Bibi harusi atoroka saloon na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba

Pilu ngoja baas nijifanye nimeamini...... Haya basi naomba nijibu hili.... Ina maana Bwana harusi akishauri kumuoa huyo mwanamke yupo tayari kuoa? Mie assumption zangu ni hizi tokana na majibu atatoa..... (take note, naweza kua wrong, hayo ni mawazo yangu)

Kama yupo tayari kumuoa:

  1. Ni mwanaume tegemezi... Yaani mwanadada ana pesa kuliko mwanaume na she is ready to provide. Na sababu jamaa aidha ni mvivu ama tu maisha yamempiga anaona bora tu aoe ili awe guranteed uraisi wa maisha.
  2. Kapenda huyo mwanamke mpaka hajielewi kabisa!
  3. Ni mgeni anahitaji uraia kupitia ndoa.
  4. Sio rijali.... Labda hio ndoa itakua ni picha tu, na wanamakubaliano mdada aweza toka nje once married....

Kama hayupo tayari kuoa....

Hapa kwa kweli ni wazi kua ni vigumu kutaka oa mwanamke alokuadhirisha hivo mpaka jamii yooote ikajua.

Sasa Baaad Pilu naomba tueleweshe....

dier,
kwa mimi njuavyo hio point no.2 inaukweli ila hizo nyingine labda nikafatilie zaidi ili nijue ila kwa upande wa uraia wote na watanzania na bwana harusi ana kazi nzuri tu yenye kipato so sio tegemezi ,pia b.harusi anakazi.
 
Yaah kweli hii itakuwa ya kutunga kwa maelezo ya jamaa kasema kwamba bibi harusi alishapambwa ndiyo akatorola saloon akaenda guest sasa ina maana ndoa haikufungwa siku hiyo pia anatuambia bwana harusi anahitaji msaada wa mawazo kwakuwa anakosa maamuzi na maandalizi ya ndoa yako tayari.
Ndoa ipi sasa wakati haikufungwa na lazima kama haikufungwa lazima itolewe sababu kwa watu ambao wangeuzulia hiyo harusi sasa atwambie waliwapa sababu gani

ndoa ilikua bado ndomani kama ukisoma hio habari vizuri utaona imeelezwa kua mkewe mtarajiwa so nakuomba usome vizuri.
 
yanahitajika maamuzi ya haraka na bwana harusi yuko katika hali ya mshtuko,mchango wako tafadhali.

Anashtuka nini sasa kwani yeye ndio alimtoa bikra?inatakiwa ashukuru kwa kulijua hilo mapem.
 
Sasa mkuu unataka ushauri upi........kama ni kweli hii habari labda mungu amejibu sala za bwana harusi kuhusu mke mwema, Pia kama jamaa akioa labda ni kweli kila mwanamke atapata mume anayemfaa.

Muhimu ni hao maharusi kusikiliza sauti za mioyoni mwao.

NB: Mbona hujibu swali la TB
 
Asee hakuna haja ya
kujifikiria tupa huko
wanawake tupo chungumzima hatuna
wa kutuwowa
kwa maisha yapi haswa
ya kukubali upuuzi huo
wakt ni hatari tupu?
Hata vipomo vya ukimwi hakuna af
ntu achezee life yako
ufe hivihivi shenz
 
Pilu nisamehe kwam nitakukwaza BUT siamini hii habari kwa sababu zifuatazo....

  1. Bibi harusi kaenda na shela guest.... Jamani hivi waelewa karaha ya kuvaa shela let alone kuanza kuzunguka nalo? Kwamba yee ni mjinga kiasi gani aende ku cheat na nguo ambayo kila mmoja lazima amtazame apitapo.
  2. Mwanaume ambae ana cheat na mwanamke wa mtu hasa wa ndoa/anatarajia kufunga ndoa yupo soo makini. Sidhani kama alikua amebanwa saaana kutaka fanya hilo tendo to the extent ya kumpokea bi dada na shela tena guest.
  3. Ni kweli Uchumba/ndoa nyiingi zimekua za kisanii.... but siamini kua watu wahusika huagana karibu na eneo la tukio (in the sense kua vijimtaa vya karibiana saana).
  4. Kwamba bwana harusi anataka ushauri? Huyo mwanaume wa wapi? Bi harusi mtarajiwa afumaniwe ndani ya shela na woote mwajua alafu atake ushauri zaidi ya kubwaga manyanga? Dah! Enways.... Labda utakuja na wapi yameishia...

Dadangu ashadii nakuunga mkono. kwa kuongezea, najua bi harusi anapoenda salun haendi peke yake, anasindikizwa na ndogowe au wifiye au matron wake au wote hao, na mara nyingine wale maids wa harusi. so this story is obviously fake or imaginary.
 
Sasa mkuu unataka ushauri upi........kama ni kweli hii habari labda mungu amejibu sala za bwana harusi kuhusu mke mwema, Pia kama jamaa akioa labda ni kweli kila mwanamke atapata mume anayemfaa.

Muhimu ni hao maharusi kusikiliza sauti za mioyoni mwao.

NB: Mbona hujibu swali la TB

pitia vizuri thread nimejitahi kua makini kwa kujibu maswali yote kwa kadri yatukio lenyewe lilivyo.
Pili, nadhan inawezekana bwa. harusi akawa amejibiwa mapema,
je wadhani b.harusi hana nafasi ya kusamehewa tena?
 
hapana jamani habar ni ya kweli, nakushauri usingoje mpaka yakukute wewe au ndugu yako ndo uamini, binadamu wana mengi,human bebaviour is very complex si rahisi kuijua.

Yani huyo mwanamke hata awe kahaba sug hawezi kufanya ujinga kama huo alafu jinsi usivyoweza kufanya connection ya matukio haiwezekani ndoa iwe inafungwa saa7 or 9 alafu bbie afumwe then bwanaharusi awe anangojea ushauri kutoka kwetu sasa kanisani mchungaji naye anamsubiri tu?
Nyie ndo mnatupikia mpaka research
 
Dadangu ashadii nakuunga mkono. kwa kuongezea, najua bi harusi anapoenda salun haendi peke yake, anasindikizwa na ndogowe au wifiye au matron wake au wote hao, na mara nyingine wale maids wa harusi. so this story is obviously fake or imaginary.

kama nlivomjibu mmoja wa wana jf ni kwamba aliomba kwenda kujisaidia na saluni haikua na toilet na kwajirani kuna gest so alienda toilet ya gest na inavoonyesha b.harusi anaijua vizuri hio saluni na mazingira yaloizunguka.
 
Yani huyo mwanamke hata awe kahaba sug hawezi kufanya ujinga kama huo alafu jinsi usivyoweza kufanya connection ya matukio haiwezekani ndoa iwe inafungwa saa7 or 9 alafu bbie afumwe then bwanaharusi awe anangojea ushauri kutoka kwetu sasa kanisani mchungaji naye anamsubiri tu?
Nyie ndo mnatupikia mpaka research

yani tukio limechanganya mno nakuleta gumzo yani kwatarifa zilizopo sasa ni kwamba ndoa haikufungwa tena na mume mtarajiwa haja sema chochote mpaka sasa kama kasamehe wajipange upya au ndo kamwacha bado hajatoa maamuzi yupo kimnya nyumbani kwake.
 
Asee hakuna haja ya
kujifikiria tupa huko
wanawake tupo chungumzima hatuna
wa kutuwowa
kwa maisha yapi haswa
ya kukubali upuuzi huo
wakt ni hatari tupu?
Hata vipomo vya ukimwi hakuna af
ntu achezee life yako
ufe hivihivi shenz

ndio wadada wapo wengi ambao hawaja olewa mi nadhani tatizo nikujua yupi hatakua na balaa coz kama hao walipendana sana mpaka bw.harusi akaridhika kutangaza ndoa afu ndo yakatokea hayo so atajihakikishia vipi kua akimpata mwingine atakua salama?
 
yani tukio limechanganya mno nakuleta gumzo yani kwatarifa zilizopo sasa ni kwamba ndoa haikufungwa tena na mume mtarajiwa haja sema chochote mpaka sasa kama kasamehe wajipange upya au ndo kamwacha bado hajatoa maamuzi yupo kimnya nyumbani kwake.

Ngojea tuendelee kuvumilia kucheki muvi za kanumba na ray.
 
Acha kudanganya watu harusi gani inafungwa usiku huu? Mbona bado uko jf unajibu thread?
 
Jamani wana jamvi kuna hili limetokea ,bibi harusi amefumaniwa gest ndani ya room tena akiwa amevua shela{gauni la harusi} baada ya kutoroka saloon akiwa anarembwa kwa ajili ya harusi na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba,
kwa bahati mbaya au nzuri mmoja wahudumu wa gest husika alikua anamjua bi harusi huyo kwani na yeye alitarajia kuhudhuria hio harusi ndipo akatoa taarifa kwa ndugu wa bi harusi kwa kua hakufurahishwa na hilo, kwa hio watu wachache upande wa bi harusi na mmewe mtarajiwa ndo wamejua hilo tukio,mme yuko njia panda kwani maandalizi yote yalishakamilika na hata ndugu wa mbali washafika kwajili ya harusi.

Tumshauri bwana harusi afanyeje au achukue uamuzi gani kuhusu harusi?

Dawa iko wazi ni kuachana naye. Afanye mambo mengi ya maana. Atafute msichana ingawa amepoteza pesa zake.
 
Jamani wana jamvi kuna hili limetokea ,bibi harusi amefumaniwa gest ndani ya room tena akiwa amevua shela{gauni la harusi} baada ya kutoroka saloon akiwa anarembwa kwa ajili ya harusi na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba,
kwa bahati mbaya au nzuri mmoja wahudumu wa gest husika alikua anamjua bi harusi huyo kwani na yeye alitarajia kuhudhuria hio harusi ndipo akatoa taarifa kwa ndugu wa bi harusi kwa kua hakufurahishwa na hilo, kwa hio watu wachache upande wa bi harusi na mmewe mtarajiwa ndo wamejua hilo tukio,mme yuko njia panda kwani maandalizi yote yalishakamilika na hata ndugu wa mbali washafika kwajili ya harusi.

Tumshauri bwana harusi afanyeje au achukue uamuzi gani kuhusu harusi?
old z gold huh.
cha mwisho mwisho jaman teh.
 
too fictional hii....
hebu sema harusi ilikuwa ifungwe kanisa lipi?
na mchungaji yupi?
ukumbi upi mmekodi kwa sherehe???????
Is is of a bad taste to make us discuss an imaginary situation...I agree with you Boss this is made out of "the mill and boom"
 
aliendaje msalani na gauni? Haiwezekani kwenda peke yake lazima asaidiwe, kawaida gauni huwa zito,na lisipokuwa zito urefu wake lingeburuzika,lazima aende na mtu.

Hizi tantalila tu!

Tulipo muuliza mdada wa saluni yani nkimaanisha yule fundi mwenyewe akatuambia kua B. harusi aliomba akajisaidie baati mbaya hio saluni haikua na toilets so alielekea gest ambayo haiko mbali na saluni ili kujisaidia toilets katika toilets za gest na kumbe ndo ivo yaonyesha kama walishapanga mchezo na huyo mpenziwe wa zamani kukutana huko .
 
Ahsanteni sana kwa michango yenu nyote mlochangia {ndo twatoka kwenye kikao cha tathmini na maamuzi kwa yaliyotokea}.
ingawaje wengi hamkutaka kuamini yalotokea mkidhani ni hadithi tu, sina namna yakuwafanya muamini hilo labda siku mkikutana na hayo ndo mtajakumbuka{ingawaje siwaombei yawakute coz inaumiza sana} kwani haya yanatokea humuhumu duniani kama ilivotokea kwa huyu ndugu yetu, ni vema mjue watu wameharibika kimaadili naamini mifano mnayo mingi katika hili, ni vema tuache masihara katika mambo yanayo hitaji msaada wb haraka kama haya.

MWISHO; pamoja na mengi yalo jadiliwa na kufanyiwa maamuzi,bwana harusi naye ameamua kumsahau{kumwacha} kabisa mpenziwe,
upande wa b.harusi kutakapo kucha tu nduguze wameamua akaishi mkoa mwingine kwa mama mdogo wake, hivyo bw.harusi apumzike apate mwelekeo mpya.
Niwashukuru tena wana jf kama, "flora msoffe, Navoyne,AshaDii,Kichomiz, Obsesd na wengineo kwa michango yenu na Mbarikiwe sana!

Kheri ya mwaka mpya!
 
Hii habari mbona imekaa kama ya kidaku? kwa uelewa wangu bibi harusi siku ya harusi wala hapati muda wa kwenda hata kununua vocha. kila kitu anafanyiwa. issue ya kutoroka na shela na gauni la harusi nimelipinga, matron alikuwa wapi na je wote waliombatana nae walikuwa wapi? au utuambie hiyo saluni iko ndani ya hiyo guest.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom