Biashara ya kuagiza na kusafirisha Matunda

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Habarini wandugu....Nafikiria kufanya biashara ya matunda ila ni kusafirisha kwenda nje na pia kuagiza baadhi ya matunda ambayo hayapatikani kwa wingi kama Tufaa(Apple) je nini kinachohitajika kama kuna vibali ama leseni ambavyo vinanilazimu kuwa navyo kabla ya kuanza biashara husika.Natanguliza shukrani zangu.
 
ok mm najua kutoa nje apple uwe na kibali cha Tfda ambacho unakilipia kwa miezi kadhaa mitatu,sita au kwa trip na import permit ambacho unakipata pretoria haulipii ni bure..kwa apple iliyotoka South Africa inatakiwa uwe navyo ivyo na Sadc export permit ya kupitishia Zambia ili usipate usumbufu..
 
Nashukuru ndugu Isanga...nitakuja kwako tena kutaka details zaidi.
 
ok inatakiwa uwe na roli lako ndio utaondokana na adha zingine au ukishindwa kapakie mzigo uje kwa meli kupitia durban ingawaje gharama huea juu huko kuriko katika usafiri wako ikiweza nunua truck ilo na ulitumie kuleta mzigo wako likiwa na nambs za south Africa ili kuondoa usimbufu huko njiani namba za GP hazizimbuliwi kuriko mataifa mengine..na hayauzwi bei kubwa hayo maroli pia yapo mengi.
 
habari yako mkuu nilikua napenda kuuliza kama mtu akitaka kupeleka mchele south africa taratibu za kufuata zinakuaje Asante sana
 
Mkuu South Africa hawaitaji wanahitaji sana chakula na hasa mchele kutoka Tanzania wao wameupitisha katika ubora kuwa upo katika kiwango kizuri kuingia hawahitaji kibali chochote ni mchele tuu hata uwe na maroli mia watakachofanya boarder ni kukagua tuu kama hujauchanganya na madawa ya kulevya basi..vibali wanataka ukipeleka asali tena unapeleka sampo pretoria wizara ya biashara wakiikubali ndio unapita na kibali..mchele hauitaji kibali ingiza Tani yako ila pita Zambia,zimbabwe ndio SA usipitishie Botswana wanahitaji vibali pale ila kama una truck kwa ajili ya Zambia na Zimbabwe chukua kibali cha TFDA kwa ajili ya transit tuu kule mbele hakuna usumbufu wowote.,,
 
kikazi mchele ulikua hauna kodi unapoingiza SA sina uhakika na mwaka huu budget yao inasemaje maana kwa sasa mimi sisafirishi hiyo bidhaa ila mwezi ujao ntakwenda Pretoria ntauliza na hilo swala lako..,
Mkuu nami nasubiri mrejesho toka kwako!!!
 
kikazi mchele ulikua hauna kodi unapoingiza SA sina uhakika na mwaka huu budget yao inasemaje maana kwa sasa mimi sisafirishi hiyo bidhaa ila mwezi ujao ntakwenda Pretoria ntauliza na hilo swala lako..,
Asante sana Mkuu na je soko la mchele kwa south africa lipo pretoria au unaweza kuuzika mahali popote ukifikisha south africa?
 
mkuu waonekana una data nzuri za biashara za kusafurishaji bidhaa je ukitaka kuexport vitu vya utamaduni kaama vikapu, vinyago unachukua hatua zipi
Mkuu South Africa hawaitaji wanahitaji sana chakula na hasa mchele kutoka Tanzania wao wameupitisha katika ubora kuwa upo katika kiwango kizuri kuingia hawahitaji kibali chochote ni mchele tuu hata uwe na maroli mia watakachofanya boarder ni kukagua tuu kama hujauchanganya na madawa ya kulevya basi..vibali wanataka ukipeleka asali tena unapeleka sampo pretoria wizara ya biashara wakiikubali ndio unapita na kibali..mchele hauitaji kibali ingiza Tani yako ila pita Zambia,zimbabwe ndio SA usipitishie Botswana wanahitaji vibali pale ila kama una truck kwa ajili ya Zambia na Zimbabwe chukua kibali cha TFDA kwa ajili ya transit tuu kule mbele hakuna usumbufu wowote.,,
 
kikazi soko zuri lipo johannesburg na ili iwe rahisi kwa gharama ya usafirishaji tumia truck mpaka lusaka pale panda basi na pakia mzigo wako katika hayo mabasi yana Tela kubwa la kupakia 20 ft mzigo wowote, haya mabasi yanarudi tupu SA kwa hiyo gharama haitakua kubwa na pia ukishusha mzigo wako katika hayo mabasi wana godown kubwa iwe Shalom basi au joldan motors hawatakuchaji kwa wewe kutunza mzigo kwao ukitafuta wateja katika yard za hayo mabasi kuna wadada wa kitanzania wanauza chakula wateja pia wanawajua wanaweza kukusaidia iwe kwenye maduka makubwa au madogo na hoteli zipo utakapishukia hapo hapo...
 
ladyfurahia vinyago na vikapu naona Wamalawi wengi ndio ubeba na kupeleka Johannesburg na soko hasa lipo Cape Town kipindi kama hiki SA ni Summer time season mpaka mwezi wa kumi na mbili...Mapambo hayahitaji vibali kuingia SA kuna kodi kidogo sana boarder yao haiwezi zidi usd 200 au 300 kwa mzigo mkubwa sana huo unaweza ukapita njia yeyote hata ya Botswana hawasumbui unapita navyo ila rahisi ni ya Zambia pale ndio SA...Sema inataka ukae SA maana ukitaka uuze kwa kuwajumlishia naona watataka kwa bei ndogo ila ukiwa na sehemu ya kuuza ndio inakua rahisi kwa kule kuna mzee mmoja mkenya ndio kazi yake hiyo na mwingine anatikea mwenge Dar sina contact zao kwa sasa ningewauliza hawana shida kama ntapata taharifa ya soko zaidi ntakujulisha...
 
mnazid kunipa ushawish wa kufanya biashara za vyakula japo sina mtaji, siku nikizikamata tu, ndiko nitaanzia
 
ladyfurahia vinyago na vikapu naona Wamalawi wengi ndio ubeba na kupeleka Johannesburg na soko hasa lipo Cape Town kipindi kama hiki SA ni Summer time season mpaka mwezi wa kumi na mbili...Mapambo hayahitaji vibali kuingia SA kuna kodi kidogo sana boarder yao haiwezi zidi usd 200 au 300 kwa mzigo mkubwa sana huo unaweza ukapita njia yeyote hata ya Botswana hawasumbui unapita navyo ila rahisi ni ya Zambia pale ndio SA...Sema inataka ukae SA maana ukitaka uuze kwa kuwajumlishia naona watataka kwa bei ndogo ila ukiwa na sehemu ya kuuza ndio inakua rahisi kwa kule kuna mzee mmoja mkenya ndio kazi yake hiyo na mwingine anatikea mwenge Dar sina contact zao kwa sasa ningewauliza hawana shida kama ntapata taharifa ya soko zaidi ntakujulisha...
Na dhamani ya pesa ya tz na us chenji yake ikoje?
 
ukitaka kuuliza kama bidhaa inataka kibali au kodi kuingiza South Africa Address hii hapa chini simu na email..
TRADE AND INDUSTRY
The dti,77 meintjies Street,
Block A 3floor,
SunnySide, Pretoria 0001
Tel: + 27 (012) 394 5561 deputy information officer ukimuuliza huyo chochote anakupa majibu ya kodi na vibali viingiavyo SA ukiandika barua wanakujibu pia
email:contactus@thedti.gov.za
+ 012 394 3075
+012 394 0323
piga simu yeyote hapo atakaepokea mueleze unachotaka kujua wana huduma nzuri utadhani wanauza duka binafsi kumbe wafanyakazi wa serikali..
 
Habarini wandugu....Nafikiria kufanya biashara ya matunda ila ni kusafirisha kwenda nje na pia kuagiza baadhi ya matunda ambayo hayapatikani kwa wingi kama Tufaa(Apple) je nini kinachohitajika kama kuna vibali ama leseni ambavyo vinanilazimu kuwa navyo kabla ya kuanza biashara husika.Natanguliza shukrani zangu.
Apple zipo baba......sema tu mfumo wa usambazaji ni wa kizembe.......iringa pale yapo mazuri tu tena makubwa.....yana maji na sukari........ukiingiza utapigwa kabali ya kodi hadi ushike adabu
 
Back
Top Bottom