Beware of Power Club Scam

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,787
1,710
Kuna mchezo uitwao POWER CLUB (eti wa kutajirishana) unazunguka hapa Tanzania. Mchezo wenyewe unatoka Ulaya, na bahati mbaya kanisa moja hapa Tanzania limejitokeza na kujipa uajenti wa kuendesha mchezo huo.

Watanzania tumekuwa tunapenda vya mkato: kughushi vyeti, kuiba mitihani, kutajirika kwa ufisadi, n.k. na kwa hiyo matapeli wa nje wanatuona ndio wa kuliwa. Nimefanya utafiti wangu katika internet na kupata yanayoweza kutuangalisha. Fungua hapa.

Ni wakati tuanze kukubali kuwa hakuna mafanikio bila jasho. Tuchape kazi, tutafute elimu kwa bidii, na mafanikio yatakuja. Pia tujiepushe na matapeli
 
Last edited:
Tafadhali tupeni habari zaidi kuhusu haka ka-mchezo. Sio tu hapo kwako Mwanaukweli, bali hata kwenye kampuni yetu imepita wimbi la DECI-Tanzania (inasemekana ina Headquarter yake Dar es Salaam - Mabibo Mwisho) , na Sijui Power CLUB. Sasa mlio na uzoefu na Vuna Vuna Time, Upatu, Utajirisho bila Jasho, Ukakamavu, Ukamuanaji, Ushindi Bila Bila nk tafadhali mtupeni basi habari, maana tunateketea bila sababu.

Hivi ninavoandika kuna wafanyakazi wame-wehuka kuanza ku-subscribe.

Nitoeni tongotongo jama....

ndimi

Mwathirika mtarajiwa.
 
Last edited:
Ndio zile dizaini za Dollarjet, utapeli kwa kwenda mbele...

Yap! Dollarjet, na baadaye ilikuja pia PENTAGONO ni mtindo huo huo. Hii Pentagono ililetwa na hao hao wanaoendesha POWER CLUB kwa sasa. Nadhani Benki Kuu ilipiga marufuku Dollarjet kama sikosei.
 
Mtuhabarishe na DECI - Tanzania (ipo hapo Dar es Salaam mabibo mwisho. Sio chama cha ukewenza wa Crisis kweli hichi? Mbona mnazungumzia Dollarjet, Pentagono, au Power-club, za nje, wakati hii DECI ni kikulacho?

Mbona hii DECI mwailetea za "Jirani Jirani Karibu Ingia, Uvungu hauna hata Kunguni. Tahamaki! mwenzio kajia mchuzi wa Ningu......"
 
Watanzania tumekwisha - tutaliwa mpka tupate pancha - nadhani pancha tulishapata tayari mpaka tube ina viraka - kazi kwenu
 
Si kwa sababu tumeamuakupenda vitu vya bure! Kijana mmoja aliyenifuata kutaka ninunue hizo ticket nikamsikiliza na kumcheka sana na nikamwambia keshaliwa. Sikujua kwamba kuna kesi linashughulikia huo upuuzi ndio maana hata kijana aliyenifuata ni mlokole. Watanzania tujiepushe na mchezo huu wa kijinga
 
Mtuhabarishe na DECI - Tanzania (ipo hapo Dar es Salaam mabibo mwisho. Sio chama cha ukewenza wa Crisis kweli hichi? Mbona mnazungumzia Dollarjet, Pentagono, au Power-club, za nje, wakati hii DECI ni kikulacho?

Mbona hii DECI mwailetea za "Jirani Jirani Karibu Ingia, Uvungu hauna hata Kunguni. Tahamaki! mwenzio kajia mchuzi wa Ningu......"

Kuna thread ina majadiliano mengi ya DECI. Ifuatilie kwenye link nayoweka hapa.

DECI, DECI, DECI, Ni nini hasa?!

Natumaini utapata unachotafuta.
 
Ninashukuru Sana. Nimefaidika na mjadala huo hapo
https://www.jamiiforums.com/business-economic-forum/22907-deci-deci-deci-ni-nini-hasa-9.html

Nawashukuru wana Jamii wote na ma-modereta.

Big Up JF

muttas
 
Hakuna njia ya mkato kuelekea utajiri, watu wafanye kazi za halali wapate vipato vya halali. Hizo schemes zimewaliza wengi waliopoteza pesa zao kwa kutegemea kupata zaidi.
 
Hakuna njia ya mkato kuelekea utajiri, watu wafanye kazi za halali wapate vipato vya halali. Hizo schemes zimewaliza wengi waliopoteza pesa zao kwa kutegemea kupata zaidi.

Yap! I completely agree with you.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom