Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Habari wanajamii, nlikua na wazo la kuanzisha local bakery kwa kutumia jiko la mkaa kwa ajili ya kutengeneza mkate na kuuza katika eneo nnaloishi na thamani ya hilo jiko ni 350,000 ila total cost na vifaa vyao vingine ambavo wamenitajia ni 450,000 na nlikuwa naomba msaada nijue ni gharama gani inatakiwa katika kuendesha biashara ya Mikate na hilo jiko lina uwezo wa kutoa mikate 18 kwa Batch 1 na nlikua na wazo la kutoa mikate 90 kwa siku ili nione hali halisi ilivo na nlikua nataka nijue gharama ikoje na hali ikoje.

Ntashukuru kwa msaada na nlitaka niuze kwa 800 per bread.
 
Habari wanajamii,nlikua na wazo la kuanzisha local bakery kwa kutumia jiko la mkaa kwa ajili ya kutengeneza mkate na kuuza katika eneo nnaloishi na thamani ya hilo jiko ni 350,000 ila total cost na vifaa vyao vingine ambavo wamenitajia ni 450,000 na nlikua naomba msaada nijue ni gharama gani inatakiwa katika kuendesha biashara ya Mikate na hilo jiko lina uwezo wa kutoa mikate 18 kwa Batch 1 na nlikua na wazo la kutoa mikate 90 kwa siku ili nione hali halisi ilivo na nlikua nataka nijue gharama ikoje na hali ikoje.

Ntashukuru kwa msaada na nlitaka niuze kwa 800 per bread

Wazo zuri sana hili.
Changamoto ni hizi hapa.
  • Jiandae kupata 'usumbufu' toka kwa bwana afya wa kata.
  • Jiandae kukabiliana na 'mizengwe' ya jamaa wa TFDA na TBS.
 
Thanks sana kwa kunipa changamoto za hii biashara ndugu na je gharama zinakuaje kwa mkate mmoja,unahitaji unga kiwango gani na vitu gani vingine vya ziada?Jamaa wa TFDA na TBS nadhan itakua rahisi mana kama ntakua natengeneza na kwenda kuweka katika duka kwa ajili ya kuuza
 
Kaka wewe ndio mwenye recipe ya kuhoka mkate. Ushari nunua kilo moja ya ngano kisha jumlisha ingratiate zote za mkate za kutosha Kwa kilo moja. Kisha angalia kilo moja itatowa mikate mingapi chukua gharama gawa Kwa idadi.

Mfano ngano 1000, Amira 2, 200, sukari 1/2kg 300 na vinginevyo 500. Jumla 2000 na unapata 10 mikate basi gharama yako itakuwa 200 jumlisha Mark up 80% ( my favorite) then sale price is 360. Make sure una include labor charge per mkate. Let me know kama unaitaji help Kwenye pricing
 
Thanks sana kwa kunipa changamoto za hii biashara ndugu na je gharama zinakuaje kwa mkate mmoja,unahitaji unga kiwango gani na vitu gani vingine vya ziada?Jamaa wa TFDA na TBS nadhan itakua rahisi mana kama ntakua natengeneza na kwenda kuweka katika duka kwa ajili ya kuuza

Mkuu kama upo dar nenda SIDO Vingunguti
 
Thanks sana kwa kunipa changamoto za hii biashara ndugu na je gharama zinakuaje kwa mkate mmoja,unahitaji unga kiwango gani na vitu gani vingine vya ziada?Jamaa wa TFDA na TBS nadhan itakua rahisi mana kama ntakua natengeneza na kwenda kuweka katika duka kwa ajili ya kuuza

Hawa jamaa wa ofisi ya kata na jamaa wa TFDA na TBS huwa ni wasumbufu tu.

Huwa wanatumia sheria zao kusumbua wazalishaji wadogo wa bidhaa.

Mfano wa usumbufu wao ni kama vile 'traffic police' wanavyosumbua madereva barabarani.

Yaani uwe na kosa, au usiwe na kosa watakuja kusumbua. Itabidi utoe 'ushirikiano' kwao kama vile madereva wanavyotoa 'ushirikiano' kwa traffic police barabarani.

Mara utasikia, mikate yako haina viwango vya TBS na TFDA, mara 'kiwanda' chako kiko maeneo ya makaazi ya watu, mara mikate yako haina mifuko maalum ya kuitambulisha, n.k.

Hapo ujue 'kitu kidogo' ndio mpango mzima.
 
Samahani kwa usumbufu ila what if nkianza na mtaji wa Laki 6 kwa kununua kila kitu like mashine na unga na vitu vingine vinavyochangia katika utengenezaji wa mikate
 
Ni idea nzuri sana jordan23. Mimi pia nina hilo wazo ila nataka kupika cake tu sio mikate. na nimeplan kuanza hiyo business. Naomba tu unifahamishe umepanga kutumia mixer gani kuchanganya unga wa mkate? Natafuta mixer nzuri itakayoweza kuchanganya unga kilo 4 na zaidi. Anayejua tafadhali anijulishe.
 
Habari wanajamii,nlikua na wazo la kuanzisha local bakery kwa kutumia jiko la mkaa kwa ajili ya kutengeneza mkate na kuuza katika eneo nnaloishi na thamani ya hilo jiko ni 350,000 ila total cost na vifaa vyao vingine ambavo wamenitajia ni 450,000 na nlikua naomba msaada nijue ni gharama gani inatakiwa katika kuendesha biashara ya Mikate na hilo jiko lina uwezo wa kutoa mikate 18 kwa Batch 1 na nlikua na wazo la kutoa mikate 90 kwa siku ili nione hali halisi ilivo na nlikua nataka nijue gharama ikoje na hali ikoje.

Hongera sana kiongozi! unataka kufanyia biashara hii wapi? kwanini umeamua kutumia jiko la mkaa? Mashine ya kukandia unga unayo? nijibu hayo nitajaribu kukusaidia japo kwa mawazo maana na mimi nilipitia njia hiyo.
 
Sina uzoefu na aina hiyo ya jiko unalotaka kutumia,mahitaji muhimu katika kutengeneza mkate bora ni unga, sukari, chumvi, margarine, improver, calcium na hamira. Vitu ukinunua kwa jumla ndio huwa inalipa zaidi kuliko rejareja, mfano kiroba cha unga azania/azam 50kg ni sh 54,000/= una uwezo wa kutoa mikate zaidi ya 200(kutegemea na uzito wa mkate,hapa ni 500gms).

Siku hizi kila kitu kipo hapa mjini, ukitembea mitaa ya posta karibu na jm mall kuna maduka yanauza hizi mashine za ukubwa tofauti, kuna wengine niliwaona Kariakoo.
 
Habari wakuu,

Kama una ndoto ya kuwa na bakery ninatoa ushauri wa namna ya kuanzisha katika maeneo yafuatayo:

1. Vifaa (equipments) muhimu vinavyohitajika na wapi kwa kupata kwa bei na ubora. Vifaa kama commercial oven, mixer machine, loaf slicer, workbench, bread and cakes moulds, proofer etc
2. Upatikanaji wa bakery ingredients na accessories kwa ajili ya cakes na bread.
3. Utaalamu wa upikaji keki na mikate, cookies, biscuits etc
4. Na mambo yote kwa ujumla katika tasnia ya bakery etc

Utaratibu wangu wa kazi ni ushauri na wapi utapata huduma zote nilizoainisha hapo juu.
 
Tangazo la biashara au unamwaga maujuzi ili wanajamvi wafaidike?
 
Gharama ndio zenyekuwafanya mana JF tupate hamasa yakujiingiza katika biashara husika, unaweza kunidokeza nawza kuanza nakiasigan tafadhali.
 
Natumaini unayesoma hapa uko poa salama salimini.

Naomba unijuze garama ya kufungua bekari ya mandazi na mkate, na mengine yote yanayohusiana na hiyo biashara.

Asante
 
Natumaini unayesoma hapa uko poa, salama salimini.

Naomba unijuze garama ya kufungua bekari ya mandazi na mkate, na mengine yote yanayohusiana na hiyo biashara.

Asante

Hiyo bznes inamilikiwa kwa %kubwa na wapemba na wahindi sitegemei kama utapata ushirikiano wa kutosha mkuu.
Jaribu kwenda madukani kuulizia mitambo kwajili kuokea hiyo bidhaa from there u will get to know where to start.
 
Vifaa vinavyohitajika ni Oven kwa ajili ya kuokea mikate, slicer kama utahitaji kuuza mikata iliyokatwa slice ,machine ya kukandia unga, pan za kupikia mikate, mzani nk. Gharama kubwa ni oven, sliber machine na ya kukandia lakini itategemea wewe unataka uanze bakery ya kiwango gani.

Kama ni home bakery unaweza kuanza hata kwa oveni ya jiko la mkaa ambayo unaweza yapata Sido taratibu biashara ikakua.

Commercial bakery lazima uwe na vyumbavya bakery ambavyo TFDA watakagua na kukupa kibali hawa jamaa wana masharti yao ugonjwa wa moyo,tembelea ofisi zao watakueleza.

Vifaa vya bakery nenda kariakoo maeneo ya Goldstar ,na Mtaa wa Samora kuna duka linauza.

Kama unafungua bakery na ukataka vifaa vyote hivyo si chini ya 15m we zunguka mjini utapata majibu.
 
Safi sana kwa maelezo yasiyo na uchoyo kaka.
 
Back
Top Bottom