Bia bei juu katikati ya mwaka wa fedha!

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,517
4,987
WANYWAJI wa bia zinazotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) sasa itabidi wajitutumue zaidi kugharimia starehe hiyo kutokana na bei ya bidhaa hizo kuongezeka.

Afisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema kwamba bei hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia leo.

Malulu alisisitiza wauzaji wa rejareja kuuza kwa bei iliyoidhinishwa na TBL ili kuepuka dhuluma na kuwaongezea mzigo wanywaji.

Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba kama bei hiyo mpya itazingatiwa hasa kwa jiji la Dar es Salaam, huenda isiwe ni jambo la ajabu kwa sababu baa nyingi tayari zilianza kutumia bei hiyo tangu Julai, mwaka jana.

TBL walijaribu kupambana na walanguzi hao tangu mwaka jana kwa kusambaza vibao ili vibandikwe kwenye mabaa na kuonyesha bei halisi, lakini baadhi ya mabaa walivitupilia mbali na kuuza kwa bei wanazotaka wao.

Kwa mujibu wa bei hiyo mpya iliyotangazwa na TBL jana, bia za Safari, Kilimanjaro, Tusker, Bingwa na Balimi ambazo zinauzwa kwa ujazo wa mililita 500, sasa bei yake halisi ni Sh1,400 badala ya bei ya zamani ya sh1,300.

Aina ya bia hizo, ambazo zinauzwa katika ujazo wa mililita 330, badala ya Sh1,100 sasa zitauzwa kwa Sh.1,200, isipokuwa Balimi ambayo itakuwa Sh1,000.

Akifafanua zaidi juu ya bei hiyo mpya, Malulu alisema kwa ujumla bei ya bia zote kwa rejareja zimeongezeka kwa Sh100.

Bei mpya ya aina nyingine za bia za TBL pamoja na kiwango cha ujazo wa mililita kwenye mabano ni Ndovu Special Malt (375) Sh1,400, Castle Lager (500) Sh1,500, (330) 1,300, Castle Milk Stout (500) Sh1,600 na (375) Sh1,300.

Guinness (500) Sh1,800, Redd's Premium Cold (330) na (375) Sh1,400 wakati bia zinazopatikana zaidi Kanda ya Kaskazini za Eagle (500) Sh1,100 na (300) Sh700.

Kwa mujibu wa bei hizo mpya, Kinyaji kisicho na pombe cha Guinness Malt (300) kitauzwa kwa Sh900 na (330) Sh1,100.

Malulu alizitaja sababu za kupanda kwa gharama za vinywaji wanavyozalisha kuwa ni kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji.

"Bei zimepanda kutokana na sababu mbalimbali miongoni ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za malighafi, usafirishaji, kupanda kwa bei ya mafuta na kushuka kwa thamani ya shilingi," alisema Malulu.

Alisisitiza kwamba matangazo ya viwango vipya vya bei za jumla na rejareja tayari wameyachapishwa na yanasambazwa kwenye baa na mawakala wao kote nchini.
 
Ofcourse wanasema kuongezeka kwa production cost,lakini wameongeza wakati huu ili kupata faida bada ya bajeti kupitishwa.wanataka pia ku-take advantage ili kutoa kisingizio kwamba kodi imeongezwa otherwise kama kodi itaongezwa (ofcourse lazima iongezwe) basi hawa jamaa wa brweries kama ni wakweli waongeze bei ya hiyo tax iliyoongezwa tu kwani swala la gharama ya uzalishaji wamemalizana nalo kwa sasa
 
Bongo money is toilet paper
1500/= nothing but vapors
Can't even knock some sense into hecklers
Can't even get a decent pair of gators
You re on your own, meet your maker
The president pictured swinging in Jamaica
They killed everything, from Tanganyika Packers
The port, the rail down to the corner bakers
While posing pious like Quakers
The moneytakers, resources rakers
Word to JK, he who forsakes us
And CCM, they won't protect us
And JF, That's where we wake up
Where we do the fine tunings and basic check ups
Reshuffle the cards, then we deck up
Revolution like Copernicus
Let's deal with the matters perpendicular
Murder me a bigwig with this force vehicular
I'm not a Communist but this cross is sicker than a cell that's a sickle
Sicko than Biko, sicko than Ditto in Gitmo
With the Orwellian twang, some are more equal than equal
And I will be back like Terminator in the expected sequel
 
Why siku zote serengeti wao huwa hawapangi bei? wanafuata mgongoni kwa TBL? waache zao bei ya sasa, ujue hawa jamaa wanapata supr profit hawana hasara hata mwaka mmoja, kila mwaka faida inaongezeka, sasa hapa ni ushenzi wao tuu! anyway after all beer sio basic need, hata iwe 1m poa tu
 
Maeneo mengi ya Dar walikuwa wanauza bia kwa shs 1,500/=. wamefanya utafiti na kuona kuwa bora waongeze bei ili wao wachue hiyo faida badala ya kwenda kwa wafanyabiashara. Vilelile wanatakiwa wawape ccm hela ya uchaguzi
 
Kiranga bwanaa...

Nimecheka katika msiba.

Anyway,hata kama nguvu ya soko ndiyo imeamua..ikifika July hawa jama watapandisha tena..kuna turnover wamepanga
 
wacha ipande tu labda walevi watapungua...tsh 1500 maanake ukiwa na tsh 15,000 unapata bia 10,ndio maana watu wanashinda baa...its too cheap!!!
 
Back
Top Bottom