TANZIA Bi. Nasma Hamisi Kidogo Afariki dunia

Oloronyo

Member
Mar 29, 2009
80
9
Yule Nguli wa miziki yenye mahadhi ya Pwani yaani Taarab amefariki dunia,Jijini Dar. Hii ni kwa mujibu wa mtangazaji wa Leo tena wa Clouds FM Dina Marios.

1635154868446.jpeg
4943d1245671215-bi-nasma-hamisi-kidogo-afariki-dunia-1245666321_nasma_kidogo_crop.jpg

Nasma Hamisi 'Kidogo' amefariki dunia juzi usiku katika hospitali ya Temeke jijini Dar.

Kwa habari za uhakika zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu wa marehu zinaeleza kuwa Nasma alilazwa katika hospitali ya Temeke ijumaa mchana akisumbuliwa na malaria pamoja na presha ya kushuka,ugonjwa huo ulikuwa ukimsumbua kwa takriban miaka miwili.

Msiba upo kwa baba yake mdogo,Mzee Kaniki.Kinondoni maeneo ya ya hananasifu karibu na shule ya TAPA,Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa saba mchana kwenye makaburi ya kisutu jijini dar.

Baadhi ya nyimbo alizotamba nazo msanii huyo ni Mwanamke mazingira,Subira Heri,Mpenzi na sanamu la michelin,pia enzi za uhai wake aliimbia vikundi kadhaa kikiwemo Egyptian,Babloom,Tanzania One Theatre na Muungano Cultural Troup.

Nasma ameacha watoto sita, wanne wa kike na wawili wa kiume.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMIN
 
Poleni sana wanandugu na wapenzi wote wa muziki wa taarabu. Tumeondokewa na gwiji kwa hakika. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen.
 
RIP Nasma Hamis Kidogo! Kipi kilichomuua jamani ama aliugua kwa muda mrefu?
 
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amina.Oloronyo, chanzo cha kifo chake kimesababishwa na nini?
 
Dah Poleni wafiwa poleni mashabiki.
Watazika kesho makabuli ya Kiondoni saa kumi.
Msiba upo karibu na shule ya Juhudi Kinondoni.
 
Yule Nguli wa miziki yenye mahadhi ya Pwani yaani Taarab amefariki dunia,Jijini Dar. Hii ni kwa mujibu wa mtangazaji wa Leo tena wa Clouds FM Dina Marios.

Kabla hatujatoa pole na kuonyesha hisia zetu,..JE habari hizi zimethibitishwa?
 
R.I.P Nasma Kidogo!

Tutakukumbuka kweli kwa jinsi ulivyoichachafya TOT ya CCM kipindi kile ...cha sanam la Michellin...na jinsi walivyotumia nguvu kubwa kukuzima na kundi lako la Muungano.
 
Daah! Inauma sana, kapumzike mahali pema peponi dada Nasma. Utakumbukwa kwa mengi hasa ule wimbo wa ' Wadudu wadogo wananyambua nyambua'
 
RIP Bi Nasma Kidogo ulileta changamoto sana kwa Bi.Khadija Kopa kipindi kile cha miaka ya mwisho ya 90... Muungano Cultural Troupe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom