Bibi harusi ajifungua kanisani

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Hii hali imetokea maeneo ya Muheza bibi harusi alishikwa uchungu kanisani na kujifungua wkt ibada ikiendelea.

Mwandishi Wetu, Muheza
BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.
Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/3...usi-ashikwa-uchungu-ajifungua-kanisani-muheza

mi huwa sielewi kabisa hii habari! utafurahiaje harusi yako ukiwa mjamzito kiasi hicho? na wachungaji wa siku hizi wanapotezea utasema hawaoni! enzi za mwalimu hufungishwi ndoa hadi ujifungue kwanza! eeh,hongera zake!

Tatizo wanaume wanapenda kujaribu kwanza je anadaka kama hadaki anamtema

hakuna lolote, visingizio tu! ya mungu mengi, atajifungua huyo mtoto bahati mbaya afariki. na kupata mtoto wa pili iwe kimbembe! watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, na anaweza chukua anytime.
haya sasa, kajaribu na imekubali. sasa ndo wasubiri miezi yote hiyo kufunga ndoa? si wangefunga chapchap! show zote za nini, unazaa mbele ya babako na kadamnasi nzima? mweeh! wengine tuko too conservative i guess...

Tatizo wanaume wanapenda kujaribu kwanza je anadaka kama hadaki anamtema

Wewe hukufanya kabla ya ndoa? Una bahati mlifunga ndoa hajanasa. Angemtapikia pastor kwa kichefux2 cha mimba

Hii imenikumbusha harusi flan nilihudhuria miaka ya nyuma. Ilikuwa inapelekwa fastafasta, saa 1 jioni maharusi wakaondoka wakatuacha tunaendelea kugonga mvinyo. Kwenye saa 2 usiku, mc akatutangazia kwamba bibi harusi amejifungua salama, mtoto wa kiume!

Wewe hukufanya kabla ya ndoa? Una bahati mlifunga ndoa hajanasa. Angemtapikia pastor kwa kichefux2 cha mimba

Saa zingine tunayataka wenyewe......kukamata ujauzito kabla ya ndoa na mtu huyo huyo utashangaa eti atafanyiwa kicheni pati na send-off na bridal shower prior the big wedding in a white gown.....damn!! tumepoteeza kabisa maadili.

Zaa kwanza then ubariki hiyo ndoa wala sio kufunga tena maana mpaka mmeshapata mtoto ni zaidi ya uchumba

Hii imenikumbusha harusi flan nilihudhuria miaka ya nyuma. Ilikuwa inapelekwa fastafasta, saa 1 jioni maharusi wakaondoka wakatuacha tunaendelea kugonga mvinyo. Kwenye saa 2 usiku, mc akatutangazia kwamba bibi harusi amejifungua salama, mtoto wa kiume!

Hii kali...

Afadhali kama walikuwa wameshavalishana pete, huo ndo utandawazi, siku hizi kutest kwanza. Hongera yao, na possibly mtoto atakuwa mtumishi wa Mungu.

Hii imenikumbusha harusi flan nilihudhuria miaka ya nyuma. Ilikuwa inapelekwa fastafasta, saa 1 jioni maharusi wakaondoka wakatuacha tunaendelea kugonga mvinyo. Kwenye saa 2 usiku, mc akatutangazia kwamba bibi harusi amejifungua salama, mtoto wa kiume!

Bi shaka walikuwa ktk usomaji mzuri wa alama ya nyakati.

hakuna lolote, visingizio tu! ya mungu mengi, atajifungua huyo mtoto bahati mbaya afariki. na kupata mtoto wa pili iwe kimbembe! watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, na anaweza chukua anytime.
haya sasa, kajaribu na imekubali. sasa ndo wasubiri miezi yote hiyo kufunga ndoa? si wangefunga chapchap! show zote za nini, unazaa mbele ya babako na kadamnasi nzima? mweeh! wengine tuko too conservative i guess...

Maandalizi yalichelewa si unajua tena mpaka ujipange

Back
Top Bottom