Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari: Utaratibu wa Kiserikali, Ushauri, Changamoto na Faida

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
2506742_Darasa.jpg

Habari wakuu,

Ninaamini hapa ni home of Great Thinkers kwelikweli, watu wenye mawazo mazuri sana kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea katk jamii. Kwa sababu hiyo, ninaomba mawazo yenu kuhusu mambo yote yanayo husu biashara ya shule kuanzia taratibu za kiserikali katika uandikishaji na mapato, capital requirements na jinsi ya conduct effectively, na mambo yote mengine yanayohusu hii biashara ninayopaswa kujua.

Natanguliza shukurani zangu wakubwa.

WADAU WENGINE WANAOTAKA KUELEWA KUHUSU BIASHARA HII
Wakuu nimedunduliza dunduliza mpaka nilipofikia nina kamtaji kidogo sasa nataka nifungue shule ya sekondari.

Kwa yeyote anayefahamu anipe dondoo muhimu kuhusu hii biashara, mchanganuo kiujumla kuhusu taratibu za usajili, namna ya kupata faida kupitia biashara hii nk.
Habari zenu wana-Jamiiforum,

HISTORIA FUPI
Nimekuwa na ndoto ya kuanzisha biashara ya kudumu (Ya kitaasisi) kwa muda mrefu sana, na ndoto hii ilianza tangu nikiwa kidato cha sita miaka ya 2000.

Moja ya vitu ambavyo nimewahi kujaribu na kwa sehemu flani nilifika hatua flani ambayo si ya kuita mafanikio, la hasha lakini mchakato (Process) ni kama ifuatavyo;

1. 2009-Nikiwa nimeajiriwa, niliweza kuanzisha NGO pamoja na rafiki na family friend, wakati huo yeye akiwa bado chuoni (Mwenye ndoto za kisiasa pia). Tuliweza kufanya usajili na kupata ofisi maeneo ya Mwanza, tukapata site sehemu ambayo ingetumika kama Project site kulingana na lengo na mipango ya NGO. Hii hatukuweza kwenda mbali sana baada ya rafiki yangu kufanikiwa kupata ubunge na kujikita kwenye siasa, huku mimi nikiwa bado kazini.

2. 2011-Nikiwa na huyu bwana tena, wakati huo akiwa Mbunge, tulianzisha kampuni na malengo makubw aikiwa ni kuingia kwenye biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji. Tuliweza kununua ekari 100 maeneo ya Mkuranga kwa lengo kufanya kilomo na ufugaji wa kisasa kabisa. Pia tukiwa na usajili wa kampuni, tuliweza kupata ofisi maeneo ya Mkumbusho, kulipia na kufanya designing-Hii nayo haikuwezekana ikaishia njiani.

3. 2015- Niliamua kufungua kampuni yangu binafsi na mke wangu, tulikamilisha usajiri na hatua zote, tulipata frem ya biashara, na tulianza biashara ya Huduma za fedha na baada vipozodi ambalo mpaka sasa linaendelea, ingawa huduma za fedha (M-PESA, TIGO NA HALOPESA) tumesitisha kwa muda. Malengo makubwa ni kuweza kufanya biashara na ofisi binafsi kama NGO na serikali na tunampango wa kujisajili GPSAA ili kuweza kupata fursa hizo.

4. 2015- Niliweza kununua ekari 5 za Shamba maeneo ya Bagamoyo,lengo kuu ikiwa ni kilimo na ufugaji wa kisasa, lakini ambacho kilinikwambisha ni upatikanaji wa maji. Nilipeleka wataalamu wa ku-drill kisima, maji yapo 130m, na gharama ilipaswa kuwa 10,540,000/= Nikashindwa kwa kuwa budget yangu ilikuwa ni only 5m.

5. 2017- Niliweza kununua maeneo kadhaa Dodoma, maeneo mawili tofauti kuna ekari 1 kila eneo, na eneo lingine lina ekari 2. Eneo la ekari 2 na 1 yote yapo nje ya mji kidogo umbali wa 12km toka Dodoma Mjini. Eneo la ekari moja tayari limepimwa kwa ajili ya makazi, bado tunasubiri hati kutolewa.

SHULE KWENYE ENEO LA EKARI 2
Ushauri wenu wana-Jamii.
Kwakuwa Dodoma unakuwa Makao mkuu wa nchi na kwa kukuwa, shughuli nyingi za serikali zimehamia huko, na kwakuwa projection inaonyesha kutakuwa na ongezeko la watu na mahitaji kuongezeka, ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha na shule, kwa kuamini wafanyakazi na wafanyabiashara wakazi na wahamiaji wanalo hitaji hili kwa sababu ya watoto wao.

Na kwakuwa maisha bado yanaendelea na hitaji la shule kwa kikazi ni muhimu sana. Na kwakuwa pia Eneo lipo karibu na barabara kuu ambayo TARURA wapo kwenye mpango wa kui-upgrade kwenye kiwango cha Changarawe na baadae Lami, na kwa kuwa Halimashauri tayari eneo moja yaaani upnde mmoja wa eneo lote umekamika utaraibu wa upimaji, na eneo linalofuata ni eneo ambalo ninazo hizo ekari 2. Na kwakuwa eneo la ekari 2 na hilo la ekari 1 (ambalo upimaji tayari umkamilika), ni maeneo ya makazi tayari, na huduma zote muhimu kama umeme, maji na barabara vipo, na kwakuwa mke wangu kitaaluma ni mwalimu na HR pia (Kwa kuwa amefanya mastaers ya HR-UDBS), na kwakuwa mimi pia ni Administrator mzuri na mwenye uzoefu wa kuongoza watu kwa zaidi ya miaka 13 ambayo nimekuwa kazini.

Hivyo basi nafikiri kuanzisha shule mahali hapo linaweza kuwa ni wazo sahihi sana, ingawa sina uzoefu, sina taarifa za kutosha, wala sijui gharama zipi zitakutakiwa kuweza kufanya hii project to success, hata kama return on investment siitarajii kuipata in less than 5 years, lakini nahitaji kufanya hili kwa kupata msaada wenu.

Naombeni ushauri, mawazo na njia sahihi ya kuwea kulifanya hili.

NB:
Nmeshalifanyia utafiti eneo, bado Halimashauri hawajalipangia matumizi,(Hakuna TP), hivyo niliongea na mtaaramu mmoja wa masuala ya upimaji (Kampuni binafsi), wamenishauri kuweza kulipima na kuweza kupata viwaja. Na gharama ya kufanya hivyo tayari ameshanipati.

Hii inatokana na ukweli kwamba kwa kufanya hivyo itanisaidia hata Halimashauri watakapokuja kufanya upimaji maana yake watakuta tayari eneo langu limeshapimwa na hivyo halitapata changamoto yoyote.
Habari zenu wana jukwaa.

Nina eneo lenye ukubwa heka 10 lipo Kimanzichana Mkuranga na nina ndoto za kujenga shule ya sekondari ya bweni katika eneo hilo.

Nilifanikiwa kuonana na mkaguzi wa mashule wa wilaya na mkandarasi wa wilaya kwa ushauri kidogo. Kwa sasa nimeongea na afisa ardhi ili anisaidie kuandaa mchoro wa mipango miji kwaajili ya kupata hati.. na ameniambia itachukua miezi 2 hadi hati kutoka.

Nilitamani kupata mtu ambaye amefanikisha ndoto hii ndani au nje ya jukwaa.

Natamani kufahamu:

1. Ilichukua muda gani maombi yake kujibiwa na wizara na kupewa kibali vha kuanza ujenzi.

2. Alipewa leseni akiwa amekamilisha vyumba vingapi vya madarasa na miundombinu mingineyo.

3. Changamoto mbalimbali katika soko la elimu.

Asanteni
Nawasilisha.

UTARATIBU MWEPESI WA KUFUNGUA SHULE
Wapo Watanzania ambao ndoto zao ni kumiliki shule. Ninapoongelea shule simaanishi lazima yawe yale mashule makubwa. Hata shule za awali ambazo zinaanzishwa na wajasiriamali wadogo mitaani nazo ni shule kwa maana hii katika makala haya.

Nyaraka kuu inayoongoza taratibu za usajili wa shule binafsi huitwa fomu namba RS8. Huu ndio mwongozo mkuu wa usajili. Kuna mambo ya msingi na ya kisheria ambayo mtu hutakiwa kujiandaa nayo iwapo anataka kuanzisha shule binafsi.Mambo haya huwa yanakamilishwa kwa wepesi na bila usumbufu ikiwa yanapitia kwa wanasheria lakini pia mtu anaweza kufanya mwenyewe isipokuwa hata akifanya mwenyewe kuna document za lazima ambazo lazima zisainiwe na kuthibitishwa na mwanasheria.

1. USHAURI MUHIMU KWA WALIO/WANAOTAKA KUANZISHA SHULE
Kwanza kabisa kabla ya lolote ni muhimu kujua shule yako itamilikiwa namna ipi kisheria. Utaimiliki binafsi wewe kama wewe, utaunda kampuni halafu kampuni ndo imiliki shule, au utaweka chini ya taasisi fulani. Kila kimoja katika haya kina faida zake halikadhalika hasara zake. Pamoja na hayo faida na hasara hizo zinazidiana viwango. Katika baadhi ya makala zilizopita niliwahi kuzungumza umuhimu na faida za kitaalam za kufanya biashara chini ya kampuni.Kwa ushauri wangu wa kitaalam hasa katika masuala ya makampuni nashauri kuwa ni vema sana ukianzisha mradi wa shule fungua na kampuni ili shule iwe chini ya kampuni. Zipo faida nyingi sana utazipata kupitia kufanya hivyo. Hata wenye mtaji mdogo hasa ndugu zangu wanaoanzisha nursery mitaani fungua kampuni na nursery yako iweke chini ya kampuni halafu utaona matokeo yake baada ya muda.Kufungua kampuni ni bei ndogo sana na rahisi mno hivyo si jambo la kumuogofya mtu.

2. MAOMBI YA USAJILI WA SHULE HUPELEKWA WAPI
Maombi ya usajili wa huelekezwa kwa kamishna mkuu wa Elimu. Ofisi ya kamishna mkuu wa elimu Tanzania iko Dar es Salaam. Hata hivyo nakala ya maombi hayo hupelekwa kwa mkaguzi mkuu wa elimu wa kanda husika. Kanda husika ni kanda ambayo itaanzishwa shule husika. Mkaguzi wa kanda ndiye hujushughulikia karibia mambo yote ya msingi kuhusu usajili wa shule.

3. MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA KUJIANDAA NAYO
Kila biashara huwa ina maandalizi yake kabla ya kuanza kwake. Shule binafsi nayo kama biashara nyingine yoyote inayo mambo ya msingi na ya kisheria ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia kabla ya kuanzisha biashara hii.Mambo haya pia ndiyo hayohayo utayotakiwa kuyajaza kwenye fomu maalum ya kuombea usajili wa shule yako.

(a) Jina la shule. Lazima kwanza ujue shule yako itaitwaje.Huwezi kufanya mipango ya shule bila jina. Pia jina hutakiwa kujazwa kwenye fomu maalum ya kuombea usajili.

(b) Lazima ujue unataka kuanzisha shule ya aina gani. Shule ziko aina nyingi, unataka shule ya awali(nursery),shule ya msingi,sekondari ya form iv au v & vi. Pia ujue iwapo shule hiyo itakuwa kutwa au ya kulala, ya wasichana na wavulana au wavulana tu au wasichana tu. Kama shule yako ni sekondari lazima ujue itakuwa inashughulika na michepuo ipi sanaa, biashara,kilimo, sayansi, elimu ya ufundi au kitu gani.Haya lazima ujiandae nayo na uyajue.Pia taarifa hizi huwa zinahitajika unapokuwa unajaza fomu ya usajili hivyo ni muhmu kuziandaa.

(c) Jambo jingine ni tarehe au kipindi ambacho shule inatarajiwa kufunguliwa. Taarifa hii hutakiwa kwasababu mamlaka za usajili zinajenga dhana(assume) kuwa mtu anapoamua kujaza fomu ya usajili basi huwa yuko tayari kuanzisha shule na hivyo lazima awe na tarehe ambayo shule yake itaanza.Hivyo lazima uandae tarehe kama una mpango huu.

(d) Pia huwezi kuanzisha shule bila kuwa na Meneja wa Shule. Sheria inataka kabla ya usajili lazima awepo meneja na atajwe katika fomu ya usajili.

( e ) Anuani kamili ya mahali ambapo shule inakusudiwa kufunguliwa ni jambo jingine linalopaswa kufafanuliwa kupitia fomu hii. Anuani hapa si tu P.O BOX..., hapana. Unataja mtaa, kitongoji, kata, wilaya, na mkoa. Hii ndio anuani.

(f) Pia uandae hati ya Umiliki wa Ardhi au Mkataba wa Pango wa eneo ambalo shule itafunguliwa.

(g) Utatakiwa kuonyesha sifa na idadi ya walimu watakaoajiriwa, uwiano wa walimu na wanafunzi kwa maana ya wastani wa mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi wangapi (Teacher-Students ratio)

(h) Utatakiwa kueleza vifaa vitakavyokuwa shuleni na pia kuonyesha kiwango cha juu zaidi (maximum) cha wanafunzi wanaoweza kusoma kwa wakati mmoja katika shule itakayofunguliwa.

(I) Kutaja kiwango cha ada unachokusudia kuwatoza wanafunzi wa shule hiyo, huku ukipambanua pia tozo nyinginezo kama vile gharama za bweni na aina ya vifaa ambavyo wanafunzi wenyewe wanapaswa kuja navyo shuleni.

4. VIAMBATANISHO MUHIMU
Vimbatanisho muhimu vya kuandaa ni Hati za Idhini za matumizi ya Ardhi chini ya taratibu za mipango miji kutoka mamlaka husika hasa manispaa, Mhandisi wa Wilaya au Mji, serikali za vijiji, na kadhalika.

Cheti kutoka kwa bwana afya kuthibitisha kwamba eneo litakalotumika kwa ya ajili ya shule linakidhi vigezo vya afya na usalama wa wanafunzi, pia ambatanisha taarifa za wafanyakazi wasio walimu, na nakala ya ramani ya majengo.

Chanzo: Bashir Yakub/HabariLeo

MAONI NA USHAURI WA WADAU
MWENYE NDOTO HII, ANZIA HAPA

Kwa wenye ndoto za kuwa na shule. Please anzia hapa. Sio lazima uanze kujenga shule na kujitanagaza unajenga shule. Jenga vyumba viwili vya ukubwa wa madarasa andikisha watoto wa nursery school waanze kusoma.Then fuatilia usajili wa nursery school ambao hauchukui mda mrefu. Then kupitia hao watoto wa nursery utapata uzoef wa kuendesha shule for one to two years.

Ndani ya hiyo miaka weka tuition ya jioni ya wanafunzi wa msingi na secondari kuendeleza kipato na kukuza kituo.Maana kwa mda huo itakuwq nursery na tuition center. Ukishajipanga ndo uanze kufuatilia taratibu za usajili ujitahidi kiwafuata right people kuwauliza taratibu za usajili. Hasa hawa wanaomiliki shule watakusaidia. Ukipata majibu ya kukatisha tamaa kwa mmoja jaribu kwingine.Hii ni kwa eng medium pri and primary school.

Mimi nasimamia shule amabayo boss wangu alianza hivyo na sasa hivi ndo tupo kwenye hatua za mwesho za uasajili ila tuna hadi darasa la pili wanasomea kule nursery. Cha msingi ni elimu bora ambayo itamfanya mzazi akutangazie shule.

Kwa secondary sina uzoef sana japo tuna mpango wa kujenga. Kama kipato chako ni cha chini anziaha tuition Centre ambayo haihitaji hata kuwa na kabali cha kuendesha. Naomba niishie hapa kwa hiki kidogo mnaotaka kuanzisha shule mtajifuza kitu.
USHAURI KWA MWENYE NIA YA KUMILIKI SHULE

Mimi sio mahiri saana kwenye kujadili humu ila leo imenibidi nichangie mawili matatu.

Binafsi nafanya kazi kwenye taasisi ya kielimu ambayo kazi yake kubwa ni kuendesha mashule na kuanzisha mashule. Na npo dodoma miaka miwili sasa nikiwa kama mratibu wa kanda ya kati wa taasisi hiyo.

Kwa Dodoma hapa tuna project ya ujenzi wa shule wa eneo flani hapa hapa dodoma mjini.

USHAURI WANGU JUU YA WAZO LAKO

1. Kwa eneo lako hilo ni dogo kulingana na vaigezo vya serikali ni vema utafute eneo kubwa zaidi kuanzia hekari 3 mpaka 7. (Tatu kwa mjini na 7 kwa nje ya mji)

2. Kwa uzoefu ulioelezea hapo naona ni bora ungeanza kukodisha shule kwa kuingia mkataba wa kisheria wa uendeshaji wa shule, ili kidgo kidgo uweze kukusanya mtaji kwa ajili ya ujenzi wako binafsi (binafsi taasisi yangu inaendesha shule zaidi ya 30 ila inamiliki shule 1 tu. Ila ina waajiriwa zaidi ya 200)

3. Watu wengi kwa sasa wanashindwa kuendesha kwa changamoto kadhaa wa kadhaa kwa hiyo huo uzoefu ulio nao nahic bado hutoshi. Coz kwa mfano taasisi imeweka waratibu kila mkoa kwa ajili ya kutangaza shule kukusanya wanafunzi.

4. Kuna mbinu nyingi za kupata wanafunzi, kuimarisha matokeo, kupunguza matumizi katika shule ambapo ni tofauti kabisa sehemu au kampuni nyingne.

5. Yaani HR wa kampuni nyingne kuna uwezekano mkubwa akafeli endapo akiingia shuleni. Na hata mwalimu wa kawaida, kwenye kuendesha shule binafsi kwenye zama hzi anaweza akaferi kama hana skills na machachari ya kusavaivu kwenye tasnia.


HATUA TANO (5) ZA KUANZISHA NA KUSAJILI SHULE YA MSINGI AU SEKONDARI
Ili kuanzisha na kusajili Shule yenye ubora unaostahili wadau hawana budi kufuata hatua mbalimbali kama zilivyoainishwa kwa kina katika “Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982”. Kwa kifupi hatua hizo ni kama.

1. Hatua ya kwanza: Kibali cha Kujenga Shule
Mwenye nia na uwezo wa kuanzisha Shule atume maombi ya kutaka kujenga shule kwa maandishi kwa Afisa Elimu

Kiongozi. Maombi haya yapitishwe kwa Afisa Elimu wa Wilaya Shule itakapojengwa na Afisa Elimu Mkoa yakiwa na viambatisho vifuatavyo:
  • Rejea mwongozo wa andiko la mradi la Wizara,
  • Bank Statement yenye zaidi y ash. Milioni 62,000,000/=
  • Nakala ya hati/offer/uthibitisho wa kumiliki ardhi iliyotolewa kwa matumizi ya shule inayotambu8lika kisheria na serikali kuu ya mtaa au kijiji ( eneo lisipungue ekari 71/2 kijijini na 31/2 mjini)
  • Michoro ya majengo ya shule inayoonyesha vipimo kwa kuzingatia viwango vya Wizara na Elimu ya mafunzo ya ufundi,
  • Ramani ya shule inayoonyesha mpangilio wa majengo na viwanja vya michezo,
  • Cheti cha usajili wa kampuni, shirika , umoja , NGO iwapo shule ni ya jumuia na katiba yake au mkataba wa maridhiano.
  • Endapo mdau anataka ikutumia jina la Mtakatifu ( Saint ) awasilishe kibali toka kwa askofu wa dini inayotambulika kinachoidhinisha matumizi ya jina hilo.
  • Kamishina wa Elimu akiridhika na maombi hayo atatoa kibali cha kujenga Shule kimaandishi, ndipo ujenzi utaanza.
2. Hatua ya pili: Kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na Meneja wa Shule
Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na inahusisha yafuatayo:
  • Mwombaji ajaze fomu Na. RS. 6 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na RS. 7 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Meneja wa Shule.
  • Hatua hii itafanywa baada ya mwombaji kuwa amekamilisha ujenzi wa majengo yote muhimu kwa asilimia 75%
  • Majengo hayo ni vyumba vya madarasa, Jengo la utawala/Ofisi za walimu, Maktaba, vyoo vya wasichana, wavulana na wafanyakazi bwalo/ukumbi, maabara.
  • Majengo hayo lazima yawe yamekaguliwa na mamlaka za Wilaya, ambazo ni ; Mhandisi wa Majengo , Afisa Afya na Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Wilaya na kwamba fomu hizo ziwe zimepitishwa na Afisa Elimu wa Wilaya, Afisa Elimu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa.
  • Wizara ikiridhika itatoa kibali cha maandishi cha kumthibitisha Mwenye Shule na Meneja wa Shule.
3. Hatua ya Tatu: Maombi ya Kusajili Shule
Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na ya pili na inahusisha yafuatayo:
  • Mwenye Shule hujaza fomu Na. RS 8 ya maombi ya kusajili shule baada ya kuwa amekamilisha mahitaji yote yanayotakiwa kwa Shule ya aina anayoiomba: ambayo ni Majengo na Samani, Vitabu, Mihutasari ya masomo, Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia na Kuajiri walimu na wafanyakazi wengine wenye sifa na uzoefu.
  • Mwenye Shule ambaye Shule yake imetimiza vigezo vyote na shule kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda hupewa taarifa ya kusajiliwa kwa Shule yake kimaandishi. Aidha, atapatiwa cheti cha usajili chenye namba ya usajili .
Usajili wa Shule za Kimataifa
Wizara husajili shule zenye hadhi ya kimataifa, usajili huo unafanywa na Taasisi za kimataifa zinazosajili Shule za aina hiyo. Wizara huthibitisha na kutambua shule zinazosajiliwa na taasisi hizo kama za kimataifa. Taasisi hizo ni “European Council for International Schools” (E.C.I.S) na “Association of International Schools in Africa (AISA). Taasisi hizo zimeweka vigezo vya kusajili Shule za kimataifa. Shule itapewa usajili pale tu itakapotimiza vigezo vyote vilivyowekwa.

Hatua za kufuata ili Shule iwe ya Kimataifa

Mwenye Shule yeyote anayetaka Shule yake iwe na hadhi ya kimataifa anapaswa kufuata hatua zifuatazo:
  • Shule isajiliwe na Wizara kama shule ya kawaida.
  • Mwenye Shule aiombe Wizara kimaandishi kutaka Shule yake iwe ya kimataifa.
  • Endapo Wizara itaridhika na ombi hilo itatoa kibali cha maandishi na Mwenye Shule ataendelea na hatua za kutuma maombi kwenye taasisi zinazosajili shule hizo.
  • Shule itakaposajiliwa kama ya kimataifa, Mwenye Shule aijulishe Wizara kimaandishi na kuambatisha nakala ya usajili huo.
Usajili wa shule/Taasisi za kidini
Taasisi za kidini zinazotaka kuanzisha na kuendesha Shule/Taasisi za kidini zinapaswa kufuata hatua zote tatu kama zilivyoelezwa isipokuwa wanapaswa kujaza fomu Na. RS.9 katika hatua ya usajili.

Tanbihi
Uvunjaji wa Sheria kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kifungu cha 59.

Ni nani anayehusika katika mchakato wa usajili wa shule?

Katika ngazi ya Wilaya:
Wakaguzi wa Shule; Maafisa Elimu; Wahandisi wa Majengo na Maafisa Afya wana wajibu mkubwa wa kuthibitisha kuwa maandalizi ya kutosha kuhusu majengo na mazingira ya Shule kiafya yanafaa kwa matumizi ya shule. Taarifa zinazoandaliwa na watendaji hao husaidia kutoa picha halisi ya matayarisho na kutoa mapendekezo sahihi pale wanapopitisha fomu za maombi ya kumiliki na kuendesha shule. Maombi haya huisaidia Wizara kupata picha halisi kuhusu matayarisho ya mwombaji na kufanya uamuzi sahihi.

Watendaji wa Serikali ya Kijiji/Mtaa na Kata
Hutoa taarifa mahsusi zinazosaidia kutoa picha ya mahitaji ya Elimu katika eneo lao na kumthibitisha anayetaka kuanzisha Shule kama ndiye mmiliki halali wa eneo la Shule itakapojengwa.

Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda
Hufanya ukaguzi maalumu kwa lengo la kusajili shule na hukamilisha fomu Na RS. 8 kisha kutuma fomu hizo kwa Kamishina wa Elimu pamoja na taarifa ya Ukaguzi wa Shule husika. Mkaguzi Mkuu wa Shule husimamia na kutathimini utekelezaji wa mitaala pamoja na uendeshaji wa shule kwa ujumla.

Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
Husimamia masuala yote ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao. Wanajukumu la kutoa maamuzi juu ya aina ya mipango inayotakiwa kufanywa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za serikali za msingi na za sekondari. Wanasimamia uhamasishaji wa maendeleo ya sekta ya elimu ya jamii inayowazunguka pia wanapokea na kupendekeza maombi ya kutaka kumiliki, kuendesha na kusajili Shule.

Waziri wa Elimu
Waziri wa Elimu humthibitisha Mwenye Shule na huidhinisha usajili wa Shule za dini.

4. Usajili wa Walimu
Usajili wa walimu unafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 sehemu ya VI na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 pamoja na Kanuni ya Elimu ya mwaka 2002.

Makundi matatu ya walimu yanayoweza kusajiliwa
  • Mwalimu aliyefuzu na kufaulu mitihani kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Mtu asiye na taaluma ya Ualimu atakayeomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.
  • Walimu wasio raia wa Tanzania waliofuzu taaluma ya Ualimu wanaoomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.
Walimu wenye sifa
  • Mwalimu mwenye sifa husaini mkataba na mwajiri wake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi za Walimu za mwaka 2003
  • Mwalimu huyu husajiliwa kutoka rejesta Na. II kama mwalimu anayesubiri kuthibitishwa.
  • Baada ya kumaliza muda wa kusuburi kuthibitishwa kwa mwaka mmoja, mwalimu huthibitishwa kwenye rejesta Na. I ya walimu waliothibitishwa kazini.
Walimu walio na taaluma ya ualimu ambao sio watanzania wanaotaka kufundisha nchini
  • Mwombaji ataomba kupatiwa leseni ya kufundisha kupitia kwa uongozi wa shule anayotaka kufundisha na kuyapitisha maombi hayo kwa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda. Mwombaji anaambatisha vyeti vya taaluma na umri wake.
  • Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda. hupitia na kutoa mapendekezo ya maombi hayo kwa Kamishina wa Elimu
  • Maombi ya ajira ya Walimu huchambuliwa na kamati maalum ambayo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala kisha humshauri Waziri kupitisha maombi haya.
  • Waziri akiridhika hutoa kibali cha kufundisha nchini.
  • Kamishina wa Elimu hutoa idhini ya mwombaji kupatiwa leseni.
  • Walimu wenye leseni wanasajiliwa kwenye rejesta Na. III
5. Mwongozo wa Usajili wa Shule 1982
Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982 unapatikana katika Ofisi za Elimu za Wilaya, Mkoa na Makao Makuu ya Wizara. Mwongozo huu unatoa tafsiri ya Sheria ya Elimu na Kanuni za Elimu kuhusu usajili wa shule na walimu.

Mambo muhimu yaliyopo katika mwongozo ni pamoja na fomu za usajili wa shule na walimu. Aina ya fomu (majina mapya katika mabano) hizo ni:
  • Fomu Na.6 (RS 6) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Mwenye Shule na fomu Na. 7 (RS 7) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Meneja wa Shule.
  • Fomu Na. 8 (RS 8) kuhusu maombi ya usajili wa shule zisizo za Serikali na Fomu Na. 9 (RS 9) kuhusu maombi ya leseni na usajili wa Shule/Taasisi za Dini.
  • Fomu Na. 4 (RT 4) kuhusu maombi ya kutaka kupatiwa leseni za kufundisha.
  • Fomu Na, 3 (RS 3) kuhusu taarifa ya kusajiliwa walimu wenye leseni katika rejesta Na. 3
  • Fomu Na. 1 (RT 1) kuhusu cheti na taarifa ya kusajiliwa walimu ambao wamemaliza muda wa mwaka mmoja na kusubiri kuthibitishwa kazini.
Chanzo: Lemburis Kivuyo
 
Find a good location first, then njoo hapa tukupe datas, ila angalizo, tegemea kubreak even after 5yrs, thn profits after 7 years.
 
Tafuta wataalamu wa biashara ambao wana uzoefu wa kuandaa michanganuo wenye uzoefu na sector hiyo new mzalendo anaweza kuwa mmoja wao.
 
Nashukuru sana wakuu kwa mawazo yenu mazuri, nitayafanyia kazi.

NINAOMBA MAWAZO ZAIDI KUTOKA KWA WADAU WENGINE ILI NIWE TAJIRI WA MAWAZO KATIKA HILI, NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU WAKUU.
 
Je unataka shule ya aina gani, boarding au day school, kama ni boarding, girls tu au boys tu au mseto.ukishajua utajua ni eneo gani litakufaa, unatakiwa ujue vitu muhimu vitakavyokurahisishia kusajiliwa kwa shule yako n.k. gud lak.
 
Here we go again. Shule nazo zinakuwa ni biashara. Suala la kutoa service na ku-uplift jamii halijadiliwi
 
Here we go again. Shule nazo zinakuwa ni biashara. Suala la kutoa service na ku-uplift jamii halijadiliwi

Afadhali umeuliza,

Shule zilishakuwa biashara tangu siku nyingi sana na serikali yetu kama kawaida imesinzia na kukoroma.Kufanya mitihani ya kuqualify ada, matokeo yalitoka kama hujafikia maksi fulani huchukuliwi (pamoja na kuwa shule ni sehemu ya kujifunza) sasa hivi shule tunazoziita nzuri sio nzuri ila tu ni sababu zinachukua wanafunzi wenye msingi mzuri.

Ada za baadhi ya nursery schools na primary schools sasa hivi ni kubwa kuliko tuition fee ya chuo kikuu. (Justification ya hili hakuna) nakadhalika unaweza andika mpaka mkono uchoke.

Shule kupokea ada kabla shule haijasajiliwa na mwishowe wanafunzi kushindwa kufanya mitihani .

Matatizo no mengi sana.
 
Nashukuru kwa ushirikiano wako mzuri, shule ninayotaka ni boarding ili kuwaepushia wanafunzi adha za USAFIRI na kupoteza muda mwingi ambao wangeweza kuutumia kwa kujisomea na kufanya vizuri zaidi, pia nina mpango wa kuwa na shule ya jinsia moja ama GIRLS tu au BOYS tu, lakini kwa kuanza BOYS tu. Sina mpango wa shule ya mchanganyiko kabisa.

Bila shaka kwa kukujibu hivi unaweza ukanipa mawazo ya maeneo gani yanafaa zaidi, na naomba sasa kwa wakuu wote wenye kujua taratibu za kusajili shule wanisaidie maelekezo au mawazo kuhusu hili...namalizia kwa kusema. THE MORE YOU GIVE THE MORE YOU GET EVEN MORE. Asante sana
 
Asante sana mkuu,,,kwa kudokeza kipengele cha social welfare, biashara zipo za aina mbili kwa mgawanyo huu, kuna biashara ya service na biashara ya bidhaa nyingine. Na katika biashara lengo lake ni kupata faida, asikudanganye mtu, lengo kuu ni hilo,,isipokuwa lengo hilo ili litimie lazima ufanye kitu, kama vile ilivyo mtaka cha uvunguni sharti ainame, katika elimu ya masoko(MARKETTING) ya kisasa tofauti na ya kale ni kwamba mfanyabiashara mwenye mafanikio ni yule anayeangalia kile mteja anachotaka kwa upana sana nikimaanisha UHITAJI WAKE (WILLINGNESS) na UWEZO WAKE (CAPACITY) kwa kufanya hivi ile huduma au bidhaa atakayo mpelekea mteja huyu itakuwa inaendana na uwezo wake na uhitaji wake. Kwa hivyo atafanikiwa.

Uhitaji wa jamii ambao ndio wateja wa huduma hii ni mafanikio ya watoto wao kielimu na uhakika wa huduma wanayopewa ikiimaanisha iwe na risk ama ndogo sana ama hamna kabisa ya watoto wao kupiga ngumi hewani kwa kusoma muda mrefu kumbe shule haijasajiliwa.

Ni kweli lililogusiwa kwamba wapo wengi sana wanaoanzisha shule sasa hivi wanaotoa huduma mbovu kinyume na mategemeo na uhitaji wa wanajamii, lakini hii haimaanisha elimu kuwa biashara ni kitu kibaya, isipokuwa elimu kuwa biashara mbaya ni kitu kibaya maana tukisema kwa ujumla kamba BIASHARA ni kitu kibaya tutakuwa tunakosea,,maana tutajiuliza wangapi wanaaishi hapa tu tanzania kwa kutegemea BIASHARA. Hatujaenda dudiani kote, biashara nadhani kwa mtazamo wangu ndio shughuri yenye mchango mkubwa zaidi na tija zaidi kwa maendeleo ya nchi yeyote duniani.

Ninaunga mkono kwamba elimu ni huduma kama ilivyo huduma nyingine zikiwemo za kibenki, na kama hizi huduma nyingine zilivyo BIASHARA hasa zikifanywa na watu binafsi basi nayo elimu haizuiwi kuitwa BIASHARA, lakini kuna BIASHARA MBAYA na BIASHARA NZURI. Inakuwa mbaya pale inaposhindwa kukidhi matakwa ya wanajamii, na inakuwa nzuri pale inapokidhi matakwa ya wanajamii kwa mapana zaidi hata kuliko watoa huduma wengine.

Namalizia kwa kusema ELIMU KWA WATU BINAFSI NI BIASHARA lakini ili biashara hii ifanikiwe lazima matakwa ya wanajamii yawekwe mbele maana hao ndio MABOSI katika BIASHARA, ukiwaletea ujinga kama wanavyofanya hao mkubwa aliosema utawanyonya kwa muda mfupi lakini baadaye wote watakukimbia.

Natanguliza shukurani zangu kwa wakuu walioguswa kuliongelea hili.

ASANTENI
 

Habari zenu wana jukwaa.

Nina eneo lenye ukubwa heka 10 lipo Kimanzichana Mkuranga na nina ndoto za kujenga shule ya sekondari ya bweni katika eneo hilo.

Nilifanikiwa kuonana na mkaguzi wa mashule wa wilaya na mkandarasi wa wilaya kwa ushauri kidogo. Kwa sasa nimeongea na afisa ardhi ili anisaidie kuandaa mchoro wa mipango miji kwaajili ya kupata hati.. na ameniambia itachukua miezi 2 hadi hati kutoka.

Nilitamani kupata mtu ambaye amefanikisha ndoto hii ndani au nje ya jukwaa.

Natamani kufahamu:

1. Ilichukua muda gani maombi yake kujibiwa na wizara na kupewa kibali vha kuanza ujenzi.

2. Alipewa leseni akiwa amekamilisha vyumba vingapi vya madarasa na miundombinu mingineyo.

3. Changamoto mbalimbali katika soko la elimu.

Asanteni
Nawasilisha.
 
Mkuu shule za sekondari kwa sasa nchini ni nyingi sana, na itakuchukua miaka minne kutengeneza jina, kwa ushauri wangu jenga kiwe chuo cha uwalimu ngazi ya cheti au diploma, vyuo vya uwalimu ni vichache sana Tz watu wengi wanakosa nafasi sabab ya uchache.
 
Asante Mkuu kwa ushauri nitaufanyia kazi.
Muda mwema.

Mkuu shule za sekondari kwa sasa nchini ni nyingi sana, na itakuchukua miaka minne kutengeneza jina, kwa ushauri wangu jenga kiwe chuo cha uwalimu ngazi ya cheti au diploma, vyuo vya uwalimu ni vichache sana Tz watu wengi wanakosa nafasi sabab ya uchache
 
@Ipilimo bado napokea maoni kuhusu kuanzisha chuo badala ya shule ya sekondari.

Nahitaji kufahamu tofauti na kungoja kwa miaka minne ili shule ijulikane je kuna changamoto nyingine yeyote ambayo inakifanya chuo cha ualimu kuwa biashara bora dhidi ya shule ya sekondari?

#Dzudzuku hii idea nzuri ila nimekwama kutokana na comments za wadau maana nilishaimba afisa ardhi anipimie eneo na liwe kwaajili ya sekondari hivyo naangalia kama nikiona maelezo ya wadau yapo poa itabidi nimuombe abadili matumizi na asiyafanye kwaajili ya sekondari.

Asante.
 
Mkuu chuo cha uwalimu wala hautatumia nguvu nyingi kukitangaza, raia wata kuja wenyewe, kuna uhaba mkubwa sana wa vyuo vya uwalimu katika nchi hii, wanaoomba kujiunga vya serikali huchukuliwa wachache sana na wengi hukosa.
 
Me nakushauri uangalie upungufu wa walimu serikalini na idadi ya walimu vyuoni kisha ufanye maamuzi kwani kwa sasa ualimu wa Certificate unatoweka labda wa Diploma kwa college alafu upungufu wa walimu ni Elfu 20+ kwa sasa kwa ujumla idara zote.

Tofauti na shule ya secondary kwani ni lazima na sio kusomea ajira kama ualimu ambao unaendeshwa na uhitaji wa soko

So nakushauri ufanye research na feasibility study for both projects kwa kuangalia demand competitors challenges per the project Area.
 
Mkuu ualimu ni kwa sasa baada ya miaka 2 hawahitaji kwa wingi, na sasa ata vyuo vikuu wameanzisha dipu, ushindani mkubwa.
 
Mkuu fungua chuo cha masomo ya biashara utapata vichwa vya kufa mtu tena kozi ziwe. BUSINESS ADMINISTRATION, INFO. TECHNOLOGY, TOURISM, EARLY CHILDHOOD, CUSTOMER SERVICES, SECRETARIAL STUDIES, COUNSELLING etc. tena kwa Dar utawapata pia wakufunzi kwa bei nafuu sana. tena wengi kama part-time unawalipa kidogo tu
 
#Ipilimo bado napokea maoni kuhusu kuanzisha chuo badala ya shule ya sekondari.

Nahitaji kufahamu tofauti na kungoja kwa miaka minne ili shule ijulikane je kuna changamoto nyingine yeyote ambayo inakifanya chuo cha ualimu kuwa biashara bora dhidi ya shule ya sekondari???

#Dzudzuku hii idea nzuri ila nimekwama kutokana na comments za wadau maana nilishaimba afisa ardhi anipimie eneo na liwe kwaajili ya sekondari hivyo naangalia kama nikiona maelezo ya wadau yapo poa itabidi nimuombe abadili matumizi na asiyafanye kwaajili ya sekondari.

Asante.




QUOTE=IPILIMO;9600063]Chuo cha Ualimu kwa sasa ni zaidi ya shule ya sekondari kibiashara. SISI www.kimiconsultancy.blogspot tupe kazi ya kukuandikia proposal na mchanganuo wa kuanzisha chuo au shule.
Thanks
[/QUOTE]

Ndugu, hakuna biashara mpya hapa duniani, kila biashara inawatu tayari, suala kubwa ni umejipanga vipi.
 
Kufungua chuo ni vema, ila usilenge walimu.

Pia upatikanaji wa wakufunzi wa hivyo vyuo utawapataje?
 
Back
Top Bottom