Biashara ya viwanywaji vya jumla-ushauri

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,528
12,365
Wana JF habari za Jumapili!
Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo

Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani gin, grands, wine na jamii zake.

Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!

Karibuni kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom