Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao. Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!
Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasas kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 . Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri.
Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700. Ndugu mwanajamvi hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo.
Huwa najiuliza, hili jamvi ni la kutuma hoja nzito au pumba? Hv kweli unapoteza mda wako kutuma ujumbe kwenye jf the home of great thinkers kuwa unatafuta kuku wa kienyeji!!! Embu acha utani ww.
mimi nataka kuku wa kienyeji wa kula..nitapata wapi?niko Dar.
Mtoa hoja yuko sahihi kabisa,yawezekana hata wewe kuku anaowatafuta huwajui. Elimu juu ya kuku wa kufuga ni pana zaidi ya wengi tujuavyo,si suala la kuona kuku mitaani ktk vibanda ukadhani ndio ufugaji.
La msingi ni hili, kuku wa kienyeji na wazuri pamoja na size nzuri ni kuchi, hawa hupatikana kanda ya kati na kisiwani Mafia, kuku wafupi wa kiluguru ni wazuri kwa mayai na kutunza watoto, hawa wapo wengi Mlimba/kilombero.
Kwa biashara inayoweza kututajirisha ni kuku tu!!!!, sasa wote tukiuza kuku nani atatuuzia kilauri na kitimoto, si tutapata shida!
Halafu hizi dvd na vitabu si ni njia tu ya kufikisha ujumbe kama ujumbe huu ulivyonifikia kwa kupitia ka smartphone kangu, kwa hisani ya JF, au dvd na vitabu zina alergy (sijui nimepatia?) na utajiri?
Afu wamesemaje vilee! ... Eeeh eti kuku wa kisasa ni mataahira, mimi ndio leo nimejua, ninachoshangaa zaidi ni nini kimewafanya hawa kuku wa kisasa wakawa mataahira?
Haya ni maelezo mafupi ya jinsi ya kuandaa dawa ya Alovera. Kata majani 3 hadi 5 makubwa. Kata vipande vidogo vidogo kisha lweka kwenye maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kwa siku 5 hadi 7 isiyotumika mwaga. Hii dawa ni nzuri sana kuzuia magonjwa ya Kideri, homa ya matumbo, kifua ngozi na Cholera. Maji haya pia ni tiba nzuri kwa ng'ombe (Fuatilia zaidi kwa mtaalam wa mifugo aliye karibu nawe.
Mkuu nimependezwa sana na article ulizoleta hapa Javini na namna unavyo jibu haraka, Mwanzo nilijua unakandia sana watu wasisome hivyo vitabu vya inspiration vya akina Robert Kiyosaki (Rich Dad and Poor Dad, Guide to Investments, The Cash flow quadrant,.....n.k); Napolean Hill (Think Big and Grow Rich); Jack Canfield (The Success Principle, The Chicken soup of the sour); The Baron Son, The Richest man in Byblon, The Millionaire Mind set (Gerry Robert); Gifted Hand and Think Big (Dr. Ben Cansons); and many others.
Ni kweli hapa tunahitaji zaidi practical, but how! kwanza unahitaji upate the theory behind ndio uanze na kufanya practical, ingawaje watu wengine wanachallege sana hivyo vitabu na kusema havitoi picha halisi ya mazingira ya kwetu, vinaangalia mazingira ya U.S.A and Europe kuliko Africa/East Africa specificaly Tanzania. Tukipata watu wanaweza kutuletea Historia za watu kama akina Backresa, Mengi, Rostam Aziz, Edward Lowasa, wale Wahindi wanye pesa nyingi wale wanao jenga jengo la Umoja wa vijana(Estem). Tukapata historia zao njisi walivyopata utajiri wao! inaweza kutu inspire sie na kujua njia halisi wanazotumia kupata pesa.
Je kweli wanaanza na ufugaji wa kuku kama unavyosema GAZETI?? au kuna njia zingine short cut wanatumia kufikia huko??

Mkuu kwa hapa bongo short-cut ni kuingia kwenye siasa na kuwa sehemu ya mtandao wa ufisadi, hao uliowataja nafikiri kikubwa walichofanya ni hicho! Bongo majambazi ndio yenye nafasi ya kutajirika kwa haraka!