Biashara na usimamizi wake

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
bot_tabimg.gif

1.NAMNA YA KUKUZA NA KUENDELEZA BIASHARA Send to a friend Wednesday, 11 May 2011 21:04 0diggsdigg

Na Staphord Kwanama
BIASHARA yoyote si majaribio, hakikisha umeibuni vizuri ili iwe endelevu na yenye kukuletea faida.

Kutambua vizuri soko la bidhaa au huduma yako
Unaweza kujua nani ni wateja wako (soko) kwa kuangalia;
Uhitaji - angalia uhitaji walionao watu katika eneo fulani kisha tafuta biashara ambayo itaweza kuondoa au kupunguza uhitaji huo. Mfano, Watu waliona huduma ya Babu wa loliondo inachukua muda mrefu hali watu wanahitaji chakula na kulala, hivyo biashara ya chakula na malazi ikaanzishwa.

Mapenzi ya kuwa na kitu Fulani – Watu hutokea wakapenda kitu fulani kwa sababu mbalimbali. Mfano kutokana na foleni za Dar es salaam watu wengi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwa mafuta ya gari. Hivyo watu wengi wanapenda kutumia magari madogo kwa kuwa yanatumia mafuta kidogo, na biashara ya magari hayo ina fursa ya kuongezeka na kukua zaidi.

Uwezo wa kununua – hakikisha watu unaotaka kuwauzia wana uwezo wa kununua kwa maana ya kwamba utarudisha gharama zako na faida.Mapungufu ya bidhaa zingine – Hakikisha unauza bidhaa zenye ubora zaidi kuliko washindani wako ili ujijengee uhalali kwenye soko na wateja watakuamini na utawapata wengi.

Jinsi ya kudumu na wateja
Uza kile anakithamini mteja na si chochote kilichopo - hakikisha unauza bidhaa waipendayo wateja na si chochote tu. Jitahidi kuwa na suppliers kutoka sehemu mbalimbali. Hii itasaidia kama leo hana bidhaa fulani basi unaweza kuipata kwa mwingine na si kuwaletea wateja chochote kwa kisingizio kuwa ndio kilichopo tu.

Mbinu zingine ni pamoja na kuchagua kundi la wateja watakaonunua kwa faida na uwe karibu nao, jitahidi kufanya utafiti wa soko, kuwa msikivu kwa maoni ya wateja wako na siku zote weka hazina ya uaminifu.

Jinsi ya kujijengea jina kibiashara
Biashara yako itakuwa endelevu iwapo jina lake ni imara. Zifuatazo ni kanuni za kujijengea jina kibiashara; kutoa huduma bora na si bora huduma, kutoa ahadi timilifu na za kweli kwa wateja, chagua aina fulani tu ya wateja ambao unajua utawahudumia vema kwa kuwa si rahisi kuhudumia kila mtu vema, toa huduma zako kwa ufanisi mkubwa, acha na blah…. blah…, fanya biashara ambayo si rahisi mtu mwingine kuiga kirahisi, ambatana na mteja na achana na wasio walengwa, jitangaze.

Njia za kutangaza biashara kwa gharama nafuu
Kutangaza biashara ni muhimu sana vinginezo itakuozea, kutangaza biashara ni gharama sana ila kuna baadhi ya njia za kutangaza kwa gharama nafuu nazo ni kama ifuatavyo;
Kutoa motisha kwa wateja na kuwabembeleza wakuletee wateja wapya, weka matangazo kwenye nguzo, majumba au mbao ambapo watu wengine wameweka, onyesha kwa vitendo jinsi ya kutumia bidhaa unayouza, zungumza kuhusu bidhaa zako katika mkusanyiko wa watu,fadhili timu katika eneo la karibu na biashara, fadhili mashindano mbalimbali, andika makala katika magazeti juu ya biashara yako.

Mbinu nyingine ni kama utumiaji wa simu kwa kuwaandikia ujumbe mfupi wateja wako kuhusu bidhaa mpya,tumia barua pepe (e-mail) tovuti, blogu, facebook,twita.
Mchanganuo wa biashara
Ili biashara iwe endelevu ni lazima iwe na dira, mipango na mikakati inayotekelezeka ambayo huwekwa katika mchangunuo wa biashara. Mchanganuo huu utakuonesha namna biashara yako ilipotoka, ilipo na inapokwenda kwa kipindi ulichojipangia mfano miaka 3 hadi 5. Aidha, mchanganuo utakuwezesha kupanga mikakati na mbinu za kuendeleza biashara. Na hatimaye itakuwezesha kuongeza mtaji kwa kupata mkopo kutoka benki au taasisi ya fedha.

Kuandaa mchanganuo unaotekelezeka ni vyema kuwaona watalaamu wanaotoa huduma hizo mathalani unaweza kuwapata kwenye mtandano mfano google (wataalam wa business plan Tanzania) na vitabu mfano National Business Directory.

Mbinu nyingine zinazoweza kukusaidia kukuza biashara yako ni pamoja na;
-Hakikisha unafanya ukaguzi wa mahesabu yako walau mara moja kila mwaka (external audit)
-Hakikisha unakuwa na mtandao wa watalaam mbalimbali mfano, mambo ya biashara, wanasheria, watalaam wa kodi, wahasibu,bima na wengine wengi kulingana na aina ya biashara yako
-Daima timiza matakwa ya kisheria, mfano, kulipa kodi kwa wakati, kama unawafanyakazi peleka michango yao ya penseni kwa wakati na kuhakikisha vibali na leseni ya biashara iko ndani ya muda wake.

-Jenga utamaduni wa kujifunza mambo mapya yahusuyo biashara yako kwa kuhudhuria kozi fupi, mikutano, semina, n.k.
-jitahidi kujifunza kompyuta, namna ya kutumia huduma kwenye simu yako ya mkononi. - Jitahidi kuhudhuria maonesha mbalimbali ya biashara.

-Pata taarifa mbalimbali, “taarifa ni nguvu/mamlaka” (information is power). Taarifa zitakuwezesha kujua hali halisi ya soko na mambo mengi yanayokuzunguka. Na pia utakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi sahihi.
-Wakati wote kopa kwa malengo maalum, na hakikisha mkopo wote umekwenda kwenye shughuli uliokusudia na si kuhamisha matumizi.
 
Back
Top Bottom