Biashara ya kuni/mkaa kurudi kwa nguvu: Gesi imepanda maradufu ndani ya wiki moja!

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kusikitisha serikali inahamasisha upandaji miti na usafi wa mazingira, sasa hivi gesi imepanda kiasi cha kutisha, hivyo kuonekana kama mitungi ni maapambo ndani ya nyumba zetu.

Mkazo wa serikali ni kuhimiza kutumia ges ambayo watanzania wengi walikuwa waniogopa sana kuwa inalipuka hivyo wakendelea na ujinga huo takribani ya mika zaid ya mitano, sasa baada ya mafunzo makali pamoja uvumbuzi wa njia rahis ya kuepuka hatari na kuanza kutumia ges sasa imepanda sana kiasi cha kukumbuka jiko la nchina ambalo tulishalipa kisogo siku nyingi.

Haya hawa watu wa EWURA wako wapi au wameula wakanyamaza, huenda wanapewa posho na walanguzi wa gesi maana sijawahi kuona wanakemea, wakati huo huo kumbuka gesi inachimbwa Tanzania, la kushangaza zaidi uchafu wa mazagazaga mengi yanapotea bure kwa nini halmashauri ya Jiji isiagize vifaa vya kutengeneza mkaa wa uchafu wa Jiji kama mradi hili magari yao yasiendelee kukosa petroli ya kukusanya uchafu.

Hii sehemu ya nishati inahususiana nini na mazingira labda wizara hizi zinachanganywa,
 
Mimi sijui tunafaidi nini kama watanzania kuwa SONGAS GAS ni aibu sana gas kuwa bei juu wakati Mungu alituwekea bure itusaidie
 
Tatizo watanzania uwa hatuna wa kututetea,kikitokea chama cha siasa kutoa kauli kwa hili utasikia wanaleta uchochezi,ingekuwa gesi inatoka nje tungeambiwa exchange rate,ajabu hata dola inaposhuka thamani bei zinabaki palepale,tusipokaa sawa bei ya gesi itakuwa juu zaidi ya umeme,EWURA wamelala tu,inavyoonekana nao ni wajasiliamali kwenye hizo biashara hivyo si rahisi kujimaliza.

Bei ya bidhaa zote imepanda,ukiingia madukani utafikiri mwenye duka kakuibia,kwa sasa kuomba stakabadhi ni jambo la kawaida ili ukapige hesabu zako mbele kwa mbele ili kudhibitisha kuwa hujaibiwa,kwa hili nadhani hata TRA watapata mapato kama wenye maduka hawana vitabu viwili viwili kwa lengo la kukwepa kodi,TUTATESEKA MPAKA LINI?
 
Bei ya gesi yazidi kupaa

Tuesday, 28 December 2010
Editha Majura

WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari namna watakavyokabiliana na ongezeko la gharama ya maisha kufuatia ongeza la bei ya umeme kwa asilimia 18.5, imebainika bei ya gesi ya kupikia imeongezeka kati ya Sh 4000 mpaka Sh9000 ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Utafiti uliyofanywa na gazeti hili kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa tangu mwezi Oktoba mpaka Desemba mwaka huu, bei hizo zimepanda kwa kasi ambapo mtungi wenye uzito wa kg 6 ulikuwa ukiuzwa Sh 16,000 kisha Sh 18,000 na sasa unauzwa Sh 20,000.

Wenye uzito wa Kg 12 awali uliuzwa Sh 32,000 ukapanda mpaka kufikia Sh 36,000 sasa unauzwa Sh 39,000 huku wenye kg 12 ambao ulikuwa ukiuzwa Sh 37,000 kisha Sh 42,000 sasa unauzwa Sh 49,000.

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo, akizungumza na Mwananchi jana kuhusu suala hilo alisema gesi inazalishwa pamoja na nishati ya mafuta hivyo bei ya petrol inapopanda na bei ya gesi inapanda.

"Kweli bei ya gesi imepanda na ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wetu kwa sababu ni bidhaa ambayo bei yake inadhibitiwa kwenye bei za soko la dunia," Kaguo alisema.

Kaguo alisema mwamko mdogo wa wafanyabiashara wa kuuza gesi nao unachangia kuongezeka kwa bei kwani wakiwa wachache wanaringa.

"Tumeanza kutekeleza hatua za awali za kuhamasisha Wafanyabiashara wengi wauze gesi ili kuwapata wengi na wauze kwa ushindani," alieleza.
 
Mpaka hii miaka mitano iwe imepita tutajikuta tumebanwa mbavu kila mahali..umeme juu, mkaa juu, mafuta ya taa juu, gesi nayo sasa haikamatiki...............kuni juu..........................mwisho wake utakuwa mlo mmoja baada ya siku mbili.................
 
Bei ya gesi yazidi kupaa
Tuesday, 28 December 2010 20:25

Mkuu ebu check hapo kwenye red color kama umerudia kg 12 mara 2.
 
Mie mwenzenu jana nimem2ma dada wa ndani akachukue akaambiwa imepanda akauliza nyie mbona mnapandisha bei kila siku ? muuzaji akamjibu kamuulize Kikwete? sasa mie ninachojiuliza gesi tanzania si ipo? na huu utetezi wa kuwa kwa sababu wafanyabiashara ni wachache naona ni wa kipuuzi kabisa...full ungese! ...

Nitarudi bidae na hii mada..
 
Mpaka hii miaka mitano iwe imepita tutajikuta tumebanwa mbavu kila mahali..umeme juu, mkaa juu, mafuta ya taa juu, gesi nayo sasa haikamatiki...............kuni juu..........................mwisho wake utakuwa mlo mmoja baada ya siku mbili.................

hii kitu tumeitaka wenyewe ngoja tunyooke kwanza labda tutafunguka akili na tutaanza kuona badala ya kutazama tu

watu kama kina dar es salaam sijui wana mtazamo gani kwenye hili..
 
PR wa Ewura na majibu mepesi mepesi ! Serikali na vita vya kutunza mazingira haviwezekani kwa spidi hii!
 
Saaaaaaaaaaaaafi saaaaaaaaaaaaaaaaaana huo mwanzo na baaaado Tutashika adabu! Si tunajifanya...Tunaipenda sana ARI ZAIDI<NGUVU ZAIDI,NA KASI ZAIDI....Ndo hiyo sasa. Si tuliitaka wenyewe......jamani au nasingizia ??????????? Slaa akaonekana mwenda wazimu?!!! Na kuna wengine wakisoma hii thread yangu wataniona kama na mimi ni mwenda wazimu..!!!!!!!!!!!!! yaani kunawatu wanafikiri Watanganyika tumeumbwa tupate shida...na yakuwa maisha yetu hakuna anaye weza kuyabadilisha labda MUNGU!!!!!!!!!!!!!!!!!..Ngoja MAISHA YATUKONG"OLI tushike adabu kwanza ndo tutajifunza 2015!!!......Chama Chetu cha KUpindua Daima ...ndio kimetufikisha hapa..!!!!!!!!!! BIG UP SANA Mzee wa kaya kaza buti ili watanzania wafumbuke vichwa!!! Wanyonye kabisa wabakie mbavu tu....
SI wanapenda Maisha duni au sio?
Si wanafaagilia chama chako au sio?
Si walisema hakuna chama kingine ila chama chetu au sio?
Si walikuwa wanaselebuka pamoja na wewe au sio?
Si wengine walisema wewe mteule wa Mungu au sio?
Si wengine Walikesha kwenye jua ili wakuone mkombozi au sio?
Waminye baba waminye ili wakufahamu vizuri au sio?
Wakamue baba wakamue ili vichwa vyao vifumbuke au sio?
Si ulisema hutaki kura zao lakini wakakupa au sio?
HIYO NDIO DAWA YAO SASA. KAZA BUTI KAKA KAZA KABISA
 
mie nitaanza kula kwa mama lishe,mana kupika mwenyewe naona gharama zinaongezeka tofauti na kununua kilichopikwa tayari
 
Mpaka hii miaka mitano iwe imepita tutajikuta tumebanwa mbavu kila mahali..umeme juu, mkaa juu, mafuta ya taa juu, gesi nayo sasa haikamatiki...............kuni juu..........................mwisho wake utakuwa mlo mmoja baada ya siku mbili.................

from Ari mpya,kasi mpya to Ari zaidi ,nguvu na kasi zaidi,bado safari ndiyo imeanza Dk Slaa alisema ni Itatugharimu kuirudisha serikali ya CCM madarakani,hata sikumoja alitamani Mungu awafungue macho watanzania waone tamaa ya uchu wa mali ulioko katika mioyo ya viongozi wao,na sasa kweli tunaiona gadhabu hiyo,huu ni mwanzo na miaka mitano itakuwa mingi sana kwa kasi hii iliyo zaidi.

Mungu atutetee kwa kuwa haikuwa mapenzi yetu wote bali ya wachache ili wapate kujifunza.
 
Saaaaaaaaaaaaafi saaaaaaaaaaaaaaaaaana huo mwanzo na baaaado Tutashika adabu! Si tunajifanya...Tunaipenda sana ARI ZAIDI<NGUVU ZAIDI,NA KASI ZAIDI....Ndo hiyo sasa. Si tuliitaka wenyewe......jamani au nasingizia ??????????? Slaa akaonekana mwenda wazimu?!!! Na kuna wengine wakisoma hii thread yangu wataniona kama na mimi ni mwenda wazimu..!!!!!!!!!!!!! yaani kunawatu wanafikiri Watanganyika tumeumbwa tupate shida...na yakuwa maisha yetu hakuna anaye weza kuyabadilisha labda MUNGU!!!!!!!!!!!!!!!!!..Ngoja MAISHA YATUKONG"OLI tushike adabu kwanza ndo tutajifunza 2015!!!......Chama Chetu cha KUpindua Daima ...ndio kimetufikisha hapa..!!!!!!!!!! BIG UP SANA Mzee wa kaya kaza buti ili watanzania wafumbuke vichwa!!! Wanyonye kabisa wabakie mbavu tu....
SI wanapenda Maisha duni au sio?
Si wanafaagilia chama chako au sio?
Si walisema hakuna chama kingine ila chama chetu au sio?
Si walikuwa wanaselebuka pamoja na wewe au sio?
Si wengine walisema wewe mteule wa Mungu au sio?
Si wengine Walikesha kwenye jua ili wakuone mkombozi au sio?
Waminye baba waminye ili wakufahamu vizuri au sio?
Wakamue baba wakamue ili vichwa vyao vifumbuke au sio?
Si ulisema hutaki kura zao lakini wakakupa au sio?
HIYO NDIO DAWA YAO SASA. KAZA BUTI KAKA KAZA KABISA

it sound funny but with reality.
 
..wakuu huyu Rytashubanyuma si pro-CCM,sasa analalama nini? au tayari ameshukiwa na Roho BWANA na sasa anaona mwanga wa ukombozi?
 
hivi tunaelekea wapi jamani hivi gas ingekuwa aipatikani hapa tanzania tungeishije jamani juzi nimekwenda kununua nikashangaa na roho yangu bei ilivyopanda
 
Back
Top Bottom