Best Quote: "Hata ingekuwa JM ningemtosa"

Field Marshall ES,
humfahamu mama anne kilango malechela.

jaribu kumfahamu mama anne kilango kabla hujaamua kumtetea.

hata jina la familia yake hulijui. hilo kione ni jina lake la kinyumbani. siyo jina la baba yake.

unapodai mama anna kilango amezaliwa kihurio siyo uzambara unadhihirisha uwongo na unafiki wako. kauli sahihi ni kwamba amezaliwa kitongoji cha uzambara katika kijiji cha kihurio.

humfahamu anakotoka na hata tabia zake, lazima itakua vigumu kwako kuamini kauli hii aliyoitoa kwa wananchi wa kitongoji cha jitengeni ktk kijiji cha kihurio.

"mimi anna kilango nasema hakuna shule itakayojengwa hapa Jitengeni. sitaki kusikia mtu anazungumzia suala hili tena. anayetaka kuliendeleza akazungumze na mkewe chumbani."

kwasababu umesema unaijua same east tueleze manufaa ya kuzuia ujenzi wa shule katika kitongoji cha jitengeni. tueleze kwanini watoto wa uzambara alikozaliwa mama kilango wanastahili elimu kuliko wenzao wa jitengeni.

tunamuomba mama kilango atekeleze maamuzi ya vikao na kuruhusu ujenzi wa shule uzambara na jitengeni.

huzifahamu siasa za same na pare.humfahamu cleopa msuya.

upare imegawanyika katika south pare/same na north pare/mwanga.

wakati wa ukoloni na miaka ya 1970 kulikuwa na jimbo moja tu Pare District.

south pare/same ina watu mara mbili zaidi ya wale wa north pare/mwanga. kwa kila wapare 3 utakaukutana nao uwezekano mkubwa 2 wanatoka south pare/same.

chediel yohane mgonja ndiye mbunge pekee kushinda uchaguzi wa upare nzima. alifanya hivyo ktk uchaguzi wa 1965 alimshinda elias kisenge.

mwaka 1970 tanu ikaamua kuweka majimbo mawili south pare na north pare. chedile mgonja 'kaghembe' alipita bila kupingwa south pare.

mwaka 1975 majimbo yakaunganishwa tena, chediel mgonja akashinda. mwaka 1980 wilaya ikagawanywa na kuundwa wilaya za same na mwanga.

kwa data hizo nilizokupa hapo juu mawazo kwamba msuya ndiyo 'mtawala' wa upare umeyatoa wapi? au maneno hayo amekufundisha rafiki yake msuya, jumanne malechela?

hujuma za cleopa msuya dhidi ya chediel mgonja zimeumiza sana wananchi wa south pare. miaka ya 80 barabara yetu kihurio-kisiwani-same ilipaswa ipandishwe daraja kuwa barabara ya kitaifa lakini tukahujumiwa na msuya. mpaka leo barabara hiyo haijatiwa lami. huenda waziri wa ujenzi aliyeshiriki hujuma hiyo ni jumanne malechela au samwel sitta.

Lunyungu,

mama anna kilango ni mapepe ana tabia ya kupandwa jazba na kutoa matusi mara kwa mara.

mama anna kilango alifukuzwa kazi gulf air akikabiliwa na tuhuma za upotevu wa fedha.

wananchi wa same mashariki walishampa ndhira 'daniel yona' notisi asigombee ubunge watamuaibisha. mama alitumia upenyo huo kugombea na akapata.

moja ya maendeleo yaliyopatikana wakati ndhira akiwa mbunge ni ujenzi wa sekondari katika kila kata isipokuwa kihurio. sasa mama kilango kuleta kontena moja la vitabu ndiyo imekuwa nongwa?
 
la sivyo watu ndio watapigilia hapo hapo hata kama wanachosema wanajua ni uwongo....

humfahamu mama anne kilango malechela.

jaribu kumfahamu mama anne kilango kabla hujaamua kumtetea.

hata jina la familia yake hulijui. hilo kione ni jina lake la kinyumbani. siyo jina la baba yake.

unapodai mama anna kilango amezaliwa kihurio siyo uzambara unadhihirisha uwongo na unafiki wako. kauli sahihi ni kwamba amezaliwa kitongoji cha uzambara katika kijiji cha kihurio.

humfahamu anakotoka na hata tabia zake, lazima itakua vigumu kwako kuamini kauli hii aliyoitoa kwa wananchi wa kitongoji cha jitengeni ktk kijiji cha kihurio.

mama anna kilango ni mapepe ana tabia ya kupandwa jazba na kutoa matusi mara kwa mara.

mama anna kilango alifukuzwa kazi gulf air akikabiliwa na tuhuma za upotevu wa fedha.

wananchi wa same mashariki walishampa ndhira 'daniel yona' notisi asigombee ubunge watamuaibisha. mama alitumia upenyo huo kugombea na akapata.

moja ya maendeleo yaliyopatikana wakati ndhira akiwa mbunge ni ujenzi wa sekondari katika kila kata isipokuwa kihurio. sasa mama kilango kuleta kontena moja la vitabu ndiyo imekuwa nongwa?

Mzee Mwanakijiji

I'm really bored...

Bangusule,

Heshima mbele mkuu, next time kabla hujamshambulia kiongozi yoyote wa siasa bongo hapa JF, hakikisha una facts, sio hadithi za mitaaani, ninaomba kukwambia kuwa nimeteta watu wengi sana hapa JF, kuaniza viongozi mpaka wananchi wa kawaida, hakuna aliyekuwa rahisi kumtetea kama huyu mama, maana mambo yake yako clear, uzushi na uongo ndio hasa uliomfanya mama Kaboyoka, yule mama msomi wa milimani kule Pare ashindwe ubunge na huyu mama, unachekesha zaidi unapojaribu kumtukana Msuya, maana bongo nzima tunajua kuwa bila Msuya, huko Pare kusingekua na kitu kabisaa the man sacfrificed kila kitu cha taifa ili kuwasaidia huko "kwenu", sasa kuwa na shukrani japo kidogo mkuu kwa kazi nzito aliyoifanya Msuya huko.

Otherwise, mkuu hii forum kuna watu wanailipia mkuu, kwa hiyo sio haki kwao kuwajazia maneno mengi ambayo ni hewa, mama kilango sasa yuko shule akiongeza degree ya uchumi, ili aweze kuongoza vyema katika century ya technologia, na ataendelea na uongozi wake imara na kuwafichua mafisadi.

Ahsante Mkuu!
 
Field Marshall ES,

wewe ndiye usiye na facts, au labda neno hilo limebadilishwa maana. uwongo wako kuhusu mama kilango na wananchi wa same hatutauvumilia.

cleopa msuya hajawahi kuwa mbunge wa pare nzima, pare district. yeye amekuwa mbunge wa jimbo, jimbo la mwanga. katika mazingira hayo angetusaidia vipi?

msuya alijaribu kugombea mwaka 1975 wakati huo mgonja akiwa mkuu wa mkoa wa mtwara lakini mgonja hakumuachia kiti na msuya akanywea. baada ya hapo mwaka 1980 wilaya ya pare ikagawanywa kuwa wilaya ya same na jimbo la uchaguzi mwanga.

tangu kipindi hicho msuya amekuwa na chuki kubwa sana na mgonja na wananchi wa wilaya ya same/south pare. ametumia kila mbinu kumhujumu mgonja na kila jitihada alizofanya kuendeleza wananchi wake.

niko hapa kuondoa uongo na dhana iliyopandikizwa na msuya kwamba kila mpare ameendelea kwa huruma zake yeye msuya.

niko hapa kutoa ushuhuda wa same, pare ya kusini, pare iliyosahaulika.

msuya angetukomboa tusingekuwa hapa tunalilia shule miaka 47 baada ya uhuru.

msuya alikuwa wapi leo wakati wananchi wa same wanalilia
ujenzi wa barabara ya kihurio-ndungu-kisiwani-same. kama anatupenda sana si angetuwekea lami.

msuya hajawahi kusaidia jimbo la same. hata sasa hivi hatutaki ktk dayosisi ya kkkt. anataka dayosisi ya himaya yake, ufalme wake mwanga.

wako wanaotoa mapesa yao kufadhili jambo forum. sasa siyo vizuri kuruhusu chombo hiki kikatumiwa na wazushi kama wewe kueneza uongo na majungu dhidi ya wanyonge wa pare ya kusini, au eneo lolote lile la tanzania.

mwisho.

wanyonge wa pare ya kusini watapenda kujua kama jumanne malechela ndiye aliyeshirikiana na msuya kuzuia barabara ya kihurio-ndungu-kisiwani-same kuwa barabara ya taifa.
 
Wewe ni msemaji wa kina nani hapa lakini? mbona unatumia sana wingi?

msuya hajawahi kusaidia jimbo la same. hata sasa hivi hatutaki ktk dayosisi ya kkkt. anataka dayosisi ya himaya yake, ufalme wake mwanga.

Huyu Msuya ameingia vipi hapa?

wako wanaotoa mapesa yao kufadhili jambo forum. sasa siyo vizuri kuruhusu chombo hiki kikatumiwa na wazushi kama wewe kueneza uongo na majungu dhidi ya wanyonge wa pare ya kusini, au eneo lolote lile la tanzania.

Una maana kuwa JF ipo kwa ajili ya kutetea watu wa pare ya kusini? kwa nini usianze foundation au forum kwa ajili ya watu wa huko mkuu?

mwisho.

wanyonge wa pare ya kusini watapenda kujua kama jumanne malechela ndiye aliyeshirikiana na msuya kuzuia barabara ya kihurio-ndungu-kisiwani-same kuwa barabara ya taifa.

Hizi siasa za majungu na fitna zina sehemu yake kule darhotwire na forum mbofumbofu na wala sio hapa JF...... huyu Jumanne Malecela anaingia vipi kwenye hii thread!? grrrrrrrrrrrrr
 
Mkuu Pundamilia07,

Heshima yako mkuu, hivi kweli unaweza kusema hizo quote mbili hapo juu, zimetolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri mpaka kuwa na authority ya kutukana Senior members ambao ni the real deal hapa JF kama Mwafrika Wa Kike?

Pundamilia are you serious au you are having April Fool on a Valentine's day in February?

Nipe tafsiri ya neno kutukana and then uniambie katika niliyoandika lipi ni tusi?

Pili, humu ndani ya JF kuna untouchables?
 
Mkuu Pundamilia07,

Heshima yako mkuu, hivi kweli unaweza kusema hizo quote mbili hapo juu, zimetolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri mpaka kuwa na authority ya kutukana Senior members ambao ni the real deal hapa JF kama Mwafrika Wa Kike?

Pundamilia are you serious au you are having April Fool on a Valentine's day in February?

Soma postings tofauti za Mwafrika wa Kike kama zinaleta sense yeyote au zinasaidia nini kwa wasomaji na wachangiaji hapa JF.

Posting yangu ya pili ndiyo ilikuwa litmus test yako wewe kama kweli unamjua huyu mama, kwani katika maelezo yako, pamoja na mambo mengine unataka tukubali kuwa huyu mama ni safi. Hata hivyo kwa wale wanaoelewa watajua swali langu nililielekeza wapi na kwa sababu zipi. Kama unataka kuanika zaidi jibu hilo swali.
 
Mama Kilango, hajawahi kufukuzwa kazi mahali popote, alianza kiwa Mwalimu wa Sekondari Kisutu, Accountant Air-Tanzania, Accountant Gulf Air, Mfanya biashara, Mwenyekiti UWT Kinondoni, Mbunge wa Rais, na sasa Mbunge wa Same East, nirudie tena kuwa hajawahi kufukuzwa kazi mahali popote kwa wizi, ni uongo mkuu wa mchana, cc huwa hampitishi mgombea yoyote aliyewahi kutuhumiwa na wizi, ni opportunist wa siasa kama walivyo wote wanasiasa, na kiboko wa ufisadi sasa hivi tunajribu kumuomba ahamie kwenye waliojiuzulu kupelekwa mahakamni, mkuu Bangusile acha uzandiki mkuu uweli ni kwamba huna convincing argument against mama, ila una maneno mengi ya chuki na ya kijiweni huko Same, otherwise nipo mkuu kukusaidia kuhusu jimbo la Same East na mbunge wake mkuu, maana hulijui.

Mkuu FMES,
Nilikutaka uniombe msamaha lakini naona umekauka, anyway sio kitu kwani hiyo iko ndani ya hiyari yako. Hata hivyo unaweza kuniomba msamaha 'kimoyo-moyo'

Hata hivyo naona Mkuu nia yako ni kutaka kumtetea huyu mteja wako kwa hali yeyote ile.

1. Je, unaweza kutuambia kwanini aliacha kufundisha pale Kisutu Sekondari?
2. Je, unajua kuwa unasema uwongo kuwa huyu mama alikuwa 'Accountant' pale Air Tanzania? Je, unaweza kutupatia sifa za mtu anayeitwa Accountant huku ukifanya marejeo katika professional qualifications zake?
 
Mzee ES ita make sense sana kama hata mtu una facts za kuambiwa maana najua utakuwa umesoma ama kusikia zaidi kwa njia zako .Lakini huyu mtu kama anatoka Same na anasema haya lazima ufike mahali useme una za kuambiwa na huyu wa Same anazijua maana anakaa pale .Wanao teseka ni watu wa Same na wanajua more than you am sure .

Kuhusu untouchable nasema hakuna sote ni sawa mbele ya hili jamvi hakuna wa maana zaidi ya mwenzake .At least najua haya toka siku ya kwanza tunaanza na hii Forum .
 
Aminia mkuu kanyaga twende.....
 
"Heshima yako mkuu, hivi kweli unaweza kusema hizo quote mbili hapo juu, zimetolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri mpaka kuwa na authority ya kutukana Senior members ambao ni the real deal hapa JF kama Mwafrika Wa Kike?"

Mzee ES ita make sense sana kama hata mtu una facts za kuambiwa maana najua utakuwa umesoma ama kusikia zaidi kwa njia zako .Lakini huyu mtu kama anatoka Same na anasema haya lazima ufike mahali useme una za kuambiwa na huyu wa Same anazijua maana anakaa pale .Wanao teseka ni watu wa Same na wanajua more than you am sure .

Kuhusu untouchable nasema hakuna sote ni sawa mbele ya hili jamvi hakuna wa maana zaidi ya mwenzake .At least najua haya toka siku ya kwanza tunaanza na hii Forum .

Nakushuru Mkuu Lunyungu.
 
Aminia mkuu kanyaga twende.....

Ndiyo Mkuu Masatu .Ifike mahali tukubali kujifunza kwa uwazi kama hivi .Jamaa ana point sana na hata Es ana point zake sana kwenye hili lakini sasa tuone nani anaweza kuwa na ukweli zaidi .Mimi siwezi kukubishia juu ya habari za Majita, Mugango, Makoko,Nyamiongo, Buhare, na hata kule Mazami, Busegwe kwa kuwa sikai wala sijatoka huko .Wala Mbunge wa huko simjui vilivyo mbali na yeye kuwa rafiki wa mtu wangu ama mume ama mke wa ndugu yangu .Natives always wasikike ndilo nalo omba hapa kwamba kila mmoja sasa aone umuhimu wa kusikiliza kilio cha wana Same na hasa aneno ambalo huyu Mama ni Mbunge .
 
kwanza mkuu pia tuelewe kuwa si kila mwenye kukaa eneo la mbunge anamjua mbunge kuliko asiekaa.

pili si kila anaekaa huko huwa anampenda mbunge na kuwa hawezi kulengesha kuhusu sifa zake.

hata hivyo tusonge mbele
 
Soma postings tofauti za Mwafrika wa Kike kama zinaleta sense yeyote au zinasaidia nini kwa wasomaji na wachangiaji hapa JF.

Wasomaji ambao ni watetezi wa mafisadi kama wewe posting zangu haziwasaidii chochote. Kama ulitegemea nianze kukuimbia nyimbo za Komba hapa kusifia ccm wakati mafisadi kibao huko mnauza nchi basi sahau hicho kabisa.

Mafisadi mmeanza kampeni ya kumpondea mama Malecela baada ya kuwa mkali katika hii issue ya Richmonduli na alipomtetea zitto kuwa asifukuzwe bungeni na mafisadi.

Mimi huwa tunapingana na FMES mambo mengi sana na ilifikia hatua tukatoleana maneno makali hapa JF lakini katika hili la mama Kilango Malecela ninakubaliana na facts zake kuliko majungu yenu mnayotoa hapa ambayo hayana uthibitisho kabisa.

Hapa ni mpaka kieleweke na hakuna mambo ya kupakaziana kashfa zisizothibitishwa kwa sababu tu kuwa humpendi mama Malecela au mzee Malecela mwenyewe.
 
Ndiyo Mkuu Masatu .Ifike mahali tukubali kujifunza kwa uwazi kama hivi .Jamaa ana point sana na hata Es ana point zake sana kwenye hili lakini sasa tuone nani anaweza kuwa na ukweli zaidi .Mimi siwezi kukubishia juu ya habari za Majita, Mugango, Makoko,Nyamiongo, Buhare, na hata kule Mazami, Busegwe kwa kuwa sikai wala sijatoka huko .Wala Mbunge wa huko simjui vilivyo mbali na yeye kuwa rafiki wa mtu wangu ama mume ama mke wa ndugu yangu .Natives always wasikike ndilo nalo omba hapa kwamba kila mmoja sasa aone umuhimu wa kusikiliza kilio cha wana Same na hasa aneno ambalo huyu Mama ni Mbunge .

Lunyungu,

Hao natives wa Same hapa ni kina nani? Na hii sheria ya kuwa watu wa sehemu fulani tu ndio wana mamlaka ya kuongelea mambo ya jimbo hilo yameanza lini? just curious
 
what is all this about?

kwasababu Mama Kilango kasimama na kusema kweli? mnatafuta pa kukimbilia? The point here is not what she is the point is for the first time in my life nilishuhudiwa mbunge wa CCM akisimama na kusema kweli akiwa kwenye record (mbele ya umma)kwakweli everybody nilikuwa mtaani alishangilia ushujaa ule, ungeona sura za mafisadi zilivyokuwa! nilifarijika sana.

Sasa ndugu yangu unayedondosha nyeti za Anna Kilango kwani huko nyuma hata tuseme miezi 4 iliyopita hukufanya ushujaa kama wa Mama Anna hata kwa halaiki ya JF na kuingia kwenye rekodi kusema mabaya yake uko Same? hapa sisi tunakuona mchafuzi na mlaghai unayetaka kushift mambo lakini nadhani hapa Mama Kilango anasimama juu regardless of whatever u r saying.

Ushauri: Anzisha thread, iite MABAYA YA ANNA KILANGO KWA WANANCHI WA SAME baada ya hapo tutajadili hilo kwa uhuru na kujaribu kujua ukweli. LAKINI KWA SASA TUACHE TUJIMWAYEMWAYE NA HILI SAKATA NA TUENDELEZE MAPAMBANO YA KWELI
 
Ndugu yangu Lizard,

Hii ni kampeni imeanza kumuangusha huyu mama kwa habari za majungu na uongo kwa vile wameanza kuogopa indepence yake na namna anavyosema mambo kuikosoa serikali in public. Kuna watu huko ccm hawapendi hili, wanataka mambo yafanyike kimyakimya tu huku nchi ikipotea.

Haya mambo yalianza alivyoonekana kuchukizwa na kitendo cha kumfukuza zitto bungeni. Baada ya mafisadi huko ccm kuona kuwa alikuwa right na wao walikuwa wrong kumfukuza bungeni basi wakaanza hii kampeni ya kumdiscredit. Msumari ulipigiliwa juzi bungeni kwenye hii issue ya richmonduli. In the next few months utasikia mengi sana yakisemwa hapa juu ya huyu mama na mengi ni ya uongo.

Wafuate ushauri wako na waanzishe thread ya kumpondea Mama Malecela na waje na data sio majungu tu ya mtaani. Gosh, watu wamesahau kuwa hii sio darhotwire au dailynews!?
 
Huu ugonjwa wa kufikiri kila mtu anayefanya vizuri katika jambo fulani basi anafanya hivyo kwa lengo fulani binafsi inabidi tujitibu haraka. Hii tabia chafu ya kufikiri kwamba akina Mwakyembe, Kilango, etc wamefanya waliyofanya kwa kujipendekeza au kwa malengo binafsi ikome. Kauli za kijinga kama hizi ndizo zinazokatisha tamaa wajasiri wachache wanaoanza kujitokeza katika nchi yetu na lazima tuzikemee sana tena kwa mjina yote makubwa yakiwemo ya Yesu na Muhamad. Tunawatia moyo watu kama akina Mwakyembe, Kilango, Zitto, Slaaa na wengine wote wanaojitoa muhanga kwa ajili ya nchi yetu wasonge mbele na wasibabaike na maneno ya wachovu wa kufikiri na wenye wivu wa aina ya fisi. Walitaka wao ndio wafanye kama nyie mlivyofanya lakini hawana nafasi wala uwezo wa kufanya mambo makubwa sasa walichobaki ni majungu na kutoa kauli za kukatisha tamaa. Habari njema ni kwamba mamilioni ya watanzania wanaunga mkono sana juhudi zenu madamu mtaendelea kupigania kusimama kwa ile nchi. Basi nyie endeleeni huko bungeni na kwingineko, sisi tuachieni hapa tuta-deal na baadhi ya wafuasi wa hao mafisadi waliojeruhiwa hapa JF. Tunawahakikishia kuwa hapa hawatafua dafu na baada ya kitambo watakimbia na kuuacha huu uwanja ukiendelea kudunda. Walikuwepo watu sugu kama akina tafiti then jadili na mugongomugongo wakakimbia itakuwa hawa...thubutu, mtakimbia wenyewe, tena very soon.
 
ndugu yangu we, waache tu waangaike. Jana nilikuwa naangalia channel 10 usiku katika kipindi cha pambanua walikuwa wanajadili baraza la mawaziri, wananchi walikuwa wanapiga simu nakusema wazi kuwa huyu kikwete vipi mbona anaendelea na mafisadi wake kina chenge, mtangazaji akawa anaogopa na kutaka kuzima issue kwa kudai hayo ni mapenzi ya rais tuwape nafasi wafanye kazi wageni wakasema ww vipi hujui rais anafanya kazi si kwa matakwa yake? ikasemwa zaidi hapa hamna kumpa mtu nafasi tutasema tu nafasi ndiyo waliyonayo lakini kusema hatuachi na hamna kumchekea tena rais...hapa najaribu kuonyesha hata wakijaribu vipi watu si wajinga tena sasa wanasema bila uoga ni kama moto wa nyika unasambaa kwa kasi.

Ngoja nikaangalie bunge linavyoendelea
 
Masatu JF Senior Expert Member Join Date: Mon Jan 2007

Aminia mkuu kanyaga twende.....

Quote:- Masatu

The greatest lesson in life is to know that even fools are right sometimes

Quote: Kitila

"Huu ugonjwa wa kufikiri kila mtu anayefanya vizuri katika jambo fulani basi anafanya hivyo kwa lengo fulani binafsi inabidi tujitibu haraka. Hii tabia chafu ya kufikiri kwamba akina Mwakyembe, Kilango, etc wamefanya waliyofanya kwa kujipendekeza au kwa malengo binafsi ikome. Kauli za kijinga kama hizi ndizo zinazokatisha tamaa wajasiri wachache wanaoanza kujitokeza katika nchi yetu na lazima tuzikemee sana tena kwa mjina yote makubwa yakiwemo ya Yesu na Muhamad. Tunawatia moyo watu kama akina Mwakyembe, Kilango, Zitto, Slaaa na wengine wote wanaojitoa muhanga kwa ajili ya nchi yetu wasonge mbele na wasibabaike na maneno ya wachovu wa kufikiri na wenye wivu wa aina ya fisi. Walitaka wao ndio wafanye kama nyie mlivyofanya lakini hawana nafasi wala uwezo wa kufanya mambo makubwa sasa walichobaki ni majungu na kutoa kauli za kukatisha tamaa. Habari njema ni kwamba mamilioni ya watanzania wanaunga mkono sana juhudi zenu madamu mtaendelea kupigania kusimama kwa ile nchi. Basi nyie endeleeni huko bungeni na kwingineko, sisi tuachieni hapa tuta-deal na baadhi ya wafuasi wa hao mafisadi waliojeruhiwa hapa JF. Tunawahakikishia kuwa hapa hawatafua dafu na baada ya kitambo watakimbia na kuuacha huu uwanja ukiendelea kudunda. Walikuwepo watu sugu kama akina tafiti then jadili na mugongomugongo wakakimbia itakuwa hawa...thubutu, mtakimbia wenyewe, tena very soon."

Mkuu kitila, Mwafrika Wa kike, na Lizzard,

Salute, na hakuna cha kuongeza, mbarikiwe na taifa letu libarikiwe, Wabarikiwe Zitto, Dr. Slaa, Mwakyembe na Mama Kilango Malecela, ibarikiwe JF uwanja wa moto!
 
Back
Top Bottom