Beware of this type Conmens..tiGo fuatilieni namba hii jamaa wanawachafua!

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Wadau
Nipo ofisini kwangu namalizia viporo vya wiki nzima mara inapigwa simu ya mkononi ya sales manager akiombwa kuzungumza na boss wake mpigaji akidai yeye ni Operations Manager wa tiGo.Nilipokea jamaa akajitambulisha na kuniambia request ya namba yangu ipo tayari na kuna salesman amemtuma aniletee(alarm ikagonga) hiyo namba digits zake zinafanana na namba ya sales manager wangu ambayo ni Vodacom.kilichonitia mashaka ni pia kuwa namba kama hiyohiyo tayari tunaimiliki katika mitandao ya tiGo,Airtel, Zantel na hata Sasatel

Nikapata hisia kuwa kwa kuwa namba ya vodacom ipo kwenye gari ya mauzo basi wamefikiri sina namba hiyo kwa mtandao mwingine,pia nikawa na mashaka kwani namba aliyopiga haipo katika mfumo wa tiGo staff kwani mara nyingi huanza na 123XXX
Jamaa akasema wameishaiload artime ya 45,000 hivyo jamaa ataipitisha na atakuja na gari la tiGO,nikamkubalia nione mwisho(kawaida ukipewa prepaid simcard inabidi uweke airtym mwenyewe)

In few minutes akaja jamaa akijitambulisha jina la Raymond Sanga lakini lafudhi kama ya kihaya na bahasha ya Khaki yenye hiyo Sim Card imeandikwa juu kuwa activation after 3 hrs,( Nikajua wanaprotect nisitest coz it wont work kwa muda huu)nikatoka nje kuzuga kama namuita mfanyakazi kumbe nacheki gari aliyojia nayo nikakuta hamna gari nilipomuuliza akajibu ameiacha jirani na huku akining'iniza ign switch mkononi hiyo ikanifanya niamini ni utapeli.

Nikaagiza aandikiwe Petty Cash lakini aproduce kitambulisho chake for records...hapo akaanza kugwaya nikamwambia nenda tu ukipata kitambulisho njoo( sikutaka kumuitia polisi as i was busy na kazi zangu na nilijua itahitaji kuandika statement and spoil my weekend tym) akatoka na nyuma nikamtuma kijana amfuatilie akakuta anaongea na simu then akakwea bajaj..hahaha!

Pia nilimuuliza mtu niliyekuwa namfahamu kama oprts manager ambaye kwa sasa hayupo tigo lakini jamaa akasema yupo!
wanatumia namba 0713 456666

Be ware and enjoy yr week end...wale wa mpira tutaonana saa kumi na moja!
 
Baah, Umemkosesha weekend mwenzio sio vizuri hivyo, wee ungempeleka Central ili akaelewane na wenye njaa kama zake
 
Conman wa JF? Yap namba za wafanyakazi wa voda ni 710,tiGO 123,airtel 670 zantel 491,ttcl 210 sasatel 100!
 
wao..great! thax sana ndugu ila na msisitizo kwa akili...kuna watu wana soma hii post kama adithi za sultan na kisiwa then wanapita tuu, hawa iangalii namba mara mbili zaidi waka ikariri au kuifadhi mahali..kesho ikija watokea wataanza kusema oooh labda ndio ile nili isoma mahali, na lawama kibao! Tuwe wepesi kulichukuli jambo kwa uzito fulani kama tahadhari!
Weekend njema
 
Conman wa JF? Yap namba za wafanyakazi wa voda ni 710,tiGO 123,airtel 670 zantel 491,ttcl 210 sasatel 100!
King Kong III,sio wa JF bana..hawa jamaa ni wa kimujinimujini..wanasoma namba kwenye mabango ya matangazo na magari then wanakutengenezea deal la kukurushia
 
wao..great! thax sana ndugu ila na msisitizo kwa akili...kuna watu wana soma hii post kama adithi za sultan na kisiwa then wanapita tuu, hawa iangalii namba mara mbili zaidi waka ikariri au kuifadhi mahali..kesho ikija watokea wataanza kusema oooh labda ndio ile nili isoma mahali, na lawama kibao! Tuwe wepesi kulichukuli jambo kwa uzito fulani kama tahadhari!
Weekend njema
Bakulutu...upo sahihi kabisa..
bado kuna watu watatapeliwa na pia unajua mpaka leo bado watu wanatapeliwa almasi za vichupa,kudondoshewa bulungutu la noti mkagawane,simu za sabuni,dawa ya kuzuia nafaka zisioze na dola za kusafisha. na hii ni kwa kutodhani kuwa hata wao ni target ya matapeli kwa style tofauti
sababu kuu ni kutembea kwenye kivuli cha ubinafsi ukidhani wewe mjanja na mjuaji kumbe wenzio wajanja zaidi na wanajua wanalolifanya kwa kina kuliko ujuavyo
Good day!
 
Mjini kuna degree inaitwa E3
EDUCATION
EXPERIENCE
EXPOSURE
pamoja!
 
Si Muhaya kipande ! jizi moja linatumia lafudhi ya kihaya kama part ya disguise yake!
 
wao..great! thax sana ndugu ila na msisitizo kwa akili...kuna watu wana soma hii post kama adithi za sultan na kisiwa then wanapita tuu, hawa iangalii namba mara mbili zaidi waka ikariri au kuifadhi mahali..kesho ikija watokea wataanza kusema oooh labda ndio ile nili isoma mahali, na lawama kibao! Tuwe wepesi kulichukuli jambo kwa uzito fulani kama tahadhari!
Weekend njema

Unamaanisha namba ipi? Waliyopiga jamaa au? Si watachange tu mzigo unabaki pale pale. Line bei cheee then wanatupa kule.
 
Back
Top Bottom