Bi harusi aingizwa mkenge na big boss!!!!!!!! Mji hauna mwenyeji!!!!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Niajeeeee Wadau!!!!!

Hahahahaaaaaaa!!!! LOLEST!!! Leo nimecheka kweli japo ni jambo la kusikitisha! Japo sikuwa na nia ya kuileta hii stori humu, ila wadada wa mujini inabidi muijue mjihadharii!

Bwana, kuna mdada wa mujini shosti wanguu haswaa, yuko mjini kitambooo, tena mutoto wa temeke, anafanya kazi bank moja POSTA hukooo! Yupo dirishani pale basi full mauzo ya sura!

Huyo dada anamchumba (usiringie uzuri ringia bahati) anfanya kazi kwenye shikira la kiserikali japo yupo UGHAIBUNI a.k.a MAMTONI anasoma na inshaalah! anakaribia kurudi, mambo yao sio mabaya, mkaka kakolea sana juu yake, mahari ishatolewa, Mashalaaah! mwezi wa 3 mwakani Dada huyooooo anaolewaaaa! Mashosti tushapewa tenda ya kuwa MAIDS OF HONOUR ndo tunajidunduliza tuchange. Ukubwa dawa!

Sasa bi dada pamoja na kutulia baada ya KUSTAAFU kuwa homa ya jiji historia yake huko nyuma si ya KURIDHISHA.( Ndo maana rafiki yangu atii, sie warabu wa pemba!) Alijirekebisha, akasoma na kuaquire class katika jamii. Wale watu wa uswaa aliembakiza katika circle yake ni mie tu na sababu lazima ubakize back up kidogo jst incase!!!!

Wanasemaga your past always has a way to find you, no matter how far you run, (nikilifikiria hili nawewesekaga usiku!!LOLEST!!) Juzi kati kuna Bosi lilienda pale Bank kama mara 2 au 3 counter ya shosti kuomba tu balance !!!! ( TRUST ME THE ACCOUNT WAS FULLY LOADED Hahahaaaa). Bi dada akampa, mara akaombwa kutolewa lunch, na ZOMBINIZATION ikaanza. The Boss was super NICE!!! lolest!! Anamwaga tu minoti! Bi dada akaniita kikao cha dharura JEMBE lake la BACK IN THE DAYS, agenda kubwa ikiwa, ANATAKA AFANYE 1 LAST JOB YA KULICHUNA HILO BOSI achukue mafao mazito,anaomba mwongozo. Nikamwambia hilo TEGO wewe mtu akuombe balance afu akugande, kuna walakini! Mi nikamwambia wewe LIPOTEZEEE tu, itakuwa kuna umbea umepita, watu wanataka kupeperusha harusi hiyo, utakosa yote!!

Akagoma bana, akaifanya ile KAZI, akaahidiwa HARRIER MPAYAAA na akapewa KADI LA GARI KABISAA lina jina lake, brand new toka SHOWROOM za TOYOTA TANZANIA( Kadi muhimu unaweza potezwa maboya) ila kabla ya kupewa funguo ndo wakutane PARADISE pale posta baada ya kazi kulipana fadhilaaaa! Bi dada kapewa room number kaingia, kaoga kajipumzisha. Mlango ukagongwa akajua payback time, kufungua HAMADIIII !!!FIANCE!!! Kidogo afe! Fiance akamwambia NILITAKA KUDHIBITISHA KWA MACHO YANGU,SASA NIMEONA! KWAHERI!!!! Yule bosi nilimtuma mimi! Huyoooo kaishia, bi dada ndo kuniita tutafute a way out jinsi ya kuweka KIRAKA hapo mambo yakae poa!!!

Ataiweka wapi sura yake!!! Kisa cha kuachwa mji ukikijua??? LOLEST!!!! (Its not a laughing matter) Jamani embu toeni ushauri wa kujenga, makosa yake kesha yajua ila ndo katika kuokoa jahazi aanzie wapi?.

Wanaume kwanini mnapenda kumchunguza BATA sanaaa matokeo ndo hammli kama hivo.
 
Gube gube apewe ushauri?

Mbona wake za wtu wengi magubegube wastaaafu!!! LOLEST!!! Asingechanganya madawa si angekuwa WIFE MATERIAL!! lol!! Au huonagi visa visivyoisha humu MKWE WANGU ANATOKA NJE YA NDOA???? Ndo hivo alikuwa gubegube mstaafu!
 
Mbona wake za wtu wengi magubegube wastaaafu!!! LOLEST!!! Asingechanganya madawa si angekuwa WIFE MATERIAL!! lol!! Au huonagi visa visivyoisha humu MKWE WANGU ANATOKA NJE YA NDOA???? Ndo hivo alikuwa gubegube mstaafu!

Gubegube aliyeko ndani ya ndoa hahalalishi gubegube linalotaka kuingia ndani ya ndoa.......Two wrongs............!?
 
Sasa ashauriwe nini na tayari ameonyesha siyo mwaminifu?Huyo anaonekana ni kicheche tu!
 
kazi ipo wallah! ila mi ningeruka mpaka dakika ya mwisho, hata anipe uthibitisho gani, ningemruka tu! kuna watu wana kazi jamani, na muda wanao, sasa shida yote hiyo ya nini?? ilimradi aje aproove tu kuwa mchumba hacheat, kwani alimkuta bikra?? haya wakaka nyenzo hizo igeni!
 
Watu wote wezi sema kishikwa ndo MKOSEFU MKUBWA!!! we unataka kusema huko ulaya hakupiga MECHI ZA UGENINI?

Ujue tamaa mbaya wewe mtu kuona balance yake unachachawa mi nina uhakika angeambiwa achana na yule bwana ako angemuacha tu
 
Hebu nipe jina la Bank na counter namba ili tumtoe upweke huyo bi dada...nadhani anahitaji faraja ya moyo kwa sasa.
 
Hebu nipe jina la Bank na counter namba ili tumtoe upweke huyo bi dada...nadhani anahitaji faraja ya moyo kwa sasa.

Nafikiri ndio ushauri anaouhitaji kwa muda huu; maana ulim-warn kabla na hakusikia, na kwa jinsi ilivyo sidhani kama mwanaume anaweza kurudisha majembe, so akubali maumivu na aamua au abehave hoping bahati itarudi second time au arudie maisha yake ya zamani.

Mean while msamaria mwema watu8 ameshajitolea kumpunguzia mawazo!
 
Na wewe kama unampenda kweli, kwanini ukubali kupokea ufunguo wa Harrier na unajijua unamchumba na muda sio mrefu unatarajia kufunga ndoa? Tena mtu anaekupa ufunguo hamjafahamiana hata kwa muda mrefu, mbaya zaidi unakubali kwenda guest? Mi naona ni poa tu alivyoachwa hata angeolewa huyo asingekuwa mwaminifu kwa mumewe

Ndoa ni mipango ya mungu bwana
huyo hakuwa mume wake.
Mwanaume anaekupenda kweli si mchezo hawezi chezesha game za kipuuzi hizo
 
mh wadada wa mujiniiiiii!ah aisove kimjini mjini!full uso wa mbuzi maisha yanaendelea!
 
jamani lakini manmshambulia tu huyu dada wa mujini,lakini hapa ni watu wangapi huwa mlipata cha mwishomwisho kabl ya ndoa na ma x wenu!ila dah simpatii picha huyo dada ana hali gani!la msingi ni kusonga mbele tu ameshalikoroga hapa na kuutwanga mbichi au kuuanika kwanza bhaaasi!akilazimisha kuolewa na huyo mwanaume atamtesa sana kihisia since hicho kitu kilipangwa ili aanguke aachwe!kwa hiyo hapo akiforce tu kuingia kwenye hiyo ndoa ameliwa!hataweza kuhoji kosa lolote la huyo mwanaume,atakuwa hajiamini tena!atalazimika kuvumilia kila kitu hata upuuzi usiovumilika,atalazimika kutafuta haiba isiyo yake simply because amekose na akili yake itamtuma kuwa huyo mwanaume yuko perfect 100% na yeye ameolewa kwa huruma!mwambie ajipange upya atazame mbele!aibu ya kutokuolewa hata kama mahari imeshatolewa ni afadhali kuliko kuishi kwenye ndoa yenye masimango,gubu,dharau,na kashfa!ni mara mia kama hilo kosa lingekuwa limetokea tu bila kuwa ni swala la set up!ningesema amwombe msamaha huyo mwanaume ila kwa kweli hapo wala hamna ndoa alimeze tu hilo aendelee kuwa senior spinster!
 
huyo mwanaume muoaji ndo lofa..,.majaribu gani hayo ya kumfanyia mpenzio
 
Back
Top Bottom