TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,467
- 11,166
Wakuu kutokana na hali halisi ya uhaba wa nafasi za ajira nchini mwetu, pamoja na msisitizo kutoka Serikalini kuwa vijana tutafute namna ya kujiajiri kwa kufanya biashara halali basi ninafikiria kuanzisha hii biashara kama mwitikio wa ushauri wa viongozi wetu kuhusu kujiajiri. Hivyo basi kutokana na vijisenti nilivyobakiwa navyo (ambavyo vinakaribia kuisha), nimefikiria aina nyingi sana za biashara lakini asilimia kubwa tayari zina ushindani mkubwa. Hivyo ninafikiria kutafuta nyumba kwa ajili ya utoaji wa huduma hii kwa wateja.
Kwa kuanzia nitaajiri watanzania wenzangu (Mabinti 10) ili nao pia waweze kujipatia kipato cha kujikimu, huko mbeleni nitaifanya biashara iwe ya kimataifa zaidi kwa kuajiri pia wageni, hususani kutoka mabara ya Ulaya, Asia pamoja na Amerika ya Kusini. Wafanyakazi wangu wote nitahakikisha wanapimwa afya zao kila mwezi ili kuweza kujihakikishia usalama wa wateja wangu.
Pia nitaingia mkataba na Kampuni ya Ulinzi na eneo langu la biashara litakuwa na Ulinzi masaa 24. Ninaangalia pia utaratibu wa kufungua massage parlor ambayo itakuwa inatoa huduma za massage hususani erotic massage kwa wale ambao hawatahitaji huduma nyingine.
Sasa basi, ningependa kupata ushauri wenu wadau, ni maeneo gani yanafaa kufungua hii biashara (ninafikiria Ubungo ama Mwenge, naomba mawazo yako). Pia kuweza kufahamu utaratibu wa kufuata ili kuweza kupata kibali cha Serikali ili niweze kuanza biashara (ili niweze kuchangia Taifa langu kwa kulipa kodi).
Kwa yeyote aliyewahi kuifanya hii biashara naomba kujua ni changamoto gani nitaweza kukumbana nazo kwenye huu uwekezaji?
Ni matumaini yangu kuwa mtanipa mawazo kuntu.
Asanteni sana.
Mapendo
TANMO.