Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
Nipo Dar nataka nianze biashara hii ya kuku wa mayai ila nataka kijana mtaalam mwenye uzoefu naweza mpata wap? na maeneo mazuri ya kuweka banda ni wap nina plot bagamoyo kma heka 2 na plot ya "20 kwa 30" Goba panafaa kujenga banda la kuku 2000? au wap naweza kupata plot ya kujenga banda la kuku? plot (2m - 3m)

ujenzi wa banda la kuku wa mayai (kuku 2000) linagarimu kiasi gani cha fedha? mchoro stracture yake naweza ipata wap la kisasa na economical! ntashukuru kwa majibu yenu
 
Kuna mayai yanatoka mombasa kila siku kwa mafuso, je umejipanga ushindani?
 
Weka na siredi nyingine ya kutangaza nafasi ya kazi mkuu juu ya huyo kijana wa kuangalia hao kuku.............
 
Nipo Dar nataka nianze biashara hii ya kuku wa mayai ila nataka kijana mtaalam mwenye uzoefu naweza mpata wap? na maeneo mazuri ya kuweka banda ni wap nina plot bagamoyo kma heka 2 na plot ya "20 kwa 30" Goba panafaa kujenga banda la kuku 2000? au wap naweza kupata plot ya kujenga banda la kuku? plot (2m - 3m)

ujenzi wa banda la kuku wa mayai (kuku 2000) linagarimu kiasi gani cha fedha? mchoro stracture yake naweza ipata wap la kisasa na economical! ntashukuru kwa majibu yenu

Kuna wakati nilituma uzi nikauliza upatikanaji wa eneo la kukodi kwa ajili ya ufugaji kuku...... wadau wengi walikuwa na mawazo hasi hapa... ishu kubwa ni kukwepa mkataba kandamizi toka kwa unaekodi eneo lake.kuwa mwangalifu..
 
Kweli bado tunakosa umakini humu JF. Yaani 60% ya majibu hayamsaidii huyu mheshimiwa. @ Dr wa ukweli kama hujafanikiwa ni-pm nikuelekeze kwa mtaalamu wa mambo ya kuplan hivi vi2.
 
Waone balton wana mabanda wameyatengeneza kabisa yanaweza kuweka mpaka kuku2500 watakuelekeza zaidi unahitaji mtu mmoja tu kuangalia banda
 
waone balton wana mabanda wameyatengeneza kabisa yanaweza kuweka mpaka kuku2500 watakuelekeza zaidi unahitaji mtu mmoja tu kuangalia banda
Mkuu naweza kupata contact zao hao jamaa wanaotengeza mabanda?
 
Jenga banda/mabanda.Kila kuku mia(100 ) hula wastani wa laki tisa (900,000.MAX) kwa muda wa miezi mitano pamoja na matibabu.

Baada ya miezi mitano kuku wataweza kujilisha wenyewe,muda wakutoa mayai utakua umewadia.

Nakushauri ukianza usianze na wengi mia mbili au mia tatu nivizuri kwa kuanzia.
 
Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.

uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.

kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.

mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.

Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.
 
MKUU HONGERA SANA KWA JITIHADA ZAKO, MUNGU AKUSAIDIE ZAIDI NA ZAIDI.

- KUHUSU BIASHARA YA MAYAI, NI KWELI KABISA KUNA DEMAND NA KUNA COMPETITION KUBWA SANA MKUU, WAZALISHAJI NI WENGI SANA NA MASOKO NAYO NI KAMA HIVYO NI MENGI.

- MKUU UFANYE NINI SASA? NAKUSHAURI UFANYE JAMBO MOJA LA MSINGI SANA NA JARIBU KUJIBU HAYA MASWALI,

1. JE KUNA KITU CHA ZIADA KATIKA HAYO MAYAI YAKO YAANI UMEYAONGEZEA THAMANI?
2. JE WANUNUZI WAKO NI WA KUAMNIKIKA? MMENGIA NAO CONTACT NA KUSAINI MOU?
3. JE KWA NINI WATU WANUNUE MAYAI YAKO NA SI MAYI YA WATU WENGINE?
4. UKIPATA SOKO NA KUKAWA NA SUPPLY WENGI WA MAYAI YA KIENYEJI UTAWEZAJI KU KOMPITI NA HAO WENGINE?

- MKUU JARIBU KUTAFUTA NJIA YA KUYAONGEZEA THAMANI HAYO MAYAI YAKO HASWA KWENYE PAKING. USIISHIE KUWEKA KWENYE TRY NA KWENDA KUTAFUTA MTEJA.
- TAFUTA VIFAA VYA KISASA VYA KUPAKI MAYAI KIASI KWAMBA MTU ANAWEZA BEBA BILA KUHOFIA KUPASUKA KWA MAYAI.
- UKISHA PATA PATA HIYO PACKING NZURI YA KUWEZA KUPAKI HATA MAYAI MATANO MATANO, JARIBU KUTAFUTA SOKO KWA KUZUNGUKIA SUPERMARKET MBALAMBALI NA MIN SUPRTPARKET PAMOJA NA MADUKA YA REJAREJA, MKUU NINA UHAKIKA ASILIMIA 100% UTAPATA SOKO ZURI SANA ENDAPO UTAKUJA NA AINA MPYA YA KUPAKI MAYAI,

- WOTE TUSIISHIE KUPAKI KWENYE TRY YA MAYAI 30, TUJE NA AINA MPYA AMBAZO HATA HUKU KWETU SI NGENI SANA KWA SUPERMAKET KUBWA KAMA SHOPRITE,
eggs-egg-box_%7EIS252-023.jpg

027018.jpg

015808.jpg

k2827966.jpg

- MKUU JARIBU KUPAKI IDADI NDOGO NDOGO KAMA HII MAKE KUNA WATEJA HAWAHITAJI KUNUNUA MAYAI 30 TREI NZIMA KUTOKANA NA MAISHA YAO.

- SI KWAMBA HAYA MADUKA MAKUBWA YA MAKUBURU HAYATAKI KUNUNUA PRODUCT ZA WABONGO ILA NI AINA YA PACKEGING ZOTE NDO TATATIZO.

- TUNAISHIA KULALAMIKA KWAMBA WANAAGIZA MCHICHA TOKA SOUTH AFRICA, TUKIZANI TUNAWEZA WAPEKEKEA MCHICHA UKIWA UMEFUNGWA MAFUNGU MAFUNGU NA KAMBA ZA MIGOMBA WANUNUE.

INATAKIWA TUBADILIKE HASA KWENYE PACKEGING ZETU, TUSIISHIE KULALAMIKA NYAMA INAAGIZWA TOKA SOUTH AFRICA, HAYA MADUKA YANA MAINTAI QUALITY HAYA WEZI ENDA BUCHANI PALE KARIAKOO NA KUNUNUA TU NYAMA NA KUPELEKA MADUKANI MWAO,

MKUU HUO NDO MCHANGO WANGU,

nikitaka kununua mayai yako yote.....utaniuzia bei gan kwa tray? we ucpate tabu ya ku supply?
 
Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.

uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.

kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.

mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.

Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.

Kanyagio hongera, umejenga daraja na siye tunakuja kuvuka sasa hv...jamani nashauri tuanze kitengo cha agri marketing humu humu jamvini....a toast for our fellow kanyagio
 
Back
Top Bottom