Benki ya posta yapata CEO mpya

H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,217
1,579
Benki Halisi ya Kitanzania



TAARIFA KWA WAFANYAKAZI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Tanzania anapenda kuwafahamisha Wafanyakazi wote wa Benki ya Posta kwamba Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemteua Bw. Sabasaba Kitewita Moshingi (40) kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Posta Tanzania.

Bw. Moshingi anachukua uongozi wa Menejimenti ya Benki ya Posta Tanzania kutoka kwa Bw. Alphonse Kihwele ambaye amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu (13) iliyopita. Bw. Kihwele ameitumikia Benki ya Posta Tanzania kwa uadilifu mkubwa akiwa mtumishi wa Umma na akishika nafasi mbalimbali katika Benki kwa kipindi cha miaka arobaini na miwili (42) iliyopita toka alipoajiriwa kwa mara ya Kwanza na iliyokuwa Benki ya Akiba ya Posta.

Bw. Moshingi (pichani) anajiunga na Benki ya Posta Tanzania akitokea Benki ya Standard Chartered, Kanda ya Mashariki ya Kati (Middle East Region) alipokuwa akifanya kazi kama "Regional Head of Consumer Banking Operational Risk and Sales Governance".

Kwa ujumla Kanda ya Mashariki ya Kati, ambayo Bw. Moshingi alikuwa akisimamia shughuli za kibenki za Benki ya Standard Chartered, inajumuisha nchi tano za Bahrain, Lebanon, Jordan, Qatar na Oman, makao yake makuu yakiwa Falme za Bahrain (the Kingdom of Bahrain) ambako ndiko Ofisi ya Bwana Moshingi ilipokuwa.

Kabla ya kuhamishiwa Mashariki ya Kati, Bw. Moshingi alikuwa Mkuu wa Idara ya TEKNOHAMA na Uendeshaji (Head of Technology and Operations) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania.

Bw. Moshingi ni mtaalamu wa shughuli za kibenki anayetambulika (Chartered Banker) na ni mwanachama wa taasisi za wataalamu wa shughuli za kibenki za Tanzania na Uingereza (Tanzania Institute of Bankers and the Institute of Bankers UK).

Bw. Moshingi ana shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara na Uongozi (MBA-Finance) aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana mke na watoto watatu (3).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Tanzania, Prof. Lettice Kinunda-Rutashobya, amesema "Bw. Sabasaba Moshingi ni mtaalamu na anao uzoefu wa kusimamizi shughuli za kibenki alioupata ndani na nje ya nchi yetu, hivyo atasaidia sana katika kuimarisha usimamizi wa shughuli za Benki ya Posta Tanzania ili kuifanya Benki ya Posta Tanzania kuwa moja ya Benki imara kabisa hapa nchini.

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Tanzania inajivunia ujio wake na inamkaribisha Bw. Moshingi na familia yake hapa nchini na ndani ya familia ya Benki ya Posta Tanzania".

 
Hongera sana Moshilingi.
Unakuombea upewe Uhuru afanye kazi yake Kitaalam na usiingiliwe na Wanasiasa!
 
Ninachojiuliza huyu rais vp? kila kitu anateua rais why? Siku atatuteulia hata mahausi gero majumbani mwetu!!
 
Ninachojiuliza huyu rais vp? kila kitu anateua rais why? Siku atatuteulia hata mahausi gero majumbani mwetu!!

Nafikili ni kwa mujibu wa sheria. kama itaenda hadi kwa mahousegirl bac itambidi afanye.
 
duh! Std chartered inaongoza kwa kutoa ceo's...tukianzia na mchechu,lawrence mafuru now huyu hapa..
 
Kila laheri bw Sabasaba Kitewita Moshingi! Umri wako Mzuri fanya kazi
 
Ninachojiuliza huyu rais vp? kila kitu anateua rais why? Siku atatuteulia hata mahausi gero majumbani mwetu!!

Sasa kama katiba na sheria ya nchi ndiyo inamtaka afanye hivyo unategemea nini? Yeye anatimiza wajibu wake wa kisheria. Kama ma housegirl nao wataainishwa kama wanatakiwa kuteuliwa na rais basi nao ruksa wacha ateue tu.
 
Ninachojiuliza huyu rais vp? kila kitu anateua rais why? Siku atatuteulia hata mahausi gero majumbani mwetu!!

hajateua wakuu wa wilaya wala wa mikoa kwahiyo si rahisi kufika kwa mahausigelo wetu
 
Mtindo wa Rais kuteuwa watu kwenye almost every organisation/department uliwekwa zamani hizo kutokana na mazingira ya enzi hizo. Pia tukumbuke huko nyuma Tanzania ilikuwa inafuata mfumo wa 'closed economy'. Kwa zama za leo, zama za soko horo, science & technology nashindwa kuelewa logic ya wanasiasa kwa maana ya Rais kuteuwa watendaji wakuu wa mashirika ambayo yatashindana na sekta binafsi.

Kwa nini nafasi ya CEO wa bank ya posta isitangazwe na kukawa na chombo (professional) kama Delloite, KPMG kusimamia mchakato wa kumpata mtu anayefaa? Hii kasumba ya kuteuana tumeona inauwa ATCL, Tanesco, na sasa Bank ya Posta. Hivi viongozi wetu wameshindwa kabisa kuwa na ubunifu wa kuongozi kuhusu haya mashirika? Mambo yako kama alivyoacha Nyerere enzi za chama kushika hatamu, na hapo wanategemea kushindana kwenye soko huria la dunia!
 
Mkuu hapo umenena. Tatizo kubwa katika uendeshaji wa mashirika ya Uma ni kutokuruhusu taaluma ichukue mkondo wake. Tazama yaliyomkuta mzalendo Tdo katika kuendesha TBC.

Hongera sana Moshilingi.
Unakuombea upewe Uhuru afanye kazi yake Kitaalam na usiingiliwe na Wanasiasa!
 
Interview ilifanywa na jina la mshindi (Moshingi) likapelekwa kwa rais aidhinishe.
Board ya wakurugenzi ndo ilisimamia mchakato mzima wa kutafuta the new CEO.
 
Back
Top Bottom