CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,789
- 8,914
Mkuu Chasha hiyo ni breaking news kwenye industry ya kuku! Hao kuku uliosema huo utagaji ni super!
Kusema ukweli kwa upande wangu hadi sasa kuku wa Malawi a.k.a kuku wa kienyeji ndiyo wamekuwa wakishikilia rekodi ya mayai 80 kwa mwaka! Mimi binafsi sijawahi kufuatilia kiukweli idadi ya utagaji kwa mwaka bali matokeo ya utafiti wa kuku wa kienyeji yanaonyesha kuwa kuku anaenyang'anywa vifaranga baada ya kutotoa huwa na mizunguko 6 ya utagaji kwa mwaka hapo ni mayai 60 hadi 70. Kwa utaratibu wa kutotolesha kwa mashine tukichukulia kuwa kuku akimaliza kutaga mzunguko mmoja unayachukua mayai yake yote asipate kuatamia atakaa siku 10 kabla hajaanza kutaga upya mzunguko mwingine. Kwa hiyo siku 10 za kupumzika kutaga ukijumlisha na siku 15 za kutaga mayai 13 (maana hatagi kila siku) ni jumla ya siku 25 yaani ni karibia mwezi mmoja! Kwa wastani tunaweza kuchukulia kuku wa kienyeji mtagaji mzuri kila mwezi utaokota mayai 13 (wastani) zidisha kwa miezi 12 ni sawa na mayai 156! Ingawa inahitajika kutafiti ili kupata idadi halisi ya mayai ya kuku wa kienyeji kwa mwaka ninaimani idadi haiwezi kucheza mbali sana na hapo maana kuku wa kienyeji tuliowazoea huwa wanapumzika siku kadhaa baada ya kumaliza mzunguko mmoja kabla hawajaanza tena kutaga.
Kwa maneno mafupi ni kwamba hao kuku wa Kenya wanaotaga mayai 280 kwa mwaka utagaji huo kwa kuku wa kienyeji kiwango ni cha juu sana. Kiwango cha utagaji wa kuku wa mayai kwa mwaka kinachokubalika ili kupata faida nadhani ni zaidi ya mayai 300 (watatusaidia wataalam wa mifugo). Kuku asiyefikia idadi hiyo hakubaliki kama kuku wa mayai.
Mkuu nafuatilia na Baada ya Uchaguzi naweza Tia Timu Huko kwa ajili ya Kununua Vifaranga wake na nitaarifu, Ila tatzio linakuja kwenye kuwavusha make nasiki ni lazima upewe kibali na wizara ya Mifugo na wizara zetu zilivyo na urasimu si dhani, Ila naweza fanya kila njia kuwavusha Namanga Boda