Bi Kidude Enzi Zake alivyokuwa kijana na sasa jinsi alivyo

Nampenda bi kidude mungu amjalie amkumbuke haswa kwenye hii fainal

i love u bi kidude,,,,wacha tujivunie mwanamke msanii mkongwe east africa
 
Wote tunaelekea huko huko kwa bi kidude kama hatutakuwa tumekufa? Ila kwa sasa na lishe na ukimwi huu? Maana magonjwa mengi kwa sasa yanatokana na life style- watu michemsho hatutaki ni vya kupikiliza tu sasa pressure, kisukari, gauti, mara nini na worse kala ka ugonjwa ka mtandao!! Tuko wangapi, tulizana!!
 
Hali yake ya afya haiko vema juzi SAUT YA BUSARA walimkabithi kitia cha Sh 36,000,0000 kama malipo ya kazi alifanya nchi za ughaibuni.
 
kidude.jpg
Hapa akiwa London miaka ileeeee...
 
Uzee

ujana kitu kitamu,tena ni azizi sana
maungoni mwangu humu, nilikuwa nao jana
kwa wingi katika damu, tahamaki leo sina
nasikitika hadumu,rafiki yangu ujana

kichwa kimejaa mvi, kinywani meno hamna
nikienda kama mlevi,miguu nguvu haina
kumbe ujana ni hivi, ukenda hauji tena
nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana



. . . . . . . . . . . . . Shaaban robert
 
Hivi jina Kidude ni a.k.a kutokana na mambo ya sanaa au?
nilimskia akisema kuwa wakati alipozaliwa alikuwa kajitu kadogo sana ka ajabu nadhani alizaliwa premature. sasa watu wakawa wasema njooni muone hiki kidude basi likawa ndilo jina lake la utoto na utani hata leo.
 
nilimskia akisema kuwa wakati alipozaliwa alikuwa kajitu kadogo sana ka ajabu nadhani alizaliwa premature. sasa watu wakawa wasema njooni muone hiki kidude basi likawa ndilo jina lake la utoto na utani hata leo.

got that...
 
Back
Top Bottom