Benson Bana kwa hili Umejipambanua

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Akizungumzia hitimisho la bunge lililopita ameainisha mambo mbalimbaliambayo hakika yamepambanua upeo wake kisiasa

1.amezungumzia utoro wa wabunge unavyowakosesha umakini wa kufuatilia hoja na uhalali wao wa kuwawakilisha wananchi

2.amezungumzia majibu ya mawaziri..hayalengi uhalisia wa mifumo ya nchi yetu bali yapo kibinafsi mno na kizimamoto zaidi ,amemchana naibu waziri wa Elimu mh Mulugo kwa namna anabyoyafanyia kazi matattizo ya walimu

3.Ameupongeza upinzani kwa hoja zao..hususani Mh Tundu lissu kuwa japo hoja yake ilipingwa lakini ina ukweli.hoja ilikuwa ni udhaifu katika uteuzi wa majaji ambao ni nguzo katika muhimili wa tatu wa dola,hili halina ubishi kuwa nguzo hii si imara tena kwani nondo zilizotumika kuijenga ni dhaifu,pia amepongeza hoja ya Zitto na na Chenge katika marekebisho ya vifungu vya bajeti ya wizara ya fedha,ambavyo waziri na naibu walishavifumbia macho licha ya kujadiliwa na kamati ya fedha na kutolewa maamuzi

4.amezungumzia tuhuma za rushwa kwa wabunge na kampeni za kukwamisha bajeti ya wizara ya nishati na madini kuwa ni jambo baya sana kwa bunge,japo tunasubiri taarifa ya kamati ya maadili iliyowahoji tayari ni dosari kubwa kwa watunga sheria

5.amezungumzia upimaji wa uwajibikaji wa wa maamuzi ya bunge..yaani maazimio na utekelezaji.yaani maazimio wanayopitisha hayafuatiliwi utekelezaji wake,na wanapoanza kikao kingine hakuna tathmini ya ya kuangalia milestone na waliyokubaliana awali

6.Ametoa rai yake kuwa kero yake kuu bungeni ni ileile tunayolia nayo hapa jf ya wabunge na mawaziri kupoteza muda wa bunge kutoa pongezi hadi kwa beki tatu na drivers na kuacha hoja za msingi

Pia kazungumzia mfumo wa uhitimishaji budget ya fedha kuwa mwishoni ili kuchambua wizara nyingine vizuri..haina maana kupinga wakati mlishakubaliana katika overall budget ya fedha

bravo Benson,kwa mtazamo huu umejipambanua
Source:clouds FM PB on saturday
 
Jambo ambalo naona mr Benson amelisahau na taaisii yake ya REDET hulifanya ni upigaji kura...upigaji wakura wa bunge kupitisha vifungu ni OVYO sana
 
Hakika leo kwa mara ya kwanza(kwa maoni yangu) ameongea kitu chenye mbolea kuhusu mkutano wa Bunge uliomalizika tarehe 16/8/2012.Kabla ilikuwa nibadilishe stesheni!
 
Nmemskia aisee kafunguka vizuri sana. Kama utakumbuka Mh Mbilinyi wa Mbeya aliwahi kusema mawaziri wanatoa majibu ya mazoea na rejareja kwa maswali yote.
Kaizungumzia OPRAS, ni kweli watendaji wengi hawaipendi!
 
Nimemsikiliza Mnafiki huyu. Alichozungumza ni Facts ambazo mtu mwenye akili timamu hawezi kupingana nazo. Pamoja na Ukibaraka wake kwa CCM ameshindwa kuwatetea kwa hayo ya Zitto Kabwe, Tundu Lissu na Mawaziri kutumia muda mrefu kuwataja Ma-girl friends zao.
 
huwa wanasema, kama unaona huwezi kumshinda adui wako basi ungana nae! Sasa hata kwa akili ya mlevi hayo mambo yanaonekana, hawezi kuyatetea hata kwa chembe. Mimi siwezi kumwamin huyu jamaa hata kidogo inawezekana kweli hajalipwa posho zake, kwa sababu akili zake huwa hazitambui kosa na ubabaishaji unaofanywa na CCM
 
Benson bana ni mjanja sana, anasoma upepo. Akiona jambo litamuharibia maslahi yake ya kinafiki huwa anauma na kupuliza.
 
Jambo ambalo naona mr Benson amelisahau na taaisii yake ya REDET hulifanya ni upigaji kura...upigaji wakura wa bunge kupitisha vifungu ni OVYO sana

Na hili ndio lingedhihirisha upeo wake kweli, japo nalo na moja kati ya hayo yote aliyoyataja ambayo UMA wa watanzania unayafahamu kabla yake. hana lolote huyu chumia tumbo.
 
Akizungumzia hitimisho la bunge lililopita ameainisha mambo mbalimbaliambayo hakika yamepambanua upeo wake kisiasa

1.amezungumzia utoro wa wabunge unavyowakosesha umakini wa kufuatilia hoja na uhalali wao wa kuwawakilisha wananchi

2.amezungumzia majibu ya mawaziri..hayalengi uhalisia wa mifumo ya nchi yetu bali yapo kibinafsi mno na kizimamoto zaidi ,amemchana naibu waziri wa Elimu mh Mulugo kwa namna anabyoyafanyia kazi matattizo ya walimu

3.Ameupongeza upinzani kwa hoja zao..hususani Mh Tundu lissu kuwa japo hoja yake ilipingwa lakini ina ukweli.hoja ilikuwa ni udhaifu katika uteuzi wa majaji ambao ni nguzo katika muhimili wa tatu wa dola,hili halina ubishi kuwa nguzo hii si imara tena kwani nondo zilizotumika kuijenga ni dhaifu,pia amepongeza hoja ya Zitto na na Chenge katika marekebisho ya vifungu vya bajeti ya wizara ya fedha,ambavyo waziri na naibu walishavifumbia macho licha ya kujadiliwa na kamati ya fedha na kutolewa maamuzi

4.amezungumzia tuhuma za rushwa kwa wabunge na kampeni za kukwamisha bajeti ya wizara ya nishati na madini kuwa ni jambo baya sana kwa bunge,japo tunasubiri taarifa ya kamati ya maadili iliyowahoji tayari ni dosari kubwa kwa watunga sheria

5.amezungumzia upimaji wa uwajibikaji wa wa maamuzi ya bunge..yaani maazimio na utekelezaji.yaani maazimio wanayopitisha hayafuatiliwi utekelezaji wake,na wanapoanza kikao kingine hakuna tathmini ya ya kuangalia milestone na waliyokubaliana awali

6.Ametoa rai yake kuwa kero yake kuu bungeni ni ileile tunayolia nayo hapa jf ya wabunge na mawaziri kupoteza muda wa bunge kutoa pongezi hadi kwa beki tatu na drivers na kuacha hoja za msingi

Pia kazungumzia mfumo wa uhitimishaji budget ya fedha kuwa mwishoni ili kuchambua wizara nyingine vizuri..haina maana kupinga wakati mlishakubaliana katika overall budget ya fedha

bravo Benson,kwa mtazamo huu umejipambanua
Source:clouds FM PB on saturday

Yawezekana ni maoni yaliyosukumwa na hisia na hasira ya kukosa kitu flan.gud analysis but why now?
 
Na hili ndio lingedhihirisha upeo wake kweli, japo nalo na moja kati ya hayo yote aliyoyataja ambayo UMA wa watanzania unayafahamu kabla yake. hana lolote huyu chumia tumbo.
Suala la maamuzi ya kura katika bunge letu hunifanya nimtazame spika kwa jicho la husda sana...hivi ni kweli watz tunaburuzwa kikondoo hivyo? hapana!
 
huwa wanasema, kama unaona huwezi kumshinda adui wako basi ungana nae! Sasa hata kwa akili ya mlevi hayo mambo yanaonekana, hawezi kuyatetea hata kwa chembe. Mimi siwezi kumwamin huyu jamaa hata kidogo inawezekana kweli hajalipwa posho zake, kwa sababu akili zake huwa hazitambui kosa na ubabaishaji unaofanywa na CCM
Matatizo ni elimu kwa ubongo...ufumbuzi huja baada ya mkwamo na wala si wakati wa tambarare
 
ni unafiki kulalamikia system inayokulisha au kukuvisha.toka 2010 hakujua haya yataweza kutokea?kama hakuyaona haya ambayo wasomi wengi waliyaona basi hafai kuitwa dr na pia asitafute huruma yetu sasa wakati mambo yanaenda mrama.
Narudia bana ni mnafiki na hata aseme nini hakiwezi kuniingia akilini.
 
Back
Top Bottom