shumanice
Member
- Jul 21, 2011
- 64
- 25
Kampeni hizo za uraisi 2015, na hawatamuacha......watauana hiyo 2015. Ameomba kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni awe anaulizwa maswali kama ambavyo waziri mkuu huwa anaulizwa......hapo napata kigugumizi kidogo Mh. Mamba, nafahamu kuwa waziri mkuu huwa anaulizwa maswali kwa kuwa yeye pale anaiwakilisha serikali kwani yeye ndie msimamizi wa shughuli zote za serikali bungeni. Lakini pia waziri mkuu huulizwa maswali yanayohusu serikali kwa ajili ya kujua utekelezaji wa mambo mbalimbali kwa walipa kodi ambayo serikali inayasimamia. Ni vizuri pia Mhe. Mamba akafahamu kuwa waziri mkuu huulizwa maswali ali atoe majibu kwani yeye (serikali) ndio hukabidhiwa fungu (bajeti) ya utekelezaji wa shughuli zote za serikali. Sasa iweje leo Mh. Mamba atake kiongozi wa upinzani nae aulizwe maswali na wabunge!!?? Atakuwa anaulizwa juu ya nini?? Hivi lengo la yale maswali ni kutaka kujua uwezo wa waziri mkuu kuyajibu ama kupata majibu ya hoja za msingi zinazohusu utekelezaji wa waliokabidhiwa fedha za walipa kodi?? Namuomba Mh. Mamba kama kweli anataka kiongozi wa upinzani aulizwe maswali basi wamuachie bajeti ya serikali kiongozi wa upinzani ili aisimamie then waje kumuhoji serikali yake imefanya nini. Lakini pia napata picha kuwa kumbe yale maswali huwa ni kupoteza muda tu, kwani kwa mujibu wa mamba, kama hata kiongozi wa upinzani anaweza ulizwa basi huwa si kujibu hoja za walipa kodi bali ni kutaka kujua uwezo wa waziri mkuu kujibu!!!!!!!!...........KAZI NI KWETU