamani ungewasikia vijana waliotumwa na Nyerere "kumshughulikia" kule Kiinua Miguu, Zanzibar, ungechoka mwenyewe.
suala siyo hilo unalotaka wewe, mtoa mada anauliza "bado alikuwa lulu baada ya uhuru?"
 
You got it all wrong ZM!
Kuwa hakwenda upinzani hakumaanishi alikuwa Yes woman wa Nyerere...huyu mama baada ya kutoka jela hakuwa na hamu ya siasa hasa, alichagua ku keep low profile in politics kwa kuwa yaliyomfika kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe "...namwachia Mungu...", yalimtosha na afya nayo ilikuwa shida tupu.
Vipi abaki mwema kwa Nyerere? natamani ungewasikia vijana waliotumwa na Nyerere "kumshughulikia" kule Kiinua Miguu, Zanzibar, ungechoka mwenyewe.
suala siyo hilo unalotaka wewe, mtoa mada anauliza "bado alikuwa lulu baada ya uhuru?"

You also got it all wrong my brother! Nyere alipofanya (au alipofanyiwa) birthday ya kutimiza miaka 75 (in April 1996) Bibi Titi alikuwapo pale Diamond Jubilee Hall. Runinga zilmuonyesha Bibi Titi - wakati huo kesha rudi kundini (CCM) -- kutoa speech ya kumtukuza Nyerere hadi mtu unaweza kutapika. Wengi walitegemea vyema angekuwa upinzani kutokana na masaibu hayo yaliyompata! Upo? let's c lose this topic please!!!!!!!!
 
You got it all wrong ZM!
Kuwa hakwenda upinzani hakumaanishi alikuwa Yes woman wa Nyerere...huyu mama baada ya kutoka jela hakuwa na hamu ya siasa hasa, alichagua ku keep low profile in politics kwa kuwa yaliyomfika kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe "...namwachia Mungu...", yalimtosha na afya nayo ilikuwa shida tupu.
Vipi abaki mwema kwa Nyerere? natamani ungewasikia vijana waliotumwa na Nyerere "kumshughulikia" kule Kiinua Miguu, Zanzibar, ungechoka mwenyewe.
suala siyo hilo unalotaka wewe, mtoa mada anauliza "bado alikuwa lulu baada ya uhuru?"

Mkubwa usiwe mchoyo wa habari asilani..hebu tumegee hao vijana walimshughulikiaje bibi titi huko 'KIINUA MIGUU ZANZIBAR'?
Mmmmh tanzania hii mmmh wee acha tu
 
Mkubwa usiwe mchoyo wa habari asilani..hebu tumegee hao vijana walimshughulikiaje bibi titi huko 'KIINUA MIGUU ZANZIBAR'?
Mmmmh tanzania hii mmmh wee acha tu

Mkuu huyu bibi keshafika mbele ya haki itakuwa kama kumkashifu...ila kama utaipata faili za ile kesi ya "kizushi" ya uhaini, ameelezea baadhi ya masaibu hayo yeye mwenyewe.
 
... Runinga zilmuonyesha Bibi Titi - wakati huo kesha rudi kundini (CCM) -- kutoa speech ya kumtukuza Nyerere hadi mtu unaweza kutapika. Wengi walitegemea vyema angekuwa upinzani kutokana na masaibu hayo yaliyompata! Upo? let's c lose this topic please!!!!!!!!
its not worth closing lets discuss!
Kauli na yaliyomo rohoni mwake mimi na wewe hatujuwi...Bhoke Munanka, alipoulizwa habari fulani nyeti za huyu bwana katika mambo fulani, alisema "...watu hawajuwi kuna mambo mengi yamepita hapa..." chambilecho ya akina Tambwe Hiza, akiapa kuwa atafia upinzani, may be another day, Bibi Titi hakusema kilicho moyoni mwake.
 
Bi Titi Mohamed alitoa mchango mwingine mkubwa wa kuwafanya wabunge waongee kiswahili bungeni,ni wakati bunge letu lilikuwa linatumia lugha ya kingereza alipodai "The light in the bottle" akiwa na maana ya kudai taa za umeme barabara za magomeni.Bunge likachukua busara ya kutumia lugha inayoweza kutumiwa na kila mmoja.(INASEMEKANA)

Taireeee kijana Mahinda, uzushi huu umeupata wapi?
 
Naye kwa kiasi alicheza katika nafasi yake vizuri,
ndo hivyo tena hao hatunao tena japo mchango wao ni mkubwa katika makuzi ya taifa hili.
Tulikupenda sana Bibi Titi japo uliondoka mapema kabla wengine hatujatoka tongotongo na kuzibuka masikio vizuri.
 
Mkubwa usiwe mchoyo wa habari asilani..hebu tumegee hao vijana walimshughulikiaje bibi titi huko 'KIINUA MIGUU ZANZIBAR'?
Mmmmh tanzania hii mmmh wee acha tu

haaaaah haaaaah haaaah haaaaah umenifanya nicheke dah, machungu ya mgao yamekwisha kwa huu muda mfupi!
Haya Mkuu atupe kweli habari asiwe mchoyo!
 
TUNAPOMKUMBUKA MWALIMU NYERERE



TUMEMSAHAU BIBI TITI BINT MOHAMED?

Kama Mtanzania; basi Bibi Titi bint Mohamed alikuwa namba mbili! Kama ni mwanamke "ngangari" kinoma; Bibi Titi bint Mohamed alikuwa ngangari wa "mapanga shaa shaa"…huyu alikuwa mwanamke aliyejitolea kuipigania nchi yake (Tanganyika) na hatimaye Tanzania.

Hata hivyo, sidhani kama anapewa "nafasi" yake anayostahili!
Ili kuitendea haki historia; na kuweka kumbukizi itakayojenga heshima ya nchi yetu katika kusimamia ukweli na maridhiano kuna kila sababu ya kuweka nafsi kwa wale wote waliyopigania "Uhuru wa Tanganyika" hata kama walikuja kukorofishana na Mwalimu Nyerere.

Unajua historia haiwezi kufichwa kwa gharama ya kuandika "propaganda' na kuwaficha watu kama Bibi Titi bint Mohamed na au kuwatenga kwenye "history of the making". Waandishi, wachambuzi na wapembuzi makini na wanaojali taaluma ya ukweli (na uhalisia) hawana budi kuandika ukweli juu ya mwanasiasa huyu aliyejitolea hali na mali kukiwezesha chama cha TANU kuungwa mkono na wanawake na hata akaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mbunge na waziri kwenye serikali ya Awamu ya Kwanza.


Huu ni ukumbusho kwenu nyote; mnapomkumbuka Mwalimu Nyerere mkumbukeni na Bibi Titi bint Mohamed kwani mchango wake ni mkubwa sana nay eye (Bibi Titi bint Mohamed) sasa ni marehemu anayehitaji kutajwa na kukumbukwa kama mwanaharakati.
 
Huyu mama kama sikosei, waislamu waliwahi kumtumia kutaka kuipindua serikali ya Nyerere miaka ya 60, ghafla akajikuta anawekwa detention!
 
Duuh Tz inakwenda kubaya!mtu kaleta hoja ya historia mtu bila haya anasema udini,tuache ushabiki wa kidin utaupeleka taifa hili kubaya
 
Kuna mtu mmoja ningependa sana kuipata historia yake naye ni Cecil Matola....kuna kipande hiki kuonyesha harakati za Uhuru zilivyoanza...kinasema:- Prospects in Tanganyika were not much better than other territories, as the example of Tanganyia African Association (TAA) reveils. The TAA was founded in Dar-es Salaam in 1929. Under the leadership of Cecil Matola, Kleise Sykes, Mzee Bin Sudi and Ramadan 'Ali, the Association stated its aims as being 'to safeguard the interests of Africans, not only in this territory but in the whole of Africa...
Source:- Bofya

Je, kuna mtu mwenye habari kamili huyu Cecil na hawa waasisi wa Uhuru wetu ambao wamesahaulika baada ya kizazi kipya cha kina Nyerere kuingia..
 
Back
Top Bottom