Biashara ya kusafirisha Abiria-Bus Kubwa Kwenda Mikoani-Msaada wa Mawazo

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
16,496
17,372
Wana JF Heshima Mbele.Mimi mdau mwenzenu nafikiria sana kujikita kwenye biashara ya kusafirisha abiria kutumia ma bus makubwa NIssan Diesel au hata Scania.sababu mjasiliamali mdogo sana naomba muongozo na mawazo yenu kwangu jinsi nitafanya kuweza kupata aina hizo za bus hata kama used na aina gani nzuri kwa wajasiliamali wadogo kama sisi!naomba mawazo yenu wana JF.asante
 
aaah mkuu usifanye hiyo biashara bana'majini na uchawi ndio nguzo yao kuu'kuna biashara kibao mwaya'jitahidi sana kujiepusha na biashara za strees
 
aaah mkuu usifanye hiyo biashara bana'majini na uchawi ndio nguzo yao kuu'kuna biashara kibao mwaya'jitahidi sana kujiepusha na biashara za strees

Kwa ushauri huu hatutaendelea hata siku moja! Mtu akitaka kitu mnashirikisha uchawi...

Mi si mzoefu sana ktk hili, ila usikatishwe tamaa na watu fanya mambo yako kwa amani kabisa na Ujasiri na kujiamini. Huu ndio ujasiriamali wenyewe..
 
Biashara hii ni nzuri ila mara nyingi hufa kutokana na wafanyakazi.
sijui, labda uajiri wa Zimbabwe lakini wabongo watawakera wateja na kukuibia.
jifunze kwa scandinavia na hivi sasa Dar Exp inavyo pata shida.
 
ni biashara nzuri sana zaidi ukiweza kusimamia vzuri tangu awali ujue mapato na matumizi yake kwa miezi kadhaa kuhusu aina ya gari ningekushauri YUTONG ni nzuri sana na kwavile zina garantiini alafu ni mpya bei ni nafuu sana ukilinganisha na scania alafu ulaji mafuta ni nzuri sana kulinganisha scania na nissan d kiujumla ni biashara nzuri ukiwa na malengo na usikae na gari mpaka izeeke miaka 2-3 unauza
 
Mkuu, kuna jamaa yangu anazo hzo kama kumi hv, recently zimekuwa zikimtia kichaa; kila mara inabidi aweke standby gari ya ziada maana imekuwa kawaida kufa safarini, na linapokufa mpaka afike mchina kulitengeneza!
 
Yutong ni kero. Anyway ni Mchina. sasa subiri ligome kuwaka abiria wakiwa ndani halafu milango nayo ikatae kufunguka. utalia!
 
Back
Top Bottom