Biashara Thailand

mama dunia

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
420
84
Hope wazima, mi naomba msaada jamani, ninapenda sana kuanza duka la nguo mkoani,nimefanya marketing survey nimeona mkoani patalipa kuliko hapa dar, sasa ninataka kupata usaidizi maana nataka niwe naenda kuleta mzigo mie mwenyewe kutoka huko Thailand, maana napenda sana kuchagua chagua na napenda ubora sana maana najua itaniletea wateja sana sasa shida yangu ni kama humu kuna mtu aliyewahi kufanya au anafanya biashara ya kununulia mzigo from thailand, kama italipa, bei zao, na mambo ya charges za hapa bongo, kama mzigo vizuri uje kwa meli au air cargo nk, please please naomba sana ushauri wenu na experiences pia..
 
mi ngoja nikupe experience kidogo:
Uwe macho na watu hasa waafrica utakaoenda nao au utakaokutana nao huko, watu kibao wameishia kuliza pesa zao

Pili kama wewe ni mwanamke uwe macho sana wanaume wanao-take advantage ya ugeni wako ktk business, in a foreign country plus cheap accommodation, si unajua wafanyabiashara mnavyopenda kusave pesa
 
Hope wazima, mi naomba msaada jamani, ninapenda sana kuanza duka la nguo mkoani,nimefanya marketing survey nimeona mkoani patalipa kuliko hapa dar, sasa ninataka kupata usaidizi maana nataka niwe naenda kuleta mzigo mie mwenyewe kutoka huko Thailand, maana napenda sana kuchagua chagua na napenda ubora sana maana najua itaniletea wateja sana sasa shida yangu ni kama humu kuna mtu aliyewahi kufanya au anafanya biashara ya kununulia mzigo from thailand, kama italipa, bei zao, na mambo ya charges za hapa bongo, kama mzigo vizuri uje kwa meli au air cargo nk, please please naomba sana ushauri wenu na experiences pia..

mawazo mazuri sana ya kufanya biashara ya nguo kutoka thailand, Nimeingia thai mara 4 kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho ni 2011.. thai wapo vizuri sana kwenye textile industries, bei ya bidhaa ipo chini sana, kutokana na labor costs kwa nchi za US & euro kuwa kubwa, hali hii ilipelekea bei ya bidhaa zao kuuzwa kwa bei ya juu sana na hivyo watu wa kipato cha chini kutoka nchi za asia, africa & south america walishindwa kumudu bei, alternative waliyoitumia ni kufungua branches kwenye nchi zenye cheap labor na mazingira mazuri ambapo thai na indonesia vitu hivyo vilipatikana. Kwahiyo product ya nike, gucci, fila, will smith ingetengenezwa US au euro ingeuzwa kwa $80 lakini thai utapata kwa same material & quality chini ya $50.

faida nyingine ya thai wapo vizuri sana kwa kazi za mikono i.e kuna wajasiriamali wanao design na kutengeneza nguo/viatu/mikufu/bangili vizuri sana kwa njia za asili na ukivivaa mtaani mpk ofisini utakuwa unique.. bei zao hazizidi $30.
tatizo la watu wa thai si waaminifu ukimuachia hela tofauti na china.. ni watu wa starehe sana
 
Back
Top Bottom