Berbetov na Sigara

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Mchezaji mpya wa Timu ya Manchester United Dimitar Berbetov ametakiwa kupunguza kama si kuacha kabisa tabia yake ya uvutaji sigara kama anataka kuendelea kupata namba kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Man U. Imefahamika kuwa Berbetov anavuta sana sigara na kitu ambacho kilionyesha walakini wakati wa kufanyiwa “Medical Checkup” aliposign na klabu ya Man U. “Pumzi yake haikuwa sahihi sana na vipimo vya mapafu vilionyesha moshi na ukungu baada ya kumuuliza alikiri kuvuta sigara lakini mwenyewe alisema kwa sasa amepunguza” kilisema chanzo cha habari hii ndani ya klabu ya Man U. Hata hivyo mchezaji huyo bado hajajiunga rasmi na klabu ya Man U kwani alikuwa akiiwakilisha timu yake ya Bulgaria kwenye mchezo wa awali kucheza fainali za kombe la dunia ilipocheza na Montenegro na kutoka droo ya 2-2.
 
Mbona leo nimesikia kipindi cha Udondozi wa Magazeti wakisema kuwa Berbatov anasemea yeye ni Mcha Mungu? Waandishi walimuuliza swali hilo baada ya kuonwa kuwa anatembea na Biblia.
 
Mbona leo nimesikia kipindi cha Udondozi wa Magazeti wakisema kuwa Berbatov anasemea yeye ni Mcha Mungu? Waandishi walimuuliza swali hilo baada ya kuonwa kuwa anatembea na Biblia.

Amekiri kuwa alikuwa anavuta fegi kwa sana siku za nyuma.
kwa siku za hivi karibuni amepunguza kuvuta lakini sasa ameamua kuacha na kumgeukia MUNGU ndio sababu ya kutembea ba bible ili awe anajisomea neno la MUNGU aweze kushinda majaribu aachane na sigara kabisa.
 
....Kuvuta sigara ni dhambi?????
 
Yah, kuvuta sigara ni dhambi, pia sio vizuri kwa afya.

Hivi Magehema Dhambi maana yake nini?, na nini ukifanya kinaweza kuwa 'dhambi' na nini kinaweza kuwa sio 'dhambi', binafsi naona kama ni Subjective term..! lets leave that topic kwanza.., labda zungumzia Athari zake Kiafya nitakuelewa, tukienda kwenye topic ya dhambi naona hatutafika hitimisho.

Tukirudi kwenye maada, binafsi naona kama anavuta na haimuathiri performance yake uwanjani let him carry on...unless otherwise basi hana budi kuacha...and hope kwa SAF kama anatabia hiyo 'atanyooka' tu.
 
Yah, kuvuta sigara ni dhambi, pia sio vizuri kwa afya.
..No Magehema....Nauliza kuvuta sigara ni dhambi?? Najua sigara ni mbaya kwa afya wala haina mjadala....Kitabu gani cha dini ipi kinasema kuvuta sigara ni haramu na imekatazwa???
 
Hivi Magehema Dhambi maana yake nini?, na nini ukifanya kinaweza kuwa 'dhambi' na nini kinaweza kuwa sio 'dhambi', binafsi naona kama ni Subjective term..! lets leave that topic kwanza.., labda zungumzia Athari zake Kiafya nitakuelewa, tukienda kwenye topic ya dhambi naona hatutafika hitimisho.

Tukirudi kwenye maada, binafsi naona kama anavuta na haimuathiri performance yake uwanjani let him carry on...unless otherwise basi hana budi kuacha...and hope kwa SAF kama anatabia hiyo 'atanyooka' tu.

Man u pamoja na timu nyingine kubwa za ulaya wana policy ambazo zinamlazimisha mchezaji wa vilabu hivyo kufikia vigezo walivyojiwekea.Kwa mfano inasemekana kuwa kilichomfanya mshambuliaji wa timu ya taifa ya zambia collins mbesuma ashindwe kupata namba kwenye timu yake ya Portsmouth mwaka ja alivyojiunga nayo akitokea kaizer chiefs ya sauzi alipokuwa mfungaji bora wa ligi ya sauzi, ni kushindwa kufikia kigezo kimoja cha portsmouth!alishindwa kukimbia mita 100 kwa sekunde kumi kama inavyotakiwa na policy ya portsmouth.
Kwa berbatov naye the same thing imemkuta.Kwa policy ya man u, alishindwa kukimbia kwa kasi inayokubalika kwa policy ya man u, hivyo basi katika kumchunguza ni kwa nini ashindwe hilo zoezi ndipo akafichua kuwa huwa anavuta sigara!kama kawaida yake mzee wa kazi SAF akamwambia kama anataka kuichezea man u lazima aache sigara ili awaeze ku-perform kama walivyotarajia hadi kutoa pesa mingi kumsajili.
Hayo ya dhambi au sio,fungua thread yake utajibiwa huko na wataalamu wa maandiko matakatifu na utapewa reference ukajisomee na kujielimisha zaidi.
 
Amekiri kuwa alikuwa anavuta fegi kwa sana siku za nyuma.
kwa siku za hivi karibuni amepunguza kuvuta lakini sasa ameamua kuacha na kumgeukia MUNGU ndio sababu ya kutembea ba bible ili awe anajisomea neno la MUNGU aweze kushinda majaribu aachane na sigara kabisa.

Yaani kama Mkapa vile!!!
 
Professional footballer kabla ya kusajiliwa na timu husika lazima apasi medical test ambayo inajumuisha pamoja na mambo mengine uzima wa viungo, macho,masikio na physical training kama kukimbia nk, wachezaji hufuata strict rules kufuatana na policy ya timu husika, lakini timu nyingi zinafanana katika discipline zao ambazo ni pamoja na nyakati za kulala, Diet requirements, unywaji pombe na uvutaji wa sigara, Sigara zinaathiri kwa kiasi kikubwa perfomance ya mchezaji kwa dakika 90 katika high tempo match like Arsenal or Chelsea v United ndio maana watu kama Wenger na SAF wako very strict katika anasa,SAF ana tabia ya kuwalea wachezaji wake vijana 'ki-baba na mwana'. Babu alimlazimisha Rooney kununua nyumba jirani na yeye ili isiwe tabu kumuangalia nyendo zake, alikuwa na mtindo wa kumzukia bila kutarajia saa nne za usiku!!!
 
Kuchukua Bible isiwe hoja. Majuu hawanazo kabisa - kuna makanisa kibao yana ash trays kwenye milango ya kuingia kanisani.
 
Washabiki wa Arsenal wakishaishiwa lazima hawakosi jambo la kuanzisha......ila sishangai muda wenu huu wa kuosha vinywa.
 
Back
Top Bottom