Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

RealTz77

JF-Expert Member
May 18, 2009
738
40
2397197_bajaji_1.jpg


Nawasalimu wakuu woote wana JF. Mwenzenu nimepata kamshiko kama 8m sasa ninataka ninunue bajaj najua hapa mjini Dar zinatumika sana, naomba kwa yeyote mwenye uzoefu anisaidie ni Shs ngapi dereva anatakiwa alete kwa siku au week? Nashukuru naelewa humu ndani wapo wengi wanaofanya hii biashara. Je, is it worth?

Asanteni sana, nasubiri majibu hapo chini.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UELEWA WA BIASHARA HII
Ndgu wadau mimi n mkaz wa jiji la Mwanza ktk hali ya kutaka kujikwamua kiuchumi nimedhamiria kuanza biashara ya kusafirisha abiria kwa usafiri wa bajaji. Kwa hali hiyo kwa wenye uzoefu naomba msaada wa mambo yafuatayo:

1. Naomba kufahamu bei halisi ya kununua bajaji mpya.
2. Tahadhari muhimu za kuchukua/kuzngatia pindi naponunua bajaji mpya
3. Naomba kufahamu taratibu muhimu za kufuata kabla ya kuanza biashara hii.
4. Changamoto za biashara hii.
5. Ushaur juu ya mahali panapolipa zaid kwa wenye uzoefu na mazingira ya jiji la Mwanza
6. Ushauri kuhusu mengineyo.

Natanguliza shukran zangu kwa wote mtakao amua kutumia muda wenu kunisaidia kimawazo ktk harakat zangu hizi.
Habari zenu humu ndani,

Mimi ni mfanya biashara mdogo na sina muda mrefu tangu nianze biashara, najihusisha zaidi na biashara ya suti za kike ambazo naziuzia mkononi,sina duka ila natafuta wateja maofisini na sehemu mbalimbali nawapelekea, sasa nimepata hela kama 11millioni nafikiria kununua bajaji moja na bodaboda moja ili niziweke katika biashara sijui mnanishaurije katika hili je zinalipa?

Au ni biashara gani naweza kuanzisha ambayo itaniingizia faida nzuri?

mpango wangu ni kuwa nataka biashara ya suti ijiendeshe yenyewe na mtaji ukuwe kutokana na faida inayopatikana kwenye suti ndio maana hiyo hela nataka niifanyie biashara nyingine.

Sijui nimeeleweka?

Ahasanteni sana nathamini sana michango yenu.


MICHANGO YA WADAU
MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA

Hii biashara ni nzuri lakini ina changamoto zake kama zilivyo biashara nyingine. Kwa kifupi nikupa yale machache ambayo ni ya kuzingatia katika hii biashara.

1. Hakikisha chombo kinalala kwako, maana usipofanya hivyo madereva wa bajaj wana kawaida ya kukifanyisha chombo kazi kwa muda wa saa zote 24 za siku kwa utaratibu wa kuwaachia deiwaka. Halafu wewe anakuletea Tsh 15000 tu, wakati unaweza kukuta wametengeneza hadi Tsh 70,000 (Kama siku ikiwa nzuri sana) kwa siku.

2. Hakikisha unasimamia service na uwe na rekodi ya siku unayofanya service maana usipofanya hivyo, kuna uwezekano ukaambiwa kuna service imefanyika ilipe utoe hela wakati hakuna kilichofanyika. Hii inaweza kufanya chombo kikachoka haraka hadi ukashangazwa.

3. Kama huna utaalamu hata kidogo na mambo vyombo vya moto, sikushauri hata kidogo kununua bajaj zilizotumika maana utatumia hela nyingi sana kulipa mafundi na kununua spea. Ni vizuri ununue vyombo vipya na pia usikae navyo sana, fanyia kazi si kwa zaidi ya miaka miwili, uza na ununue vingine.

4. Usiwachekee kabisa hao madereva kwenye masuala ya hesabu maana hawachelewi kukuletea stori za biashara mbaya wakati wakipiga hela hawakuongezi hata sh 100 kwenye hesabu yako. Kama biashara mbaya weka deni, siku zijazo wajazie hiyo hesabu.
KUWA MAKINI. TAFUTA DEREVA MWAMINIFU
Ngoja nikujibu

1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=
Kusema kwamba asilimia kubwa anapata Dereva na kumpangia hesabu anayopata yeye wakati yeye yupo njiani na wewe upo nyumbani.

Sasa we kwa akili yako ya kijani unafikiria kwamba anachokipata yeye na kwa juhudi zake kubwa za kufanyakazi katika mazingira magum ndio mgawe sawa?

We si umesign mkataba? Na mikataba yote kwa wazoefu wa Biashara na hesabu za Tajiri zinafahamika.
Hii ni sawa na Daladala, huwezi kusema eti wanachopata wafanyakazi kikubwa kuliko chako, wakati wenzio wote ndio wanavyofanya, mbona siku ya hasara hamsemi mgawe hasara pamoja.

Nakuonea huruma sana kwamba kasi ye maendelea ya dunia ya sasa katika biashara na maisha kwa ujumla imekuacha mbali sana.

2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kwa mwez, au moja, mbili ni bora zaidi

Hesabu inafahamika kwa wiki na kuna siku inaachwa. Na kwa kukushauri tu ni kwamba Services ya Bajaji ni miongoni mwa Services zinazotumia dakika kadhaa tu kumaliza.

3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisahara tofauti
Hapa ndio nimekuona kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya na unaishi kwa makusudi. Bajaji, bodaboda zote zinarejesha pesa yake kwa asilimia 100.

Kuna mdada mmoja anazo Bodaboda 26, na alianza na mbili, na ndio ile miaka ya mwanzo zinaanza.
Lei hii akienda bank kuweka pesa ni heshima.Tena Mdada mdogo tu. Na alipohojiwa kwenye Tv anakuambia changamoto za kawaida sana kama ukijitoa.

Mzalendo. Wewe timiza ndoto zako, nunua mpe Driver upate hesabu yako na ndani ya mwaka pesa imerudi.
Na Bajaji unatumia zaidi ya mwaka mmoja. Kuchoka kwa chombo cha moto ni matunzo yako tu.

Inapotokea kasoro basi irekebishe mapema kabla haijawa kubwa.Muhim ni kutafuta sehem ambayo utamuambia Driver wako atakuwa akipeleka kwa ajili ya Service. Maana hivi ni kama Pikipiki tu,s asa baadhi ya Drivers hujifanya kufanya services kivyao na Oil hizi za mitaani zilizokuwa na kiwango duni sana.

Kila la Kheir and Stay blessed
UZOEFU WANGU

Mimi nafanya hiyo biashara, na mpk sasa ninazo mbili! inalipa sana hapa town ila kwa njia ya mkataba otherwise itakutesa kama huyo mkuu hapo aliyekua anachukua 15 kwa siku!

Ni hivi: mkataba huwa ni miez kumi na 8 (mwaka na nusu) na kwa siku kipande ni elfu 20 na anakupa kwa wik = laki na 40/- kwa mwez ( x 4 = 560,000/-) kwa mwaka na nusu itakua 560,000 x 18 = tshs 10080000/-

Kuhusu matengenezo huduma zote za kawaida anafanya dereva icpokua huduma kubwa kubwa tu ndo utahusika tena kwa kushea gharama na dereva!

Kuhusu ipi ni bora' kwa mkataba bora piagio siyo TVS

Kwann piagio? Kwasababu inanafas kubwa ya abiria kukaa na mizigo pia ukilinganisha na TVS
Tvs ni nzuri kwa mtu anaefanya biashara bila mkataba kwasababu ikimrudishia hela ni rahis kuiuza (inauzika kirahis/inasoko kubwa) na hii ni kwasababu ziliwah kuingia hapa bongo kabla ya piagio)

Uimara wa chombo uko mikonon mwa dereva! ila piagio sina shaka nazo kwenye uimara!

Nin faida ya kuingia mkataba?

1/ Bajaj haihitaj uangaliz mkubwa kwasabab dereva anajua baada ya miez kumi na 8 bajaj ni yake! ( hawez kuitumia roughLy)

2/ Ni win-win project yaan wote wanufaika dereva na boss pia hivyo bas haitakua kaz ngumu kumpata dereva

3/ Huduma za mara kwa mara hazitakuepo mana anakua anaiendesha kwa uangalifu mfano, hata *dei waka huwa hawatoi hawa madereva wa mikataba na kama ikitokea service anamaliza mwenyewe unLess iwe kubwa na pia mtashea gharama!

4/ Payback period ni kubwa kwa muda mfupi..

ANGALIZO>> usisahau kukatia BIMA bajaj yako tena BIMA kubwa! ili uondokane na stress inapokua barabarani!
NI BIASHARA YENYE FAIDA

Nakushauri ufanye hiyo biashara kwa kuwa ni profitable. Mimi pia ninafanya hiyo biashara na mpaka sasa ninazo mbili. Three-wheeler nzuri ni TVS King maana inadumu kwa muda mrefu na pia ni rahisi kupata spare zake na bei nafuu ukilinganisha na aina nyingine za Three-wheelers.

Mimi 'Bajaj' zangu kwa siku hesabu ni sh 20,000 each so kwa mwezi inanipa sh 600,000 kwa kila moja (hapo excluding services). Bajaj kwa mwezi zinafanya service mara mbili ili ziendelee kuwa na hali nzuri na esttimation ya service ni sh 22,000 so kwa mwezi gharama inakuwa sh 44,000-45,000.

Hakikisha unakuwa na kijana anayeeleweka maana huyu ndio a 'secret' ya mafanikio yako, chukua kijana mwenye 'commitment' hapo hutapata usumbufu sana. Pia hakikisha Bajaj yako ina vibali vyote ili usiwe unapoteza hesabu yako kwa kudanganya kuwa amekamatwa na traffic imebidi ampe hesabu yako, vibali ni SUMATRA, Insurance na Road licence (Road licence unalipia once tu maana serikali imetoa msamaha kwa Bajaj na pikipiki kwenye hili). I hope nimeweza kukusaidia kwa kiasi chake.

P.S Sehemu nyingine, mfano Africana njia ya chini hesabu ni sh 25,000 kwa siku so inategemea na location pia mkuu.
Nkondo 2
AINA ZA BAJAJI, CHANGAMOTO NA USHAURI

1. Naomba kufahamu bei halisi ya kununua bajaji mpya.

TVS-7.3M na RE BAJAJ-7M
2. Tahadhar muhimu za kuchukua/kuzngatia pindi naponunua bajaji mpya.
- Nunua mpya usichukue second hand
- Umesema unatokea Mwanza, kwa jiografia ya huo mji chukua RE-BAJAJ hizi zina nguvu lakini sio fuel efficiency, spare parts zake ni ghali compared to TVS KING

3. Naomba kufahamu taratibu muhimu za kufuata kabla ya kuanza biashara hii.
- Tafuta dereva mzuri, huyu kumpata unaweza fanya uchunguzi kupitia watu wanaoendesha naye
- Ikatie comprehensive insuarance tumia bima ya CRDB ni 6% ya bei ya chombo
- Itengee akaunti special hela itakapokuwa inaingia

4. Changamoto za biashara hii
- Uaminifu wa madereva(hesabu)
- Ajali barabarani
- Service on time kufanya
- Matumizi ya spare original

6. Ushaur kuhusu mengineyo
- Hakikisha unachukua hela kwa siku, usikubali uchukue hela kwa week mtasumbuana na dereva
- Siku ya service hakikisha unakuwepo wewe/muwakilishi kujiridhisha vifaa vinavyowekwa ni Genuine
- Kuna makampuni yana jishughulisha na kufanya service, usipende sana mafundi wa mitaani kuibiwa njenje
- mzuie/muonye dereva kukitoa chombo kukoroga/day waka
- Ukinunua chombo waweza kaa nacho miezi hata 6-8 then kitoe kwa dereva kama mkataba ili kisikusumbue saana
wick
FANYA YAFUATAYO UTAIPENDA BIASHARA YA BAJAJI

Bei halisi ya bajaji ni 7mil
Insuarence, Sumatra na mambo mengine mpaka bajaji inaingia barabarani laki 4.

Sasa cha kufanya ni kutafuta dereva mzuri na mwenye mke na mtoto/ watoto ambaye anajua umuhimu wa kazi na familia. Huu ni uangalizo tu, unaweza kupata dereva bachelor na akawa mchapaka kazi

Total hapo juu ni 7.4 mil
Ingia na huyo dereva mkataba unaosema akifikisha mara 2 ya hiyo fedha ambayo ni 14.8 mil, bajaji inakuwa ya kwake. Hutahusika na kitu chochote, awe anakuletea hesabu ya 150,000 kwa wiki

Less na 2 yrs atakuwa keshakuletea hiyo 14.8mil, tena madereva wengine watakuwa wanakuletea zaidi ya hiyo hesabu ili amalize deni mapema.

Ukishafikisha 7.4mil unaenda kununua bajaji nyingine au huyo dereva akimaliza mkataba wake unamnunulia nyingine mkataba unaanza upya, ile bajaji ya zamani anampa dereva wa kwake anakuwa anamletea hesabu dereva wako au option 2 anaiuza anaanza kazi na hiyo mpya.

Dereva akishajua mwisho wa siku chombo kinakuja kuwa chake anakitunza.

Hizi ndio tunavyofanya Dar.
 
Nawasalimu wakuu woote wana JF.Mwenzenu nimepata kamshiko km 8m sasa ninataka ninunue bajaj najua hapa mjini dar zinatumika sana,naomba kwa yeyote mwenye uzoefu anisaidie ni shs ngapi dereva anatakiwa alete kwa siku?au week? nashukuru naelewa humu ndani wapo wengi wanaofanya hii biashara!!je does it worth?asanteni sana nasubiri majibu hapo chini!!

Sijui unataka kuifanyia wapi biashara yako, lakini kwa kule kwetu Tegeta unalamba 15,000 mpaka 20,000 kwa siku. Ni kabiashara kazuri ukimpata dereva mzuri. Maintenance cost yake iko chini sana. Ila ucheze mbali na kina Chenge.
 
Mtu wangu angalia huyo dereva utakae mwajiri maana wengi wao wanaua Bajaj kwa makusudi kabisa. Kwa taarifa yako wanachanganya lita moja ya petroli na lita moja ya diesel halafu wanatumia mchanganyiko huo kuendesha Bajaj. Muda sio mrefu Bajaj inaanza kufoka moshi.

At the end of the day, dereva anatengeza fedha yake thru many trips per liter of mixed diesel & petrol per day at your expense of high cost of maintenance of the Bajaj. Please Watch out if you want to invest in this project.
 
Okay nafurahi sana wadau kwa mawazo yenu, na nitazingatia hayo yote mlioniambia, especially la dereva ni muhimu sana nalo. Nitampeleka course ya integrity.
 
Okay nafurahi sana wadau kwa mawazo yenu,na nitazingatia hayo yote mlioniambia, especially la dereva ni muhimu sana nalo. Nitampeleka course ya integrity

Mkuu tafadhari watafutie nafasi na viongozi wetu wa serikali, Watanzania tupo tayari kuwalipia ada.
 
Okay nafurahi sana wadau kwa mawazo yenu,na nitazingatia hayo yote mlioniambia,especially la dereva ni muhimu sana nalo.nitampeleka course ya integrity

Where is the location of the school of integrity for these kind of drivers? Majority are either illitrate or Primary school leavers and bhang smokers having graduated from bicycle ridding. They do not pocess driving licences and do not know traffic rules and regulations. Borrow a leaf from Chenge's accident in which the Bajaj driver disappeared in the thin air todate.
 
Tafuta mradi mwingine uwekeze pesa zako. Biashara ya Bajaji ugonjwa wa moyo kweli. Madereva wezi, na Bajaji zenyewe ni target kwa waporaji. Usije shangaa ukamuokota dereva wako msitu wa Pande kaning'inizwa huko.
 
Tafuta mradi mwingine uwekeze pesa zako. Biashara ya Bajaji ugonjwa wa moyo kweli. Madereva wezi, na Bajaji zenyewe ni target kwa waporaji. Usije shangaa ukamuokota dereva wako msitu wa Pande kaning'inizwa huko.

Hata Bajaj? Nilijua pikipiki pekee, mi nataka bajaj tri-circle mkuu, sasa kama hivyo tena mimi m8 ntafanyia nini?kama sio kuanza kupanga machungwa barabarani? Haitoshi hata kodi ya mwaka kariakoo pamoja na mzigo, u see bora kama vipi nivifaidi vi 15000-20000 per day kama vipi ndo iwe ilivyo, 8m ndogo sana kuumiza kichwa kuinvest, otherwise iwe ya kupombeka?
 
hata bajaj?nilijua pikipiki pekee,mi nataka bajaj tri-circle mkuu, sasa kama hivyo tena mimi m8 ntafanyia nini?kama sio kuanza kupanga machungwa barabarani? haitoshi hata kodi ya mwaka kariakoo pamoja na mzigo, u see bora kama vipi nivifaidi vi 15000-20000 per day kama vipi ndo iwe ilivyo,8m ndogo sana kuumiza kichwa kuinvest, otherwise iwe ya kupombeka?

Ulianza vizuri sana na hii mada ila sasa busara inaanza kukutoka.Please maintain Business focus yako, usikate tamaa it's too early to think of kupombeka at this juncture. Try do some thing with that 8m,sio ndogo kivile my brother.
 
Ulianza vizuri sana na hii mada ila sasa busara inaanza kukutoka.Please maintain Business focus yako, usikate tamaa it's too early to think of kupombeka at this juncture. Try do some thing with that 8m,sio ndogo kivile my brother.

Nimekupata mheshimiwa, then no turning back.
 
I think Bajaj is a good idea.U invest capital ndogo na pia unapata faida bila cost kubwa. Cha msingi ni kupata mwendeshaji mzuri wa mradi wako huu na uweke malengo yako.Ukipata 15000 per day times 365= 5,475,000 WHICH ni gharama ya manunuzi ya bajaj hiyo baada ya hapo unaanza kula faida.

Suala la wizi ningekushauri insurance uweke COMPREHENSIVE ili ku-secure ur capital.

Good luck bro
 
Kaka hongera kwa uamuzi wa busara!biashara yoyote ile ni lazima kuwe na risk!cha muhimu ni wewe mwenyewe kuwa risk taker,si unajua tena high risk high return?

Kuhusu business ya bajaj ni very simple kuiendesha kwake!
Kuna kitu wanaita perfomance contract!unaandikiana na driver wa hiyo bajaj!makubaliano ni kuwa kila siku shs 20,000 kwa muda wa mwaka mmoja bajaj inakua ni mali yake!

Akipata ajali ya kizembe imekula kwake unachukua bajaj yako!wala hutakaa kichwa kikuume.

Mahesabu yake ni hivi kwa mwezi ni 20,000x30=600,000
Kwa mwaka ni 600,000x12=7,200,000

Bajaj umenunua milion 4 so unakunja faida ya milion 3.2 kiulainiiiiiii

Ukiwa na zo kama 2 hv unakula kuku tu.
 
Last edited:
Huo ni mtaji tosha tukachukue mbao malawi na mie nitaweka hapo another 8 m then tunashusha mbao mombasa kuna watu wana export pale infact baada ya week 3 tunakuwa tume make profit ya 2.8 mil baada ya kutoa cost zote, believe me. Kwahiyo, tukipiga pasu kila mtu ana pata 1.4m kama we ni mtu wa kupombeka toa tena hiyo 4 utabaki na 1 m piga ua.hutapata chini ya hapo. Welcome on board. Kama una uchungu wa ku make bakaaa.
 
hata bajaj?nilijua pikipiki pekee,mi nataka bajaj tri-circle mkuu, sasa kama hivyo tena mimi m8 ntafanyia nini?kama sio kuanza kupanga machungwa barabarani? haitoshi hata kodi ya mwaka kariakoo pamoja na mzigo, u see bora kama vipi nivifaidi vi 15000-20000 per day kama vipi ndo iwe ilivyo,8m ndogo sana kuumiza kichwa kuinvest, otherwise iwe ya kupombeka?

Jaribu kulima mkuu.

Mahindi heka moja kulima mpaka kuvuna ikizidi sana 300,000. Hujashika jembe hapo mkuu, ni vibarua na mashine. Ukivuna hata mahindi mabichi 5,000 tu (yanaweza kufika hata 10,000) na ukayauza kwa sh 100 kila moja. Unatengeneza 500,000. Faida 200,000.

Ukitumia 6M yako waweza kulima heka 20. Faida yako 4,000,000 . Na hii umelima mara moja tu kwa mwaka (miezi mitatu).

Kwa bajaji ikikaa barabarani siku 5 kwa wiki na bila matatizo yoyote yanoyihitaji spare, na ukichukulia mafuta yote yanawekwa na dreva, utatengenza 4,000,000 kwa mwaka mzima.
 
Oyaaa! nipe mm hiyo 8m, nitakulipa 80,000 kwa wiki kwa mwaka mmoja, then nakurudishia 8m yako.
 
Gkundi are you serious na proposal yako ya 80k per week? Nini security ili ukiingia mitini mtu ajue atapata vipi 8m yake!
 
Bei ya bajaj ni Tshs 4.5m mpaka Tshs. 5m na madereva hupelekaTshs. 15,000/= kwa siku. Kwa hesabu za haraka haraka unaweza kuona kama mradi mzuri sana lakini ukitulia na kuongea na anaefanya biashara hiyo atakwambia si biashara ya kukimbilia.

Mapungufu makubwa ya bajaj ni quality ya bajaj na short economic life. Bajaj hazina uimara wa kutosha na baada ya muda mfupi zinaanza kusumbua. Madereva ni tatizo jingine, wanaibebesha bajaj kama pick up.
 
Jaribu kulima mkuu.

Mahindi heka moja kulima mpaka kuvuna ikizidi sana 300,000. Hujashika jembe hapo mkuu, ni vibarua na mashine. Ukivuna hata mahindi mabichi 5,000 tu (yanaweza kufika hata 10,000) na ukayauza kwa sh 100 kila moja. Unatengeneza 500,000. Faida 200,000.

Ukitumia 6M yako waweza kulima heka 20. Faida yako 4,000,000 . Na hii umelima mara moja tu kwa mwaka (miezi mitatu).

Kwa bajaji ikikaa barabarani siku 5 kwa wiki na bila matatizo yoyote yanoyihitaji spare, na ukichukulia mafuta yote yanawekwa na dreva, utatengenza 4,000,000 kwa mwaka mzima.

Mkuu vipi mvua au proper irrigation? Kama irrigation sure this is a deal,na well bajaj sina uhakika kuwa ina guarantee ya mda gani!kama ni chini ya 3yrs nayo si deal kivile,well thank u much kwa michango yenu, nadhani tz tunaweza ila mawazo ya kuchangiana mtu unakosa unajikuta wajitosa kichwa kichwa at the end unaua mtaji. Very bad!!
 
Kuwa na moyo, jitahidi kupata mtu unayemuamini kama dereva na pia usicheze mbali!!kubali kitu kimoja kwamba piga ua suka lazima atakupiga bao kiasi fulani ila aghalau iwe ni kiwango cha chini!! pia, si unajua wanasema "u have to take risk in ur life, the bigger the risk, the higher the return" , usicheze mbali!
 
Usirudi nyuma ndugu yangu songa mbele na wazo lako la biashara ya bajaj, huo ndio ujasiriamali wenyewe kwani kila biashara ina risks zake.
 
Back
Top Bottom