NINAANDIKA kwa niaba ya vijana wa Kinondoni Biafra na maeneo karibu ambako tunafadhaishwa na kitendo cha kampuni kubwa kama Zena Mobile phones kuvamia uwanja wetu na kutunyima nafasi ya kufanya mazoezi na kushindana na wenzetu hususan katika futiboli.
Hivi hii ndio corporate responsibility ya watu kama Zain? Na katika eneo hili ambako kuna shule za msingi, sekondari, Chuo kikuu na mahospitali je viongozi wetu wa Kinondoni wanaona ni sawa tu kuruhusu shughuli zenye vurugu, makelele na zisizo na ustaraabu hadi saa nne usiku au zaidi?
Nchi imeshindwa kutupa ajira je, mnataka kutunyima hata kujiendelza wenyedwe ili tujiajiri wenyewe jamani?
Mzee Kikwete wewe mwenzetu Kinondoni hebu tuma watu wako uone unyama tunaofanyiwa sisi vijana wa Kinondoni kiasi wenzetu wasiogopa kifo sasa wanadandia mabasi katika mchezo wa kuteleza na roller-skaters ambao ni wa hatari sana. Wengine tena ndio wameishia kwenye ngono kwa kukosa michezo ya kufanya mzee.
Hivi awamu ya 4 inataka ishindwe pia hata katika jambo hili rahisi la kuhakikisha watoto na vijana wa Kitanazania popte walipo wana viwanja na bustani za kuchezea na kupumzikia? Itakuwa aibu kubwa kiasi gani? Tunashindwa michezo kwa sababu michezo yetu inaanzia matawini ya miti na haianzii kwenye mizizi halisi nako ni viwanja vizuri mitaani na vijijini eti?
Tunashindwa hata na Iraq ambao juzi walikuwa wakibomolewa viwanja na bustani zao na Marekani? Hata Gaza na Afghanistan kusiko na utulivu jamani?
Nilitarajia viongozi wa DINI watajenga retreat na makambi ya kisasa nje ya Jiji na watu kama Zain wataweka hata mazoo karibu na jiji badala ya wao nao kuwa ndio sababu ya kuua mchezo Tanzania na kudumaza maendeleo ya vijana!