Benson Bana: CHADEMA wana hoja ya msingi; wasikilizwe

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Lile gwiji la Sayansi ya Siasa toka Chuo Kikuu cha UDSM al-maarufu Benson Bana na mmoja wa viongozi wa Taasisi maarufu ya Utafiti ya REDET amebainisha kuwa CHADEMA WASIKILIZWE MAANA WANA HOJA YA MSINGI. Huu ni ukweli ambao hata Kikwete na CCM yake wanaufahamu. KUWA CHADEMA WANATAKA MABADILIKO YA KATIBA na si vinginevyo.

Kwa hili Benson Bana na REDET nawaunga mkono kwa 100%. Naona saa Bunsen Bana ameanza kuelewa nini maana ya Upinzani na maana ya Demokrasia ye Kweli katika nchi yetu.Bunsen alini-bore sana wakati wa utafiti wa Taasisi yake ya REDET ambayo iliwapa CCM ushindi wa 72% lakini matokeo HALISI YAKAWA 61% less than 11%.

Kwa mtu ambaye ni msomi na mkweli na anayefuatilia siasa za Tanzania kwa karibu atagundua kuwa tuna tatizo kubwa sana la KIKATIBA ambalo linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa Haraka sana na kwa muda mfupi iwezekanavyo kabla ya Uchaguzi ujao wa 2015.

Tangu CHADEMA wasusie Hotuba ya Kikwete wakti wa Uzindzuzi wa Bunge kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wasomi na wananchi wa kawaida. WAPO WALIOLAANI KITENDO CHA CHADEMA kutoka kwenue Ukumbi wa Bunge kuwa ni utovu wa nidhamu au uchanga wa kisiasa. Hasa CCM ambao ndiyo MAHASIMU WAKUBWA wa CHADEMA kwa sasa baada ya kuwalainisha CUF. Tayari tumemsikia Chiligati K/Mwenezi wa CCM akitoa tamko na kutishia kuwa CHADEMA waondolewe Bungeni kwa AZIMIO LA BUNGE. Sikubaliani na Chiligati na CCM yake. Kama CCM watakubaliana wafanye hicho kitendo cha kuwaondoa CHADEMA Bungeni kwa azimio la Bunge wajue kuwa watakuwa wanatangaza vita si kati ya CCM na CHADEMA bali kati ya CCM na Watanzania wote wapenda Haki. CCM wanatakiwa kusoma alama za nyakati. Wajue nchi hii ina Watu 45 milioni na wao wamechaguliwa na watu milioni 5 tu. Yawezekana kabisa milioni 12 kati ya waliojiandikisha kupiga ambao ni milioni 20 walikuwa tayari kuwapa kura wapinzani lakini kutoka na vitisho vya kina Shimbo-JWTZ,Polisi na UWT kwamba watu lazima wakubali matokeo watu waliamua kukaa nyumbani kwa hofu ya kupigwa mabomu.

Lakini wapo waliosema kuwa CHADEMA hawajafanya kosa lolote wakiwemo watu mashuhuri kama Jaji Sinde WARIOBA-former PM enzi za MWALIMU.
Aliyenifurahisha zaidi ni Jaji Manento Mwenyekiti wa HAKI ZA BINADAMU ambaye amesema bila kutafuta maneno kuwa KWA SASA KUNA HAJA YA KUIFANYIA MAREKEBISHO KATIBA YETU YA JAMHURI WA MUUNGANO maana imepitwa na wakti. Vipengele vingi vilitungwa wakti wa enzi za Chama kimoja na hivo basi kushindwa kukidhi matakwa ya sasa ya VYAMA VINGI. CCM wanatakiwa kusikiliza ushauri huu wa kina JAJI MANENTO,JAJI WARIOBA,BENSON BANA na wasomi wengine wengi. CCM wanadanganya kwamba waangalizi wa kimataifa walisema Uchaguzi ulikuwa Huru na Haki LAKINI ASEMI KASORO WALIZOZISEMA WAZI WAZI KABISA KUHUSU TUME YA UCHAGUZI-NEC kwamba haiwezekani itende haki wakti aliyewateua viongozi wa NEC ni Rais aliyeko madarakani. Chiligati aaache usanii kila Mtanzania alisikia walichosema Wasimamizi hao. Kinachotakiwa na kurekebisha kasoro hizo na si kuanza kuandaa maandamano na maaazsimio ya kipuuzi ambayo hayatasaidia lolote sana yatazidi kuchochea hasira za Watanzania!

Hapa chini naambatanisha vifungu vya KATIBA YETU vyenye utata kama ilivyotungwa na Bunge na kusainiwa na MWANASHERIA MKUU wa kipindi hicho Mhe. Andrew Chenge. Nimetilia mkazo kwa 'red' na 'blue' kwenye vipengele kandamizi kulingana na uzito wake.


KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


YA MWAKA 1977


____________


YALIYOMO



Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais Sheria
Na.20 ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria Na.34
ya 1994
Na.34 ib.10
41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jinginelolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi ya Makamu wa Rais.
(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na mtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kama kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.
(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotungwa na Bunge.
_________________________________________________________________
34
(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Tume ya Uchaguzi
Masharti ya kazi ya Wabunge Sheria ya
1984 Na.15
ib.13 Sheria ya 2000
Na.3 ib.14
74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume yaUchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa
Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa mahsusi na sheria iliyotungwa na Bunge kwamba ni mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya aya ya
(g) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii.
(d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(5)Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa
Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au
kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.

(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
58
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;
(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani;
(e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu
atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.
(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
(9) Tume ya Uchaguzi yaweza kutekeleza shughuli zake bila ya kujali kwamba kuna nafasi miongoni mwa viti vya wajumbe au kwamba Mjumbe mmojawapo hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi
kati ya Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi.
(10) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kuwateua Wajumbe wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya
uchaguzi na, bila ya kuathiri masharti ya Sheria kama hiyo au maagizo ya Tume ya Uchaguzi, madaraka ya Tume ya Uchaguzi ya kusimamia uchaguzi yaweza kutekelezwa na wajumbe hao.
(11) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha siasa.
(12)Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(13) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya TanzaniaZanzibar.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
59
(14) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(15) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote
wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote.
NB-Wasimamizi wanaozungumziwa hapa ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Mikoa ambao ni Wateule wa Rais. Kila mtu ni shahidi jinsi walivochelewesha kutangaza na kuvuruga matokeo ya Urais na Ubunge hasa kwenye maeneo yenye nguvu kubwa ya upinzani.
 
hii ni katibu ya kina karl peters,Tipi tip na mangi meli n.k sio ya wa Tanzania wa sasa!!
 
Safi saana wana jamii tunakazi kubwa ya kuelimisha umma tusiishie jamvini tufanye kazi ileile tuliyokuwa tukiifanya wakati wa mchakato wa kumpeleka dr slaa ikulu wakachakachua sasa mwendo mdundo taarifa hizi kwa namna yoyote ziwafikie watanzania
 
Ninapata hata ukakasi ninaposoma katiba hiyo. Hata mwendawazimu anaweza kubaini udhaifu mkubwa wa katiba yetu. Sijui kwa nini viongozi hawaoni hata aibu ya kuendelea kuitetea katiba kandamizi kiasi hicho. Sijui kama kuna nchi nyingine yenye katiba ya ajabu kama hii.
 
Huyu bunsen burner (unakumbuka chemistry ya ninth grade) ni mnafiki tu. Ameanza kujipendekeza baada ya kugundua kuwa amejidhalilisha big time.
 
Back
Top Bottom