Biashara ya kuweka nyimbo kwenye simu + haki za wanamuziki + sheria

Penguin-1

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
406
64
Habari Wadau,
Kuna jamaa yangu yupo mbali sana anataka kuanzisha biashara hizi za kuweka nyimbo kwenye simu(i believe kwa cable/bluetooth) ,amepata computer na ana miziki mingi ya nje na mingi mikali ya bongo fleva inayo hit kwa sasa.

Swali lake la msingi ,anauliza haswa kwa miziki ya bongo fleva ,je atakuwa anavunja sheria ya haki miliki?

na je nini anaweza kufanya ili asije vunja sheria?(kama itakuwa inaonekana anavunja)

Binafsi najua hizi biashara zinafanyika sana ,lakini sijui kuhusu uhalali wake.Ndio maana nimeshindwa kumpa jibu la moja kwa moja.

mwenye hizi taarifa anijuze ,niwasilishe kwa jamaa.(na kwa faida ya wasiojua)
 
hamna sheria ya hakimiliki bongo,cosota wamelala.........,piga pesa ndugu wakija kushtuka ni ........baadae sana
 
Ni kosa kisheria kunakili kazi yoyote ya kisanii kwa namna yoyte ile bila kupata kibali kutoka kwa kampuni au msanii husika.
 
Mimi si mfuatiliaji mzuri wa blahblah za bungeni lakini kama nimesikia bunge hili ltapitisha hayo masuala ya hakimiliki. Na sheri itaanza kutumika january next year. Wanafatilia watujuze. Kwa nionnavyo huyo jamaa na aanzishe tu na hapo sheria itakapofanya kazi yake ataangalia channel za kupitia kuhalalisha. Kwa sasa watu kibao wanakula hela kwa wizi huo ambao bado unaonekana ni kama halali
 
Piga mzigo kijana wakija waanze na wewe, kutokujua sheria sio kunusurika kufungwa. wewe andaa kama ka 1m ka kuonga c unajua bongo yetu. au piga za nje tu maana za vijana hawa wanaweza kuleta ngebe ukakosa ukwanja
 
Mimi si mfuatiliaji mzuri wa blahblah za bungeni lakini kama nimesikia bunge hili ltapitisha hayo masuala ya hakimiliki. Na sheri itaanza kutumika january next year. Wanafatilia watujuze. Kwa nionnavyo huyo jamaa na aanzishe tu na hapo sheria itakapofanya kazi yake ataangalia channel za kupitia kuhalalisha. Kwa sasa watu kibao wanakula hela kwa wizi huo ambao bado unaonekana ni kama halali
hili ndo jibu
 
Mawazo mazuri..Binafsi nitamshauri jamaa aweke za nje tu...
Za ndani kwa kweli sio fair hata kidogo....
niwashuru woooote!.
ova!.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom