Asante Mkuu kwa mchanganuo huu, Je wewe umeshaanza kufuga au unaelezea nadharia? Katika uwekezaji au biashara yeyote kuna changamoto zake, kwa hiyo usijekuingia katika uwekezaji au biashara kwa mahesabu haya; mambo yakienda tofauti unaweza kukata tamaa. Unaweza kuona ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi, lakini siyo rahisi kama wengi wamavyofikiria (kwa uzoefu wangu).

Nami nilikuwa na mahesabu kama haya nikanunua kuku zaidi ya 35, lakini zilianza changamoto za magonjwa na walibaki wachache sana. Unaweza kusema tumia dawa. Kwa sasa kuku wa kienyeji nimeweka kwa ajili ya matumizi binafsi lakini kwa biashara niliamua kufuga kuku wa nyama (broiler). Nimetoa comment kutokana na uzoefu niliopata lakini wengine wanaweza kuwa na uzoefu wa tofauti na michango zaidi inaweza kutolewa.
 
naona umeignore gharama za kutengeneza banda la hao kuku (250,000 haitoshi)

Ni kweli unachozungumza lakini nilichokua natoa hapo ni kama dira tu jinsi kuku wanavyoweza kuwa mtaji muhimu. Ujenzi wa banda na mahitaji mengine yanategemea na mahali ulipo, Mtu aliye kijijini au mwenye shamba ana nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.jambo muhimu kuhusu gharama za kujenga banda linategemea zaidi na changamoto za mahali ulipo.

Mfano Mtu wa Dar atatakiwa kujenga banda ambalo licha ya kuwaweka kuku katika hali nzuri pia atatakiwa aangalie jinsi ya kuwalinda kuku hao na wezi. Wako ambao watakabiliwa na changamoto za mwewe na kadhalika. Mwisho nimetoa ushauri watu wafanye utafiti zaidi kwani mimi naweza kueleza lakini nikawapoteza kulingana na utofauti wa jiografia ya mahali niliko.
 
Wazo zuri mkuu, but naona kama 1m inaweza kuwa ndogo kama utainclude operating costs kwa hiyo project!
 
Asante Mkuu kwa mchanganuo huu, Je wewe umeshaanza kufuga au unaelezea nadharia? Katika uwekezaji au biashara yeyote kuna changamoto zake, kwa hiyo usijekuingia katika uwekezaji au biashara kwa mahesabu haya; mambo yakienda tofauti unaweza kukata tamaa.

Unaweza kuona ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi, lakini siyo rahisi kama wengi wamavyofikiria (kwa uzoefu wangu). Nami nilikuwa na mahesabu kama haya nikanunua kuku zaidi ya 35, lakini zilianza changamoto za magonjwa na walibaki wachache sana. Unaweza kusema tumia dawa. Kwa sasa kuku wa kienyeji nimeweka kwa ajili ya matumizi binafsi lakini kwa biashara niliamua kufuga kuku wa nyama (broiler). Nimetoa comment kutokana na uzoefu niliopata lakini wengine wanaweza kuwa na uzoefu wa tofauti na michango zaidi inaweza kutolewa.

Asante mkuu kwa sasa mimi sio mfugaji lakini nimeshawahi kufuga na kupata faida kubwa sana kutokana na kuku. Ni kweli kuna changamoto za magonjwa lakini kama utapata ushauri kwa mtaalamu wa mifugo aliyeko karibu nawe utagundua wazi kuwa si kitu cha kuogopa.

Kwa upande wangu kipindi hicho nilichokuwa mfugaji nilikuwa natumia dawa ya asili, kuna majani ambayo nilikuwa naletewa na mtaalamu mmoja wa tiba za asili ambayo yanatwangwa na kuchanganywa kwenye maji ya kuku amini wanakuwa hawasumbuliwi na magonjwa. Si nia yangu kukuelekeza dawa hiyo kwa ni siku nyingi kidogo zimepita ila ninachokushauri onana na mtaalamu wa Mifugo.

Napenda kukufahamisha kuwa mimi nilianza na kuku watano tu lakini ndani ya miaka mitatu nilikuwa mbali sana.
 
Mada nzuri,ila hujazungumzia masoko. Kuzalisha ni kitu kimoja mauzo na gharama za uzalishaji ni vitu vya msingi pia kujua.
 
Ndio tatizo la watanzania vitu vya msingi tunaleta utani mwingi, ametoa dira not necessarily ufuge unaweza umuulize other activity, cost analysis, market na mambo mengine, lets be positive once in atime, nashukuru mimi ni mfugaji wa kuku wa mayai ya kizungu ila wa kienyeji nilikuw nao pia wakafa sana nikakata tamaa, labda kama kuna mtu anafahamu dawa za kuwastustain mbali na zile chanjo zao.
 
Mada nzuri,ila hujazungumzia masoko. Kuzalisha ni kitu kimoja mauzo na gharama za uzalishaji ni vitu vya msingi pia kujua.

Swali zuri na rahisi. Bado tunarudi kulekule kwa waliotangulia inabidi ufanye utafiti wa soko kulingana na eneo ulilopo kwani sina uhakika sana kama kuna maeneo hawapendi nyama ya kuku wa kienyeji katika nchi hii. Nasema sina uhakika kwani nilishawahi kusikia watu fulani hawapendi samaki lakini kuku bado!
 
Wazo zuri mkuu, but naona kama 1m inaweza kuwa ndogo kama utainclude operating costs kwa hiyo project!

Kitu kimoja inabidi ufahamu ndugu yangu, utafika wakati ambao huo mradi itabidi ujiendeshe wenyewe. Usiogope haihitaji sana elimu ya darasani kujua kwamba lazima kuna kiasi fulani cha kuku utalazimika kuwauza ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji.

Kama uko Mjini haraka sana rudi kijijini ukaanzishe hako kamradi katakutoa kwani yawezekana ugumu ukatokana na uwepo wako wa Mini. "MWANAFUNZI anatakiwa asikilize,atafakari, achunguze na kudadisi na atoe maoni yake na sababu za maoni hayo.Kisomo ambacho kinamfanya mtu aone tabu kurudi vijijini si kisomo bali ni mapambo. Kupata shahada ni matokeo tu na si msingi wa elimu ya chuo kikuu " Julai 4 1977 Ibrahim Kaduma, Aliyekuwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho mwaka huo. Kaduma pia aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania wakati wa mwalimu nyerere. Chanzo RAIA MWEMA Febr. 2 - 8
 
WADAU NIMETAMANI KUFUGA KUKU WA KIENYEJI NAOMBA MNISAIDIE WANAPATIKANA WAPI KWA WINGI NA WASIO NA MAGONJWA

tafadhali
 
Mkuu jama kapotea lakini wengi tunania ya kufuga hao kuku wa kienyeji walio bora kwa mtu wa dar utamsaidiaje
 
Kwa hesabu ya mtoa mada, jaribu uone mziki wake, jamaa hakusema vifaranga wangapi watakufa, gharama za dawa kwa kuku. Kideli kiki ingia kwenye banda lako, utakimbia! Heasbu haziendi hivyo la sivyo kila mtu angekuwa millionea!
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom