Bia hupunguza nguvu za kiume (research facts)

1. Kunywa ongeza nguvu yafaa angalia gongo inaua-k.o.n.y.a.g.i
2.sasa angalia F.ala anaagiza round ingine lakini angalia gharama ewe rafiki-s.a.f.a.r.i l.a.g.e.r
 
Ndio maana siku hizi wanawake wanalalamika sana!
Huo ndio ukweli kama unakunywa bia ujue kabisa huna nguvu za kiume
 
sina lengo la kuwatisha wanywa bia, lakini naamini inabidi tuwe makini.

Bia hutengenezwa kwa nafaka ambazo 'kwa kawaida' hushambuliwa sana na fungus na kupelekea kuwa na fungal toxins (mycotoxins). Inajulikana kuwa sumu hizi huharibiwa na process ya fermentation, wakati wa kutengeneza bia. Hata hivyo tafiti nyingi zimeonyesha uwepo wa viwango vikubwa vya mycotoxins kwenye bia hasa kutokana na bia hizi kutokuandaliwa vizuri. Ambapo katika utafiti mmoja, bia za pilsner na tusker zilionekana kuwa na kiwango kikubwa cha sumu hizi (http://www.scientificsocieties.org/jib/papers/2004/g-2004-0812-235.pdf).

Pamoja na madhara tofauti ya mycotoxins ikiwemo kansa kuharibiwa mfumo wa fahamu, mycotoxin aina ya zearalenone ina athari za kioestrogenic, kwa kusababisha kuzalishwa kwa kiwango kikubwa cha hormone ya oestrogen mwilini. Hii ina madhara kwa jinsia zote, lakini kwa wanaume husababisha kujitokeza kwa tabia za kike (feminization), kama vile sauti kuwa nyororo na kuota matiti (sio lazima iwe kabisa kama mwanamke).

Feminization huambatana na kupungua kwa nguvu za kiume kwa kiasi kikubwa, ambapo mwanaume anakosa au inapungua hamu ya mapenzi kwa wanawake, u.ume kuwa mdogo, na kushindwa kuhimili u.ume kusimama kwa muda mrefu.

Kwa bahati mbaya, sumu hii pia imeonekana kuwepo katika bia nyingi kutokana na maandalizi mabovu na ya haraka ya bia, mfano katika utafiti huu (estimation of the fungal toxins, zearalenone and aflatoxin, contaminating opaque maize beer in zambia - lovelace - 2006 - journal of the science of food and agriculture - wiley online library).

Upo uwezekano mkubwa kuwa bia nyingi za tanzania, hasa zile zinazonywewa sana zikawa na sumu hizi, kutokana na demand kuwa inayofanya viwanda wazalishe haraka haraka, bila kuzingatia viwango.

Usishangae kuwa tatizo la nguvu za 'wababa' linaloendelea kukua kila uchao katika jamii ya watu (hasa wa mijini), linatokana na mabia wanayobwia. Pia siku hizi kuna tabia ya wanaume kunenepanenepa kihasara hasara, kuwa na ngozi nyororo sana, na kuota vijimatiti. Tuwe makini jamini...
ni kweli mzee, nahisi hiyo kitu ninayo!!!!
 
Duh! mimi nikinywa hiyo ndo mwendo mdundo
itafika siku bila kunywa hiyo uume hausimami, kwahiyo kila utakapotaka kufanya lazima uitafute halafu itafika siku hata hiyo haitasaidia, utahamia kingine kikubwa mpaka utakapokuwa usingizimuda wote. nenda hivyo hivyo mkavumkavu utazoea tu
 
acheni ubishoo wandugu, kunywa rozella, ubuyu, na ukwaju juice nzuri sana. hizo laana za pombe balaa!
 
haya ndiyo mambo ya kujadili kabla ya kukimbilia sijuwi dawa fulani inafanya hivi au vile, kwanza tuelewe chanzo cha tatizo halafu dawa baadaye. Kimsingi siyo bia tu bali pombe zote ziwe za kiwandani au za kienyeji halafu soda zote na juisi karibu zote za viwandani, chumvi ya mezani au ya unga tuliyozoea kuitumia, chai ya rangi na kahawa, sigara na madawa yote ya kulevya na orodha inaendelea. Ni suala mtambuka. Kujaribu ni bure. maajabuyamaji2.artisteer.net
 
safi mkuu, maji tu yanatosha, maji ndo kila kitu. asilimia 85 ya ubongo ni maji na asilimia 94 ya damu ni maji. maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Back
Top Bottom