Bi Asha: "CCM Ndiyo Kinatuweka Mjini Bara na Visiwani"

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
hii ni ishara ingine kwamba ccm bado ina magamba mengi zaidi ya iliyojigambua.

mimi nafuatiliaga kauli za wana-ccm kwanzia herufi ya kwanza, koma, nukta, vifungua na vifunga semi, alama za viulizo na mshangao, mpaka herufi ya mwisho.

hii niliipata jana Star TV, saa mbili usiku:

kuna kimama kimoja kinaitwa Asha kilisimama kwenye jukwaa na kuanza kuimba taarabu. kwanza kilianza na salamu: "asalamalekooo"; wajomba wakaitika "alekomsalaa". mimi nikajua labda kitasema tena "bwana yesu asifiwe" ili kubalansisha, kama waungwana wengine vile wanafanya, lakini hakikufanya hivyo.

bada ya hapo kikapiga blaa-blaa zake pale jukwaaaaanniiii, na hatimaye kikaja kuchafua hali ya hewa pale kilipotoa kauli yenye utata:

"ccm ndiyo chama kinachotuweka mjini bara na visiwani".

hii kwa mwanaflsafa makini kama mie ni kauli tata sana ambayo kama mimi ningekuwa kiranja wa vijitu vya namna hii, siku hiyohiyo nakivua gamba. ni kauli inayowatusi moja kwa moja watu wa bushi, kule kwetu kijijini.

nimeteki noti.

nitawaambia watu wangu wa kijijini; kwamba wale wanaosema wanajivua magamba, wanafanya hivyo ili chama kiendelee kuwaweka mjini.
 
aina hiyo ndio wengi sana ndani ya ccm wanawapumbaza sana viongozi wao
 
Back
Top Bottom