Biashara ya Siasa Tanzania isiyo na VAT

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Tafsiri ya siasa ya kale na yaleo bado inarandana, hasa ikitazamwa kama ni shughuli za kujitolea zenye sura ya harakati za ukombozi,

Takribani miongo mitano sasa, siasa za Tanzania zimejihuisha nakuwa za kimageuzi, tena yakipekee kabisa.
Siasa za muongo wa kwanza ni tofauti sana na siasa za muongo huu wa tano kwa ardhi yetu ya Tanganyika na Zanzibar,

Hili linachipuza katika kipindi ambacho kwa hakika siasa ya dunia ina geuka kwa kasi sana ambapo hata mezani pawajiitao waasisi wa DEMOKRASIA duniani pamekuwa na mikingamo hasa dhana ya matumizi ya pesa katika siasa duniani.

Dhana ya matumizi ya PESA katika siasa yoyote ile duniani hubeba sura moja tena pembuzi na huru, mathalani, Pesa ikuwezeshe mwanasiasa na waambata wako kusafiri na kuyafikia maeneo husika ya kisiasa, Pesa iwasaidie wewe mwanasiasa na waambata wako kwa kula na kulala muwapo kwenye shughuli za kisiasa, Pesa iwasaidie kulipia matangazo kwa vyombo vya habari ili kuzitangaza siasa zenu.

Aghalabu Amerika, Ulaya Magharibi, Ulaya Mashariki, Asia na Kusini mwa Amerika Matumizi ya pesa katika siasa yamekuwa na maelezo stahiki pindi ikihitajika mbele ya umma.

Mwaka 1997 katika masimulizi ya kawaidi nilimuuliza Hayati Mzee Julius Nyerere swali moja la kizushi, “Baba hivi ulipata wapi pesa za kugombea urais?” Mwalimu aliniangalia kwa zaidi ya sekunde kumi hivi kisha akanijibu,

“Watanzania walinipa mioyo yao, waliniamini, hivyo hakukuwa na njia ya kuwaaminisha watu kwa PESA ndipo wakupe dhamana ya kuwaongoza, na siku ikifika hivyo mwanangu elewa kuwa Taifa linayumba”

Leo hii katika siasa za Tanzania tunashuhudia bajeti kubwa za kisiasa ambazo wanasiasa wanaamua kwa makusudi kuwekeza katika siasa, na bila ajizi anakuja kuvuna zaidi ya mara kumi ya alichowekeza tena haikatwi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) Matumizi ya pesa katika siasa za Tanzania hayaendani na nadharia ya siasa duniani bali imekuwa ni RUSHWA isiyokifani

Ninapendekeza iundwe mamlaka ya kusimamia mapato yatokanayo na biasha ya siasa, na watu wote wanaotaka kujihusisha na mambo ya siasa na utawala wasajiliwe na kupewa namba ya mlipakodi (TIN) ili taifa linufaike na uwepo wa wakwasi hawa biashara ya siasa.

Mwaka 2010 rafiki yangu mmoja aliweka bajeti yake ya siasa kiasi cha shilingi milioni mia sita, akasema anataka akagombee ubunge, kampeni ndani ya chama chake tu aliweza kutumia zaidi ya milioni mia tatu na nusu, na ilipofika sasa kwenye kampeni za ubunge rasmi pesa iliisha, akaja kuuza nyumba haraka sana na kurudi kwenye kampeni,
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Jamaa aliangukia pua kabisa, hivi sasa anapaka rangi kwenye daladala labda sasa Mwakyembe atakuwa amemuokoa kwakupata siti za treni na kukaa.

Hiyo ndio siasa ya Tanzania inayotajwa kuwa watu kama Edward N. Lowassa, Bernard Membe, na wengine wengi wamewekeza mabilioni makubwa kwaajili ya KUWANUNUA baadhi ya Watanzania kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom