Kubota; Kubota; Kubota;

Uko cha wapi Mkuu?
Hebu rudi jukwaa lengwa tunakusubiria sana tu!

Mama Joe & Mama timmy jamani mwenye nambari ya huyu mjasiriamali mwenzetu na ampigie tu amwambie maoni yake mengi tunayasubiribia hapa!

Wakubwa nipo jamani, ila Mama Timmy ameadimika au anasakanya sungura wametoroka? Mama Timmy nachemsha mchuzi huonekani mwishowe utakauka njoo unywee!!
 
newcastle au mdondo wanapewa siku za mwanzo ila wengi tunaanza na vitamin kuvipa nguvu si unajua vinakuwa dhaifu. Pia ukiweka maji jitaidi iwe ulitoa vyombo mfano asubuhi sana ukawaacha wale wakipata kiu unaweka chanjo kama saa tatu ili wote wanakuwa na kiu unayaacha masaa 2 unatoa unaweka ya kawaida na vitamin. Jitaidi kuwasogeza wote wanywe dawa. Baada ya wk tatu unarudia tena.

Safi sana yaani very practical hadi rahaaa.
 
Mkuu Kubota vipi kuhu Utagaji wa Kuku wa Kienyeji kwa mwaka? Nauliza hivyo kwa sababau Kenya kuna Aina ya Kuku wapya wa Kienyeji ambao wanataga kuliko hata Kuku wa Kisasa kwa mujibu wa Maelezo ya Ile taasisi wanataga Mayai hadi 280 kwa mwaka, kiwango ambacho wanadai ni kikubwa kuliko hata kuku wakisasa wa mayai, Naifutilia Mbegu yao, make niliwasiliana nao wakanimbia vifaranga vinapatikana ila ni ghali sana ingawa na Fertilized eggs yapo pia, so nasubilia Uchaguzi umalizike ili niwaibukie ninunua hivyo vifaranga wa hao aina mpya ya kuku wa Kienyeji, na si kwama imecrosiwa no ni pure Indegenous, na pia kuna Kuku wa Kieneyeji kutoka Isaraeli nao nawafuatilia huko huko
 
nimeshangaa aina hii ya kuku ,yaani wanataga kuliko wa kisasa!, nitafurahi kusikia toka kwako pindi ukiwanunua , niweze fahamu bei na wauzaji
 
Ndiyo maana ninaipenda Jf kila kitu unapata humu! Kubota umewahi kusikia ama kuona hii? Chasha tunakutegemea kwa hili Ndg yetu!

Mkuu Kubota vipi kuhu Utagaji wa Kuku wa Kienyeji kwa mwaka? Nauliza hivyo kwa sababau Kenya kuna Aina ya Kuku wapya wa Kienyeji ambao wanataga kuliko hata Kuku wa Kisasa kwa mujibu wa Maelezo ya Ile taasisi wanataga Mayai hadi 280 kwa mwaka, kiwango ambacho wanadai ni kikubwa kuliko hata kuku wakisasa wa mayai, Naifutilia Mbegu yao, make niliwasiliana nao wakanimbia vifaranga vinapatikana ila ni ghali sana ingawa na Fertilized eggs yapo pia, so nasubilia Uchaguzi umalizike ili niwaibukie ninunua hivyo vifaranga wa hao aina mpya ya kuku wa Kienyeji, na si kwama imecrosiwa no ni pure Indegenous, na pia kuna Kuku wa Kieneyeji kutoka Isaraeli nao nawafuatilia huko huko
 
Last edited by a moderator:
Wakubwa nipo jamani, ila Mama Timmy ameadimika au anasakanya sungura wametoroka? Mama Timmy nachemsha mchuzi huonekani mwishowe utakauka njoo unywee!!
Kubota ndugu yangu ulituweka sana wadau!wewe kila siku ni kuchoma mkaa!mwisho wa siku miti itakwisha.nipo ila majukumu ya kifamilia yalinibana.nimerudi na nimefurahi kukuta mchuzi ni wa moto sasa ni kunywa tu!twende kazi
 
Kubota asante sana barikiwa nimejifunza mengi kuhusu kuku wa kienyeji mpaka sasa, endelea kutujuza mengine pia hasa security, ila uache nyara za serikali ukikamatwa mbaya sana

Asante nitazingatia ushauri Mama Joe, kuhusu security nitakusimulia tu nilivyojilinda dhidi ya maadui pori!
 
Mkuu Kubota vipi kuhu Utagaji wa Kuku wa Kienyeji kwa mwaka? Nauliza hivyo kwa sababau Kenya kuna Aina ya Kuku wapya wa Kienyeji ambao wanataga kuliko hata Kuku wa Kisasa kwa mujibu wa Maelezo ya Ile taasisi wanataga Mayai hadi 280 kwa mwaka, kiwango ambacho wanadai ni kikubwa kuliko hata kuku wakisasa wa mayai, Naifutilia Mbegu yao, make niliwasiliana nao wakanimbia vifaranga vinapatikana ila ni ghali sana ingawa na Fertilized eggs yapo pia, so nasubilia Uchaguzi umalizike ili niwaibukie ninunua hivyo vifaranga wa hao aina mpya ya kuku wa Kienyeji, na si kwama imecrosiwa no ni pure Indegenous, na pia kuna Kuku wa Kieneyeji kutoka Isaraeli nao nawafuatilia huko huko

Mkuu Chasha hiyo ni breaking news kwenye industry ya kuku! Hao kuku uliosema huo utagaji ni super!
Kusema ukweli kwa upande wangu hadi sasa kuku wa Malawi a.k.a kuku wa kienyeji ndiyo wamekuwa wakishikilia rekodi ya mayai 80 kwa mwaka! Mimi binafsi sijawahi kufuatilia kiukweli idadi ya utagaji kwa mwaka bali matokeo ya utafiti wa kuku wa kienyeji yanaonyesha kuwa kuku anaenyang'anywa vifaranga baada ya kutotoa huwa na mizunguko 6 ya utagaji kwa mwaka hapo ni mayai 60 hadi 70. Kwa utaratibu wa kutotolesha kwa mashine tukichukulia kuwa kuku akimaliza kutaga mzunguko mmoja unayachukua mayai yake yote asipate kuatamia atakaa siku 10 kabla hajaanza kutaga upya mzunguko mwingine. Kwa hiyo siku 10 za kupumzika kutaga ukijumlisha na siku 15 za kutaga mayai 13 (maana hatagi kila siku) ni jumla ya siku 25 yaani ni karibia mwezi mmoja! Kwa wastani tunaweza kuchukulia kuku wa kienyeji mtagaji mzuri kila mwezi utaokota mayai 13 (wastani) zidisha kwa miezi 12 ni sawa na mayai 156! Ingawa inahitajika kutafiti ili kupata idadi halisi ya mayai ya kuku wa kienyeji kwa mwaka ninaimani idadi haiwezi kucheza mbali sana na hapo maana kuku wa kienyeji tuliowazoea huwa wanapumzika siku kadhaa baada ya kumaliza mzunguko mmoja kabla hawajaanza tena kutaga.

Kwa maneno mafupi ni kwamba hao kuku wa Kenya wanaotaga mayai 280 kwa mwaka utagaji huo kwa kuku wa kienyeji kiwango ni cha juu sana. Kiwango cha utagaji wa kuku wa mayai kwa mwaka kinachokubalika ili kupata faida nadhani ni zaidi ya mayai 300 (watatusaidia wataalam wa mifugo). Kuku asiyefikia idadi hiyo hakubaliki kama kuku wa mayai.
 
Namshukuru Mungu kuku wangu watatu wameanza kutotoa leo.Changamoto ya magonjwa ndio wasiwasi wangu. leo jogoo nimeona linatoa kinyesi chenye maji mengi sijui kama ndo linaharisha kama unavyona pichani! wasiwasi ni kwa vifaranga kuambukizwa. nategemea nikawatoe wote kwa mama zao. nimpatie dawa gani huyo jogoo na kuwakinga vifaranga?
 
Attachments

  • IMG-20130228-00175.jpg
    IMG-20130228-00175.jpg
    127.4 KB · Views: 539
  • IMG-20130228-00177.jpg
    IMG-20130228-00177.jpg
    133.6 KB · Views: 509
  • IMG-20130228-00183.jpg
    IMG-20130228-00183.jpg
    82.6 KB · Views: 487
  • IMG-20130228-00182.jpg
    IMG-20130228-00182.jpg
    62.2 KB · Views: 422
Hongera kwa kupata vifaranga nakushauri uwatenge na kuku wengine kama hutaweza waache na mama yao wawape joto. anza kama alivyoshauriwa LiverpoolFC jana ila nenda na dalili hizo za jogoo famasi wakupe dawa. Mtenge pekee na osha vyombo kwa dawa. Ungeanza na mdondo kama unawasiwasi na dawa nyingine za vifaranga utapewa famasi. Keep it up
 
Naaaaam Mama Joe hakika kuku wote wanne wametotoa na ingali wameanguliwa kwa kutofautiana ama kupishana siku ila hakika wote wametotolewa na kuna aliyeacha mayai kama matatu na mama zao nimewatupia majogoo wakae nao huko katika banda lingine ila sijui kama nitakuwa nimekosea sijui ila kwa kuwa tupo pamoja hakika tutarekebishana na Kubota nakuomba sana pitia huku kwani umezidi kuwa busy na magogo huko ulipo!

Hongera kwa kupata vifaranga nakushauri uwatenge na kuku wengine kama hutaweza waache na mama yao wawape joto. anza kama alivyoshauriwa LiverpoolFC jana ila nenda na dalili hizo za jogoo famasi wakupe dawa. Mtenge pekee na osha vyombo kwa dawa. Ungeanza na mdondo kama unawasiwasi na dawa nyingine za vifaranga utapewa famasi. Keep it up
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru Mungu kuku wangu watatu wameanza kutotoa leo.Changamoto ya magonjwa ndio wasiwasi wangu. leo jogoo nimeona linatoa kinyesi chenye maji mengi sijui kama ndo linaharisha kama unavyona pichani! wasiwasi ni kwa vifaranga kuambukizwa. nategemea nikawatoe wote kwa mama zao. nimpatie dawa gani huyo jogoo na kuwakinga vifaranga?

guta kuwa makini na vifaranga maana naamini masharti ya mahitaji yao ukifuatilia kwa makini hakika hafi hata mmoja!
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru Mungu kuku wangu watatu wameanza kutotoa leo.Changamoto ya magonjwa ndio wasiwasi wangu. leo jogoo nimeona linatoa kinyesi chenye maji mengi sijui kama ndo linaharisha kama unavyona pichani! wasiwasi ni kwa vifaranga kuambukizwa. nategemea nikawatoe wote kwa mama zao. nimpatie dawa gani huyo jogoo na kuwakinga vifaranga?

Mkuu Guta hapo umecheza vizuri sana kuongea kwa picha, hongera kutotolesha, sasa wewe na LiverpoolFC ndiyo muanzishe kutekeleza kwa vitendo mliyoona yanawafaa kwenye hii thread, endeleeni kutoa mshindo nyuma. Guta huyo jogoo kama ulishamrambisha dawa ya mdonde wewe usihofu huyo ni kuku wa kienyeji tena ni jogoo, kama anapata fursa ya kuchunga majani hiyo itapita tu, huo uharo mbona ni kawaida tu, hofu kwa kuku wa kienyeji mkuu iko kwenye vifaranga na VINYOYA! Picha zinaongea maneno alfu moja kuliko kuandika, asante sana kuturushia picha!
 
Naaaaam Mama Joe hakika kuku wote wanne wametotoa na ingali wameanguliwa kwa kutofautiana ama kupishana siku ila hakika wote wametotolewa na kuna aliyeacha mayai kama matatu na mama zao nimewatupia majogoo wakae nao huko katika banda lingine ila sijui kama nitakuwa nimekosea sijui ila kwa kuwa tupo pamoja hakika tutarekebishana na Kubota nakuomba sana pitia huku kwani umezidi kuwa busy na magogo huko ulipo!

Mkubwa LiverpoolFC hapo kwenye red juu umeniacha hoi mbavu zinaniuma kwa kucheka! Mimi mbona niko full hapa ninakufuatilia kwa karibu sana. Wewe na Guta msituangushe hao vifaranga hakikisheni wanakua wote. Nunueni chick marsh hata kama ni ya kupima kwa kilo! Fainali ya ufugaji wa kuku iko mwanzoni, ni kukuza vifaranga. Siku mtakapokuwa na mechi na kina Arsenal na wengine usijisahau kuwachungulia chungulia vifaranga wako.
 
Hongera kwa kupata vifaranga nakushauri uwatenge na kuku wengine kama hutaweza waache na mama yao wawape joto. anza kama alivyoshauriwa LiverpoolFC jana ila nenda na dalili hizo za jogoo famasi wakupe dawa. Mtenge pekee na osha vyombo kwa dawa. Ungeanza na mdondo kama unawasiwasi na dawa nyingine za vifaranga utapewa famasi. Keep it up

Mama Joe nashukuru sana kwa kuokoa jahazi kwa majibu yako kwa mdau. Yaani unajua ninavyobimbilika na magogo yangu huko porini nachelewa kujibu hoja. Kwa kweli udumu sana maana bila hivyo LiverpoolFC karibu atakuja kunitoa kwenye matanulu yangu. LiverpoolFC ukitaka kuja huku uwe makini usije ukanaswa na mitego, huku kuna miradi mingi.
 
Back
Top Bottom