Biashara chuma chakavu: Hujuma zatawala; Mitambo Kiltex, Mutex, Morogoro Textile yauzwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mwandishi Wetu - Raia Mwema




dewji219.jpg



Gulam Dewji

-Raia wa Lebanon wakamatwa bila vibali Keko Dar
-Yabainika wahusika si raia kutoka Palestina
-Mohamed Enterprises wadaiwa ‘kulangua' vyuma
-Mitambo Kiltex, Mutex, Morogoro Textile yauzwa


HALI imezidi kuwa tete katika biashara ya chuma chakavu nchini inayotajwa kuendeshwa katika mfumo wa ukwepaji kodi, huku Kampuni ya Mohamed Enterprises iliyouziwa viwanda vya nguo vya Mutex, Morogoro Textile, Kiltex Arusha na mashamba ya mkonge na chai ikihusishwa.


Kwa upande mwingine, msako wa kushitukiza umefanywa na Idara ya Uhamiaji nchini baada ya gazeti hili kuripoti uhusika wa baadhi ya raia wa kigeni katika biashara hiyo na kuwakamata baadhi, wakiwamo raia sita kutoka Lebanon na wengine kutoka Ufilipino, ikidhihirika kuwa miongoni mwao hakuna raia wa Palestina anayejihusisha na biashara hiyo.

Hata hivyo, wakati madai hayo yakifichuliwa, kuhusu kampuni ya Mohamed Enterprises, uongozi wa kampuni hiyo, kupitia kwa Gulam Dewji umekana kushiriki biashara hiyo na kueleza kuwa viwanda ilivyonunua kutoka serikalini vinaendelea na uzalishaji kwa mafanikio makubwa.


Lakini wakati Gulam akikanusha madai hayo, baadhi ya nyaraka zinaonyesha kuwa chuma chakavu kiliuzwa kutoka kiwanda cha Musoma Textile Mills Tanzania Ltd, yenye sanduku la posta 675 Musoma. Mauzo hayo yanatajwa kufanyika Aprili 24, mwaka 2010, kwa Sh 248,359,000.


Mauzo hayo ya takriban Sh milioni 249 yanatajwa kufanyika kwa njia ya kukwepa kodi na taarifa za tukio hilo linatajwa kuripotiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kitengo cha Upelelezi Zonal II, na kwa viongozi wengine wa TRA.


Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Kampuni ya Mohamed Enterprises wakati mwingine imekuwa ikiendesha biashara hiyo kupitia ‘pazia' la kampuni nyingine. Kampuni hizo zinazotajwa kutumika ni pamoja na One Product and Bottler Ltd, ya Dar es Salaam na 21 Century Textile Ltd.


Katika mazungumzo yake na Raia Mwema ofisini kwake Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa kampuni yake, Gulam Dewji, alikanusha akisema shughuli za uwekezaji katika viwanda walivyouziwa na Serikali inakwenda vizuri.


"Sisi hatufanyi hiyo biashara na wala hatuuzi mitambo, kama ni kweli tunauza mitambo ya viwanda tulivyonunua kwa nini uzalishaji katika viwanda vyetu vya nguo kwa mfano Musoma unakwenda vizuri? Ni madai ya uongo," alieleza Gulam.


Katika hatua nyingine, habari iliyoandikwa na gazeti hili wiki iliyopita kuhusu ushiriki wa raia wa kigeni katika biashara ya chuma chakavu bila leseni, ilisababisha maofisa wa Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam, kufanya msako wa ghafla katika eneo la Keko, kunakofanyika uuzaji na ununuzi wa chuma hiyo.


Taarifa ambazo zimethibitishwa na Idara ya Uhamiaji zinaeleza kuwa raia kadhaa wa kigeni wakiwamo wa Lebanon na Ufilipino walikamatwa, kwa kukutwa na makosa mbalimbali, ambayo ni pamoja na kutokuwa na vibali vya kufanyia kazi.


Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Khamis Abdullah, amemweleza mwandishi wa gazeti hili kuwa wahusika waliokamatwa wametozwa faini ya dola za Marekani 600 kila mmoja (takriban Sh milioni moja) na kwamba ni raia wa Lebanon pamoja na Ufilipino.


"Ni kweli tumebaini raia wa kigeni kushiriki katika biashara hii. Tumebaini wapo ambao hawana vibali vya kazi lakini wanafanya shughuli hiyo. Hayo ni makosa na adhabu yao tumewatoza faini dola 600 kila mmoja na hapo Serikali inapata mapato," anasema ofisa huyo na kuongeza:


"Baada ya kutozwa faini sasa wanapaswa kuzingatia taratibu zote ili kupata vibali na kama wakishindwa basi ndipo tutawafukuza."


Katika habari iliyoandikwa na gazeti hili wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, alikiri hali ya kutofuatwa kwa taratibu zote za msingi katika biashara ya chuma chakavu.


Kutokana na kuwapo kwa kasoro hiyo, Nyalandu alisema suluhisho pekee na muhimu kwa Serikali ni kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Kudhibiti biashara ya chuma chakavu.


Katika hali ya sasa ya kutokuwapo kwa sheria mahsusi, biashara ya chuma chakavu imekuwa ikiendeshwa kwa kuzingatia masharti maalumu yanayotokana na sheria nyingine tofauti.


Masharti ambayo yamewekwa na Serikali lakini hata hivyo yanakiukwa na wafanyabiashara wengi zikiwamo kampuni kubwa nchini na baadhi ya raia wa kigeni ni pamoja na kuwa na leseni ya biashara ya kununua na kuuza chuma chakavu.


Leseni hiyo inapaswa kutolewa na mamlaka husika, ambazo ni halmashauri za wilaya ambako ununuzi unafanyika. Sharti hili halizingatiwi.


Masharti mengine ni biashara hiyo kufanyika kupitia kampuni maalumu iliyosajiliwa rasmi katika Msajili wa Kampuni nchini (Brela), wahusika kuwa na namba ya utambulisho wa biashara (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), malipo ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), leseni ya biashara ya kuuza nje ya nchi chuma chakavu, ambayo hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.


Masharti mengine zaidi ni kupata kibali cha kufanya ukusanyaji wa chuma chakavu kwa kuzingatia Sheria ya Udhibiti wa Mazingira namba 191.








 
Yaani Jasho la Watanzania Dewji ananunua anauza mashine zote kwa manufaa yake binafsi, kwanini hatukuwauzia wazalendo? Akina Mengi walitaka Mawaziri wakati ule akina Juma Ngasongwa na Mwenzake wa Tanga waligoma wakampa Dewji

Wakawanyima wazalendo wa rangi nyeusi ona sasa
 
UMACHINGA - unatokana na RUKSA mmesahau wakati wa Mwinyi kila mtu alikuwa na hela kwa kuuza vipusa vya viwanda na magari za serikali? tumerudi palepale - UMACHINGA! unaibiwa taa za gari nenda kazinunue zilezile Kariakoo au Ilala..
 
inakuwaje mwekezaji mmoja anabinafsishwa viwanda vyote vikubwa vya nguo peke yake???yaani hakuna wawezekaji wengine hususani wazawa waliomba kuendesha viwanda hivyo???kumbuka nyerere aliingilia kati na akalazimisha urafiki kirudishwe kwa wachina kama watz wameshidwa kukiendesha,isingekuwa hivyo labda na hicho kingekuwa cha hiyo kampuni.
 
Back
Top Bottom