Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Qsm

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
444
251
2381603_Secondhand.jpg

Naomba msaada wenu nina duka la nguo la kawaida tu na lipo eneo zuri la biashara kinachonishangaza sipati faida kabisa je kuna yeyote kwenye biashara hiyo ambaye anaweza kunishauri jinsi ya kulisimamia? Mimi ni mfanyakazi kwa hiyo si mara kwa mara nakuwa dukani hapo.

Naombeni ushauri tafadhali.


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUELEWA BIASHARA HII
Ndg zangu wana JF naomba kusaidiwa mawazo katika biashara hii ya nguo za kike;

1. Mtazamo wako kama inalipa au hailipi
2. Location sahihi ni ipi?
3. Nitarajie changamoto zipi?

Pia, kama unaushauri mbadala nitaupokea na kuufanyia kazi.
Habari zenu wandugu;

Kwa wenye utaalamu wa biashara ya mitumba nahitaji elimu yenu. Wapi nitapata mabalo ya mitumba 1st grade? Ambapo hakuna kupigwa famba? Au jinsi ya kutambua grade nzuri?

Natanguliza shukrani!
Habari wana Jamii!

Niko US nataka sana kuanzisha biashara ya mitumba, ningependa kuuza marobota. Sasa basi kama kuna mwanaJamii anahusika na hii biashara ningependa kujua yafuatayo:

- Robota la grade A ni kiasi gani?
- Bora kuuza mnadani au kuwa na sehemu?
- Vipi usumbufu Bandarini?
- Ili kuchukua, approximately kiasi gani kuanza biashara?

Na kama una ushauri za zaidi ningeshukuru

Asante wanaJamii.
Wakuu habari zenu

Nina wazo la kufanya biashara ya kuuza nguo za mitumba kwa mfumo wa kununua Mabaro then kuyapeleka kwenye masoko mbalimbali, natafuta vijana wanazipiga mnada then mzunguko unajirudia kama kawa.

Mtaji nilionao mpaka sasa ni 5Million Tshs. Sina uzoefu wowote wa biashara, hivyo kwa yeyote mwenye kuielewa hii biashara please tupeane uzoefu.

Kwasasa bado nipo kwenye ajira, ila natamani sana kuanza kuwa mjasiriamali maana siko happy kabisa na suala zima la kuajiriwa, niliingia humo kwa lengo la kukusanya mtaji then nikafanye yangu.

Naomba kuwasilisha, napokea pia mawazo mapya.
Habari wadau,

Mwenye ufahamu wowote kuhusiana na zinapopatika nguo za mitumba kwa jumla, au njia za kupita ili kuweza kununua mitumba inayouzika.

Tupeana msaada wa maarifa hapa, Msaada sio lazima kumpa mtu mtaji au pesa pekee, hata kumuelewesha mtu njia za kupitia pia ni msaada mkubwa sana.

Ukizingatia hivi sasa hali ya uchumi imebana, hivyo kuna fursa kubwa sana hapa kwenye mitumba kwa kua ni bei nafuu ukilinganisha na first hand clothes.

Nahitaji msaada wenu wa maarifa na mawazo.

Ahsanteni


MAONI, USHAURI WA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
LENGA SOKO LA MKOANI, LETA MZIGO MKUBWA
Biashara ya nguo imekuwa ngumu sana kwa sasa kutokana na watu wengi kuivamia. Upinzani umekuwa mkubwa sana na ukiangalia kodi za flame zilivyokuwa juu ndio kabisaa.

Hii biashara nina experience nayo toka miaka ya 94 mpaka leo, miaka ya 94 na sasa tofauti ni kubwa sana kutokana na sababu hizo juu. Kutokana na ugumu huo wengi tunategemea wateja wetu wa siku zote miaka nenda rudi huku wao wakileta wenzao na wengine wachache. wapya.

Ningekushauri vitu viwili vitatu kama unataka kuendelea nayo manake sasa hivi kutokana na ugumu wake watu wengi wamekimbilia kwenye ukulima.

Cha kufanya unapoleta mzigo jaribu kutafuta soko mikoani. Unaweza kutafuta watu wa mikoani ukawauzia kwa jumla wao kama unaleta mzigo mwingi.

Kitu kingine jaribu kuleta mzigo mkubwa karibu na sikukuu kubwa zote,lazima hujue kutime hizi sikukuu kwnai hapo ndio biashara huwa kubwa na watu wanapenda mzigo mpya wakati huo.

Kitu cha mwisho wajue wateja wako, nikimaanisha jaribu kuangalia nguo zipi zinatoka zaidi ya nyingine, nguo za watoto ndio zaidi sijui kwako wewe kwahiyo unatakiwa kununua mzigo mkubwa wa nguo ambazo zinatoka sana.

Endelea na hizo hizo nguo za China kwani unalenga watu wenye kipato cha chini sio kila mtu anaweza kununua nguo kutoka Marekani.

Nakutakia kila kheri kwenye biashara yako.
LETA GRADE 1, CHANGANYA AINA YA MAVAZI

Ushauri wangu, lete hiyo mitumba tz 70% iwe ya kiume na 60% ya kike. Na kwakua unaanza lete grade 1, ili ujenge good will na wateja. Wahindi wanacho kifanya wanaleta grade tofauti kisha wanachanganya ili kupata super profit. Uzuri mmoja ni kuwa, ukileta mali nzuri mteja mmoja akifungua na kuona ni mzuri, huwaambia wenzake na wote huja kwako.

Kizuri kingine ni kuwa, kuna watu wana hela zao chini. Wao wanasubiri wasikie fulani kafungua mali nzuri na inakimbia. Yeye anakufuata, kisha anakupa hela ya belo zote ulizonazo store, kisha yeye anauza rejareja kama wewe ila anakuwa kaongeza elfu kumi au ishirini kwa belo! kwenye hii biashara, umakini mkubwa ni ubora wa hizo nguo. Na jinzi sio jinzi tu ziwe za kisasa, sio chupa (juu pana, chini inabana, hutouza) Nilishwahi kuingiza nguo frm TZ zamani from USA via charlestone port via S. Carolina zilinikata kwakweli!

Hakikisha kwenye huo mtumba, hakuna sox wala chupi TBS watakupa shida bandarini!

Kama unaweza, mkuu badala ya nguo za mitumba weka mitumba ya viatu vya kiume, au changanya nguo za mtumba na viatu vya mtumba ili upime biashara! open shoes, canvas, mukasin, sendoz raba n.k! Kikweli biashara ya viatu vya mtumba inakimbia kupita maelezo.

Huna haja ya kuwa na duka au stoo Kariakoo, wewe ukitangaza tu una viatu vya mtumba hasa vya kiume na kama utaweka kidogo vya kike visiwe kokoko, watu wananunua mali yote kwa siku moja! Ukiwa mvivu, utawauzia kontena lote, faida utaiona lakini ni kidogo sana ukilinganisha na watakachoenda kupata wao.

Kila siku asubuhi saa kumi uwe ushafika Kariaokoo (mchikichini) na baloo tatu au nne hivi, na kuhakikishia mpaka inafika kwenye saa moja asubuhi, unakuwa umemaliza mali yoote na unarudi home na furushi la kimango! Kule unakodisha meza kwa huo muda ni shilingi 5,000/- na vijana waaminifu wapo wa kukusaidia kulinda na kupiga debe, wewe kazi yako ni kupokea hela!

Kinachofanyika ni kuwa a day before upeleke hizo balo za viatu kariaokoo, unaita vijana wanatenganisha viatu vya kushoto na kulia, kwahiyo ukifika mchikichini asbuh unamwaga eiza vya kulia unabaki na vya kushoto and vice vser! Akikipenda kiatu unamtajia bei, bkoz kila kiatu kina bei yake, anakupa hela huku ameshika kimoja alicholipia! wakati wakufunga biashara, unampa mguu uliobakia.

Ofkoz, hadi mida hiyo lazima kuna pea kadhaa zinakuwa hazijapata wanunuzi, good news ni kuwa pembeni kuna watu kibao wanasubiri muhesabiane in a flat rate vyote vilivyobaki ana ku'cash wewe unarudi na hela home saa moja asbh na kuandaa mazingira ya kesho.

You can send mtu wako pale Mchikichini, mida hiyo asbuhi akathibitishe nilio kwambia!
Sina uzoefu sana, ila kwa sasa kila unapotembelea wauza mitumba wanadai wadosi wanachakachua sana Bales, linalosemekana grade 1 unakuta 75% ni gade ya mwisho kabisa. Kwahiyo source iliyobaki, reliable ni nchi za jirani kama Kenya na Uganda, ambapo kwa mfanyabiashara mwenye mtaji mdogo ni kitendawili.

Kwahiyo itategemea kama unaleta kusupply wauzaji wakubwa au wauzaji wa mwisho, Ila opportunity kutokana na mazingira hayo niliyokuambia ipo na tena nzuri. Kizuri kinajiuza jombaa.
KUWA NA CHAGUO LA NGUO ZA RIKA FULANI
Ni kweli watu wanafanya hii biz na ina faida ila kama ilivyo kwa biashara zote location ni muhimu pia hata bila locations ukipata contacts na kuweza ku satisfy taste na mahitaji yao waweza maintain soko. Kwa vile unaanza mtaji unatosha badala ya kwenda nairobi waweza muomba mtu akuletee uanze na mzigo mdogo ukiangalia taste ya wateja huku unatafuta contacts hata ikibidi beba kwa hanger kwa gari kuwafata.

Ukijua taste zao unaanza kwenda mwenyewe tena unakuwa kama unanunua ulizoagizwa zikifika tu nusu inaisha. Ila nadhani chagua kundi moja hasa rika lako au friends ili iwe rahisi kujua taste na ulipaji wao. Sio tofauti na wanaoleta nguo mpya toka sijui UK au US, nimeona watu wanauza hadi ml 2+ bila frame yoyote kwa kufata wateja.

Wanawake rika zote ndo soko kubwa sana, wanaume vijana sawa, watu wazima sidhani na pia frequency ndogo akinunua mwaka hadi mwaka hatakubali ya mkononi.
MAENEO MZIGO UNAPOPATIKANA KWA DAR
Balo zipo sehemu nyingi.
Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.

Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila si lazima iwe ivo.

Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wapi?

Ukifika Mnazi Mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.

Pili ukiwa Congo, K.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la Samsung.

Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za TTCL ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba hadi ya viatu wholesale bales.

Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za TTCL utaoneshwa.

Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.

Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.

Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngapi unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram

Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k

Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni
USIKATE TAMAA, INALIPA
Watu wasikukatishe tamaa ndg, tena mimi si kwa rafiki wala jirani, nilianza mtumba, kwa kununua bero moja tu pale mnazi mmoja, faida ikatoka karibu sawa na bei ya baro nikarudia.

Nguo za kike zinalipa, mashuka na viatu, za kiume suruali na mashati ila wanaume wanakamatika kiurahs ukiwafikishia maeneo yao ya kazi au kwa kufuatwa.

Nimewai kwenda Uganda, najua vizur pia huko, anzia nyumbani uimarike kibiashara, japo mimi nimeajiriwa serikalini lakn nafanya sana mtumba. Na ivi sasa naanza likizo june, nitaendelea na mtumba kama kawa.

Mil 3 ni nyingi, suala la kununua bero na au za kuotea za kutundika/mnada ni wewe tu na upendo wako, za bero lazima ukute na marapurapu ndani, ingawa huwa tunauza cheap, na hazikosi wavaaji au wanunuzi, za kuotea utauza zote bila kuacha rapurapu lkn je? Una uzoefu wa kuotea nguo? Yani ukiiona tu unapoint? Maana mnakuwa wengi katika ku point na wwngi ni wazoefu.

Hapo inahtaji mtu anaeona nguo tu nakujua hii ni sumu la sivo utaotea zote takataka au zinazokuvutia wewe binafs alafu zisivutie wateja.

Sehemu ya kupoint nguo ni ilala Boma, alifajir saa kumi na moja, baadae hakuna soko asbh meza ni za wanaouza kawaida kwa wapita njia.

Uliza swali kwa kile sikuandika nitakujibu.

Dresses za kike bero ya bei ya juu ni 380000/= kwa zile za kg 45, lakn unakuta bero ya top hadi 170000/= zinatofautiana kuanzia 150000/= mpk 400000/= hapo ndio juu sana kwa beri ya kilogram 45 na ukienda utaonesha hapa grade B hapa 1
Note: bero zinauzwa kwa kilogram, bei nilioweka ni. Kwa kg 45 ambazo mara nyingu utakuta nguo hadi 200

Bero za mil 1 ni kilograms 100 nk

Kuna maduka wana nguo uhakika. Naweza kukupa namba private nikakuunganisha.

Jaribu usikatishwe tamaa.
CHUKUA UZOEFU HUU
=> Nguo za watoto miaka 0-4, NDO ZITAKUTOA HASA WAKIUME BUKTA ZA JEANS, VIGAUNI YA WAKIKE PIA VINALIPA kumbuka watoto huvalishwa nguo zaidi ya nne kwa siku, hujikojolea kujichafua kwahiyo wanahitaji nguo nyingi kuliko rika lingne

=>NGUO za watoto utakayo muuzia MWANAUME ni bei ya juu kuliko MWANAMKE sababu ni kwa kuwa wanaume wengi hawajui bei za nguo kama akina mama

=> NGUO ZA WANAWAKE HASA WADADA ZINALIPA kumbuka wanaume hawana tabia za kununua nguo kama wanawake

=>BELO MOJA LA NGUO ZA WATOTO LINA NGUO 300 au 400 na kuendelea linauzwa GRADE Three 220,000/= GRADE TWO 350,000/=

GRADE ONE 600,000/= nyingne ni 800,000/=

Bei ni za Mnazi Mmoja DAR ES SALAM

=> UKICHAMBUA KARUME FANYA KUWAHI ASUBUHI SANA SAA 10 ASUBUHI UKACHAGUE

=>TAHADHARI: ufunguapo BELO ni sawa na nazi hujui kama ni nzima au mbovu ndani, UNAWEZA NUNUA UKAPATA NGUO NZURI MPAKA RAHA siku nyingne ukanunua zote mbovu haziuziki hata moja NDO BIASHARA ILIVYO
UZOEFU WA KUCHUKUA MZIGO NCHINI UGANDA
Nimependa ku share kuhusu biashara ya mitumba kutoka Kampala. Lengo ni kuwapa ufahamu kwa wale wenye interest. Safari yangu ya kwanza kwenda Kampala nilienda kama kutembea na kurudi na haya ndio niliyojifunza:

1. USAFIRI: Nilipanda bus la friends kutoka Bukoba mpaka Mutukula. Kumbuka lipo pia la kutoka Mwanza to Kampala. Kuna hiace/coaster za Bukoba mpaka Mutukula. Yapo pia mabasi yanayotoka Dar es Salaam to Kampala mfano Falcon, mengine siyajui. Kutoka mwanza pia Kuna mabasi mengine kama J4

2. KIBALI CHA KUSAFIRI DHARURA /Emergency travelers documents: Wengine sisi tumezoea kuita passport. Hiki hukatwa kwa mwaka mmoja. Taratibu zake ni cheti cha kuzaliwa na malipo ambayo ni elfu kumi kama sijakosea labda kama imepanda maana mimi changu nilikataa last year desemba. Kibali hiki kinakuwezesha kusafiri nchi tano mpaka sasa nazani including South Sudan ila sina uhakika. Unapokwenda Uganda ukipitia Mutukula, mihuri ya katika kibali chako unagongea Ofisi za Immigration za Uganda kwa kuanza na watanzania (exit) then Uganda (enter) and vice-versa kama utatoka Uganda kurudi Tanzania mihuri unagongea immigration ya Tanzania ila sijui kama imebadilika kwani ukisafiri kwa basi kila kitu Safi kwani utauliza kwa wazoefu au bus likifika border utaona tu wazoefu wa naelekea wapi.

3. KUBADILISHA FEDHA: Wapo watu wa ku change pesa from Tz shilingi to Uganda Shilling and vise versa, hapa epuka kubadilisha fedha kwa wale vijana wenye sare ambao wanatembea na pesa. Kuna maduka ya kubadili fedha kibao. Ukiwa mgeni na safari hizi jaribu kupiga mihuri uhamiaji then nenda ka change pesa kwa haraka maana Kuna watu huwa wanaachwa hapo kwa kuzuzuka na Mutukula.

4. KAMPALA: Ukifika Kampala utagundua tu utofauti wa kwetu Tz na Uganda. Waganda ni wachapakazi sana, biashara every corner of the city. Kuna sehemu nyingi za kufukia. Mimi nitajikita sehemu moja tu, kuna GEST inaitwa KAMPALA GUEST HOUSE iko karibu na Owino market. Bei za vyumba ni 20 mpaka 26. Kuna usalama wa kutosha na pia kwa sisi wazee wa second hand ni Bomba kwani Owino the market iko karibu.

5. MITUMBA YA KAMPALA: Hiki ndio kiini cha uzi huu. Jamani Kampala Kuna mtumba mzuri sana yaani najiuliza wao wanatoa wapi kwani ni mzuri sana, mashati, magauni, mikoba, mabegi, viatu, sweet pants n. K.

6. LUGHA: Hapa ndio kwenye shida sasa. Lugha kuu ni Luganda na Kiingereza katika mawasiliano kibiashara. Shida inakuja pale wanapojua sio wa kwao huwa wanapiga bei mbaya. Bora uwe na mwenyeji au jifunze Luganda katika kutamka pesa yao kama Lukumi (1000) mpaka milioni. Ila hata kiingereza poa cha msingi bei utakayotajiwa linganisha na ya huku nyumbani. Nashauri kwenye kununua marobota ni bora ukawa na mwenyeji muaminifu akusaidie kwani Kuna robota nyingine sio fashoinable yaani ni grade mbovu. Hakikisha unapata robota zuri usije ibiwa.

[HASHTAG]#Njooinbox[/HASHTAG] kwa maelezo zaidi au 0757463047 au 0676463047. Napatikana hewani zaidi ila nisipokuwa hewani simu inakua chaj.
MBINU ZA KUPATA MZIGO UGANDA
Huu ni mwendelezo wa kuhusu biashara ya mtumba kutoka Kampala.

Unapokuwa Owino Market jaribu kuuliza sehemu wanazouza kwa bei ya jumla. Sehemu ziko nyingiiiii sana kwani hata baadhi ya maeneo yaliyo mbali kidogo na Owino Kuna maduka ya Second hand whole salers kwa mfano maeneo ya Kisenyi Bus Terminal.

Ndani ya Owino market ni mwendo wa kutoa mguu niweke mguu maana ni watu wengi na kelele za wachuuzi za kukaribisha wateja wa retail. Ukitaka kununua kwa rejareja poa tu kwani ukiamka asubuhi saa moja, ukiwa na speed mpaka saa tano unaeza kuwa umenunua mzigo wa kutosha.

Kampala Kuna masharti ya mtumba mazuri sana. Mi huwa hata ofisini wanakubali na hata wale wa masharti ya shop special nawatoa knock out. Bei za masharti mazuri ni elfu kumi mpaka 20 ya kiganda. Ila kwa hapa nazunhumzia kwa wale ambao wanaotafuta ya kuvaa wao na sio ya biashara.

Kuna magauni na tops, pia blouse za kina dada nzuri sana yaani ukiingia Owino for the first time unaeza changanyikiwa.
Ukiwa Owino jaribu kukalili njia za kutoka maana unaeza jikuta unachanganya uliingilia wapi.

Kuna nguo za watoto nzuri sana. Unaeza nunua kwa issue binafsi au unaenda uza na kupata faida Kubwa
Karibu Owino sio kibiashara tu hata wale wapenda bling bling just go to Kampala for vacation and do shopping utaniambia mtumba ule hakunaga.

Kuna mikoba na mabegi ya mtumba mazuri sana. Hapa ngoja nikazie.

BIASHARA YA MTUMBA ILIYOPEWA KISOGO NA WENGI

Hapa naomba kuzungumzia second hand bags (mabegi, mikoba na pochi za mtumba).Wengi tumekuwa tukiangalia nguo na viatu tu na kusahau biashara moja ya bags. Napenda hapa nijikite na bags from Kampala (mivumba).Kampala Kuna bags nzuri sana, kuna mikoba, mabegi na pochi amazing. Unajua wanafunzi wanapenda begi nzuri na ngumu yaani kwa Kampala ni noma.

Vipi kuhusu mama zetu na dada zetu kwenye mikoba ;wanawake wa mji wanapenda kuwa na vitu unique bhana, Leo msibani ana pochi hii, kesho sokoni ana mkoba huu, keshokutwa saloon au jumatatu mpaka ijumaa kazini ana change mikoba tu sio anarudia mkoba mpaka unapauka kwa Jua.

Unajua Akina dada wakikutana kwenye shughuli zao hupenda kuwa wamependeza from toe to head, sasa mkoba muhimu au pochi. Kuna Luis Vuitton, Anna Sui, Gucci, Prada etc za mtumba.

Mabegi ya shule pia yapo mazuri sana na ukiwa mjini yapo unauza hata 40 kulingana na uzuri na ugumu wake.
Jaribu kufanya hii biashara kwani ukichukua mzigo the mtaji flani mkubwa hautajuutia aisee kwani biashara hii inaihitaji iwe na mzigo wa kutosha.

Kwa mfano umechukua mzigo wa milioni mbili za kibongo ukapata mzigo wenye items 600, ukaamua kila item uuze elfu 10000 utapata ngapi? Na hapa umepigia kwa bei flatlet, kumbuka Kuna mikoba ipo ya mpaka 20,, 30 na zaidi kulingana na eneo ulipo, sio uwe Chato au Buseresere afu utegemee uuze kwa bei kubwa utajikuta biashara yako unasubiri mwisho wa mwezi tu salary itoke ndio uuze.

[HASHTAG]#karibu[/HASHTAG] tuunge umoja kibiashara yaani kufanya safari za kibiashara Kampala tupige hela kabla mtumba hujapigwa stop 2018
Wale wa Mwanza, Dodoma,Geita Musoma n. K nafasi ni hii sio lazima tuende Dar. Afu mtumba wetu unachachuliwa sana.
ZINGATIA HAYA UWAPO UGANDA
Mwendelezo,
Hapa nitazungumzia machache tu yafuatayo:

1. USALAMA: Kampala ni jiji ambalo liko poa kwa usalama. Kuna polisi wanafanya sana doria. Zingatia kutembea na passport au Hati ya dharura ya kusafilia kwani polisi wa Uganda wana tabia ya usumbufu pale wanapokukuta huna passport kwa wageni. Wanaweza kukupeleka sero au kudai kitu kidogo. Wengi unaweza sema umeacha hotel wakakuelewa au wasikuelewe. Point ya msingi tembea na passport yako. Kwa mfano kwa wale wapenda kujirusha, unaweza ukawa unarudi from club usiku kwenye pikipiki afu ukakutana nao wakakusimamisha afu uwe hauna passport hapo shida sana.

2. CHAKULA: Hapa mimi ndio sehemu yangu maana katika safari zangu hata saa moja asubuhi nitakula mishikaki na chapati na yai za kutosha. Kwa vyakula wako vizuri. Mimi kwa bahati mbaya huwa sili hoteli kubwa au migahawa ya gharama. Mama ntilie wengi chakula ni elfu 3000 au hata pungufu. Baadhi ya migahawa bei ni zile zile tu ila msosi wake mzuri. Samaki, nyama, matoke etc. Hapa usiwe na wasiwasi it's like home TZ. Ila kwa bahati mbaya ndugu zetu mapishi ya wali kidogo shida kwani hapa utatajikuta unakumbuka mapishi ya wali ya Kitanga, kizaramo, kilugulu etc.

3. PERSONAL SHOPPING: Hapa sio kibiashara bali mwendo wa kununua upendeze binafsi. Ukitaka kuenjoy zaidi hapa ujue luganda kidogo hata ya kuibia kama ifuatavyo:
*1000 Lukumi
*1500 Lukumi mu bitano
*2000 nkumi bili
*2500 nkumi bili mu bitano
*3000 nkumi Satu
*3500 nkumi Satu mu bitano
4000 nkumi nnya
*5000 nkumi tano
*6000 kakaga
*7000 kasamvu
*8000 kanana
*9000 kenda
*10000 mtwalo
*11000 Mtwalo gumu mu lukumi
*12000 mtwalo gumu mu nkumi bili
*13000 Mtwalo gumu mu nkumi satu
*14000 mtwalo gumu nkumi nnya
*15000 mtwalo gumu mu kitundu (hii kitundu inatamkwa Chitundu)
*16000 mtwalo gumu mu kakaga
*17000 mtwalo gumu mu kasamvu
*18000 mtwalo gumu mu kanana
*19000 mtwalo gumu mu kenda
*20000 mitwalo ebili or bili
*21000 mitwalo ebili mu lukumi
*22000 mitwalo ebili mu bili
*23000 mitwalo ebili mu satu
*24000 mitwalo ebili mu nnya
*25000 mitwalo ebili Chitundu au mitwalo ebili mu etano
*30000 mitwalo esatu
*35000 mitwalo esatu Chitundu
*40000 mitwalo enaa
*50000 mitwalo etano
*60000 mitwalo mkaga
# pardon my poor luganda

*How much - sente meka
*Discount /nipunguzie - nkendelezako. Hapa anaweza kukuuliza una shilingi ngapi - oina sente meka?
*I want - njagala
*webale - thank you, maana ukiwa Uganda hasa Kampala utakaribishwa kw kuvutwa au kushikwa mikono we mpaka basi, wenzetu kama ni biashara wanajua.
*I will give you - njakuwa
#ni mengi ya kuandika

You can mix luganda and English Unapo ulizia bei za vitu iwe mtumba, special au hata vitu vingine.

4. Kampala Nightlife: Hapa ndio shida Sana. Wanawake wa Kiganda wameumbika bhana so if ukiwa on business trip for men uwe makini maana Kampala mdudu HIV wa kumwaga. Shida nyingine dadaz with UG wakopenda sana WaTZ yaani wakijua MTZ shida. Vipo viwanja vingi sana kama Club Ambiance, Ange Noir etc. Kuna sehemu inaitwa Kabalagala huko Kuna bar na night clubs nyingi. Kiwanja kizuri ni Club Ambiance. So if you make a trip fanya kwanza kilichokupeleka then kama ni mtu wa bata ule bata ila zile totozi usipojipanga utakosa hata nauli us kurudi TZ

Yako mengi, haya ni machache tu. KARIBU KLA CITY
 
Qsm,

Nataka kukushauri ila kwanza naomba unijibu hili swali/maswali kwani sikuona kokote ulipoeleza kwenye post yako.

Je, unapata hasara na biashara/duka lako ina muda gani?
 
Ikiwa hakuna faida kwa miaka mitatu yote na labda pia huna hasara inawezekana ni usimamizi mbaya.

Hakikisha unajitahd baada ya muda wa kazi pita dukani angalia mauzo ya siku hiyo, weka kumbukumbu ya kila bidhaa inayoingia na kutoka dukani kuwa na daftari lenye kumbukumbu za vitu vyote naamni kama nguo zinatoka na unaingiza nyingine lazima kuwe na faida.
 
Acha kuuza nguo zilizotoka Uchina, Dubai etc zisizo na ubora, usifuate mkumbo, uza vitu bora, unique vitanunuliwa.
 
Acha kuuza nguo zilizotoka uchina, Dubai etc zisizo na ubora, usifuate mkumbo, uza vitu bora, unique vitanunuliwa

Kwani kasema anauza za Kichina? lakini pia sioni shida iwe ya kichina ama inatoka uk mradi ipate mteja, ni kuchagua tu zile zilizopo kwenye fashion kulingana na wakati uliopo.
 
lina miaka mitatu sasa

Miaka mitatu ni mingi kwa biashara kama hiyo yako ya nguo. Nadhani kuna mambo machache tu unahitaji kufanya ili uweze kuiona faida hiyo ya hicho unacho kifanya.

Kama biashara/Duka linajiendesha lenyewe kwa maana lina lipa kodi zote za nyumba,TRA na Mishahara au mshahara kwa kipindi chote cha miaka mitatu,basi hilo duka lako lina faida sana, tena sana.

Kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyo shauri, fanya uwe unaangalia ana uwe na muda na biashara na hesabu zake zote, usiache kila kitu kwa mtu/watu bila ya uangalizi wako mwenye.
 
Pia angalia upande wa choice, labda hukidhi mahitaji ya wateja.
 
Acha kuuza nguo zilizotoka uchina, Dubai etc zisizo na ubora, usifuate mkumbo, uza vitu bora, unique vitanunuliwa

Sawa ila nguo hizo ndizo zinanunuliwa sana maeneo hayo, lakini nitalifanyia kazi wazo lako.
 
Dada huyu hajasema anauza nguo za China au Dubai, sasa kwanini ufikiri hivyo? Halafu JF ni The home of Great Thinkers?

Dada ni hivi

1. Nenda kwenye mipango ya awali uliyopanga kwa ajili ya duka hili.
2. Je, mipango inafuatwa?
3. Kwanini mipango inafuatwa na bado kuna hasara?
4. Je, kuna tofauti yoyote ya mauzo ya mwanzo na sasa?
5. Je, mtaji wako umeongezeka au umepungua tangu ulivyofungua?

Ninachoona hapa ni usimamizi hafifu, unajua unapoanza biashara changa ni kama mtoto mdogo anatakiwa atunzwe kwa karibu na usimamizi makini ndipo aweze kukua na kujisimamia mwenyewe.

Kwa biashara mpya unabidi usimamie kwa karibu ujue maendeleo ya mwanao (duka hili).

Usitumie pesa ya mtaji na ukumbuke kurudisha mtaji (kureinvest)

Mambo mengine je kuna ushindani mkubwa kutoka biashara za karibu,lazima zipo! Je duka au biashara yako inakidhi mahitaji ya wateja uliowalenga? Ubora wa bidhaa, bei nk.

Je, huduma kwa wateja inaridhisha? Au msimamizi ndiyo amekuwa kama ndiye mfalme wakati wafalme ni wateja!!!

Kwa ufupi unahitaji kwenda kwenye biashara yako na kuchunguza mambo madogo na ya msingi kama hayo juu ndipo utakapogundua pesa inaungulia wapi.

Yapo mengi ya kufanyia kazi lakini hayo hapo juu ni ya msingi ya kukuonyesha muelekeo.
 
Biashara ya nguo imekuwa ngumu sana kwa sasa kutokana na watu wengi kuivamia. Upinzani umekuwa mkubwa sana na ukiangalia kodi za flame zilivyokuwa juu ndio kabisaa.

Hii biashara nina experience nayo toka miaka ya 94 mpaka leo.miaka ya 94 na sasa tofauti ni kubwa sana kutokana na sababu hizo juu. Kutokana na ugumu huo wengi tunategemea wateja wetu wa siku zote miaka nenda rudi huku wao wakileta wenzao na wengine wachache. wapya.

Ningekushauri vitu viwili vitatu kama unataka kuendelea nayo manake sasa hivi kutokana na ugumu wake watu wengi wamekimbilia kwenye ukulima.

Cha kufanya unapoleta mzigo jaribu kutafuta soko mikoani.unaweza kutafuta watu wa mikoani ukawauzia kwa jumla wao kama unaleta mzigo mwingi.

Kitu kingine jaribu kuleta mzigo mkubwa karibu na sikukuu kubwa zote,lazima hujue kutime hizi sikukuu kwnai hapo ndio biashara huwa kubwa na watu wanapenda mzigo mpya wakati huo.

Kitu cha mwisho wajue wateja wako,nikimaanisha jaribu kuangalia nguo zipi zinatoka zaidi ya nyingine,nguo za watoto ndio zaidi sijui kwako wewe kwahio unatakiwa kununua mzigo mkubwa wa nguo ambazo zinatoka sana.

Endelea na hizo hizo nguo za China kwani unalenga watu wenye kipato cha chini sio kila mtu anaweza kununua nguo kutoka Marekani.

Nakutakia kila kheri kwenye biashara yako.
 
Newazz na Arsenal Wenger nawashukuru mno mno kwa mchango wenu nitafanyia kazi maoni hayo kwani nina uzembe mkubwa wa kusimamia na kufuatilia kwa karibu duka langu.
 
Wajua sasa biashara ya nguo imesambaa kila kona. Kama unaweza kubadrisha bidhaa katika duka lako au uwe unaenda na catalogue mpya mpya. Kuwa up todate kila siku.
 
Hebu pata likizo halafu simamia mwenyewe kwa muda ili uone mwelekeo.
 
Kama huwezi kukaa mwenyewe kwa muda mpe muuzaji likizo. Inawezekana anauza na kununua tana bidhaa bila wewe kujua, faida anachukua.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom