Benki ya Dunia yatoa mikopo ya nyumba ya Sh50 bilioni

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
BENKI ya Dunia (WB) imeidhinisha Tanzania kupatiwa mkopo wa dola za Marekani 40 milioni sawa na zaidi ya Sh52 bilioni ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa kwa ajili ya Watanzania wenye kipato cha chini.

Benki hiyo, iliidhinisha fedha hizo mjini Washington, Marekani jana na kueleza kwamba zimetolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Ida).

Chombo hicho cha fedha duniani kilisambaza taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mradi huo utajenga nyumba za kisasa ili Watanzania wa kipato cha chini ambao mara nyingi wamekuwa wakishindwa kupata mikopo benki kwa sababu hawana mali isiyohamishika.

"Lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wananchi, kuwawezesha kumiliki na kuishi kwenye nyumba bora," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Msukumo mwingine wa kuidhinisha mabilioni hayo,

Taarifa hiyo, inaeleza kwamba benki ya dunia, iliidhinisha fedha hizo, kwa sababu wakazi wengi katika maeneo ya mijini, wanakabiliwa na matatizo ya makazi.

Inaeleza kwamba watu wengi wana matatizo ya makazi kutokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu mjini na kusababisha ujenzi wa makazi holela bila kufuata utaratibu kwenye maeneo ambayo hayajapimwa.

"Kwa kuupa uwezo mradi wa ujenzi wa makazi, mkopo huu utawezesha wananchi uwezo wa kujiajiri wenyewe, kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini," alisema Mkurugenzi wa WB katika nchi za Uganda, Burundi na Tanzania, John Murray McIntire kwenye hafla ya kuidhinisha fedha hizo.

Source: Mwananchi.

Niliwahi kusema nyuma kuwa nilimsikia mshkaji akinambia jamaa (Nehemia Mchechu) aliteuliwa NHC aje kulisimamia hili dili naona mwezi unaandama pesa hizo zaja best wishes mzee. Tunasubiri kuona hizo nyumba za maskini zitakazojengwa.
 
hii kitu ni nzuri, kama kweli itawafikia walengwa. Waalimu, manesi, maaskari na watu kama hao wako lijibo kabisa....utashangaa wanachukua washkaji flani. Jamani tuwahurumieni watu hawa!!
 
Mh sidhani kmzitafika, zitaishia kwenye kampeni za CCM tu

Kuna watu wanadai kuwa jamaa ameteuliwa kuwa mkurugenzi pale NHC ili atumike kuzipitisha hizo hela ziende katika chama. GT upo tupe data mzee maana mama tibaijuka kazihangaikia sana zije sasa sidhani atafurahia zikiliwa na watu wengine.
 
Sasa hivi tu nilikuwa naangalia video za Dr Dambisa Moyo kwenye Youtube,ambae ameandika
kitabu kizuri sana 'Dead Aid'.Hii misaada ni utapeli tu.Do you think hela hizi zitaende kijijini Mtwara,Singida,Shinyanga kujenga nyumba za Walimu?
 
hizi zitaishia kwenye uchaguzi tuuuuuuuuu!!!!! asidanganyike mtu hapa!!! lakini tutazilipa wote wakati wachache wamechikichia!!!!!!!!!!
 
Kwani nazo zinapitia NHC? Maana labda ndiyo reason ya kufanya ile strategic move ya blue boy wao.
 
Mbona tuhela twenyewe tudogo sana?

Kama nyumba ya Gavana ilitumia Bilion 1.4, hizi ndururu sizitajenga nyumba 37 tu washkaji? Halafu hapo bado wakurugenzi na wengineo hawajakula. Labda zitakuwa 30 tu.

Mimi nadhani wangewasiliana kwanza na Ndulu kufahamu kiwango cha fedha kinachotakiwa kwa idadi ya nyumba zinazokusudiwa.
 
Hebu kwanza niweke rekodi straight,sijui ni akili zetu kujikita ktk misasada tu ama ni nini

ULIOTOLEWA NI MKOPO NA SI MSAADA.
 
'kwa ajili ya wananchi wenye kipato cha chini'

Hivi kipato cha chini kinaanzia shs. ngapi kushuka chini? Msaada tafadhali.
 
attachment.php
 
Mmh sijui kama kweli zitawafikia walengwa hizi hela jamani.Kama serikali inajali watu wake wazitumie kwenye jambo lililokusudiwa waache usanii kwenye hili la makazi bora.
 
Huo ni mkopo mzee and then!!!!

Yes Ni Mkopo!

Kuna watu walikua wameshachanganya na msaada

Pia management yake inabidi iwe wise kuhakikisha kweli mkopo huo unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na pia unatoa faida in the long run

Halafu gharama za huo mkopo ni nini by the way?
 
Kuna zile Bilioni 21 (ambazo ni zetu wenyewe) zilizoitwa mabilioni ya Kikwete kwa ajili ya kuwainua vipato wananchi wajasiriamali mbona hatupewi taarifa zake? Mradi mmoja baada ya mwingine. Halafu sie kimya tuu.
 
Hebu kwanza niweke rekodi straight,sijui ni akili zetu kujikita ktk misasada tu ama ni nini

ULIOTOLEWA NI MKOPO NA SI MSAADA.
Sawa ni mkopo lakini lini ulishawahi kusikia Tanzania tunalipa mikopo hiyo ndiyo imetoka watasubiri tulipe mwisho watatusamehe
 
Hawa world bank ni bora wangekuja wenyewe na kujenga hizi nyumbxa kuziuza, kwa kupitia serikalini hazitafika kwa walengwa
 
Sawa ni mkopo lakini lini ulishawahi kusikia Tanzania tunalipa mikopo hiyo ndiyo imetoka watasubiri tulipe mwisho watatusamehe

Hata kama hatulipi au kusamehewa mkuu,tena si ni afadhali tungetakiwa kulipa maanake always kusamehewa huko kunatugharimu zaidi
 
Back
Top Bottom