Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,444
Inauma tena inasikitisha sana kuona kila siku gesi inapanda bei kila leo unaambiwa bei mpya hivi gesi nayo tunaagiza Russia?? au huko Russia kwenye soko la dunia imependa jamani? Tuoneane huruma mmetushawishi tuachane na majiko ya mkaa wengine tulisha yatupa lengo kuu nikuokoa mazingira yetu kuepukana na tabia nchi lakini leo hii gesi tunapandishiwa kiholela hawa wanao jiita EWURA wapo kwa masrahi ya nani? gesi tuchimbe wenyewe alafu tununue kwa bei ya juu hii inaingia akilini kweli au nayo inaagizwa nje? najua mtajitetea kama mnavyo tufanyizia kwenye mafuta hapa kwa Gadaffi 1lt ya petrol ni sh 250 kwa pesa ya TZ ukiisafirisha mpaka ifike bongo hapa haiwezi fika kwa bei ya sh.1750 kwa lita.
Jamani wala nchi tuoneane huruma wajameni madarakani mmekaa kwa jasho letu alafu mnatugeuka tena dah inauma kwakweli. Au mnataka tuanze kutumia mavi ya ng'ombe kama nishati? maana hiyo ndo cheap kabisa unaagiza magunia yako kadhaa kijijini unaweka stock mpaka unasahau.
Inauma sana