Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kupongezwa kwa jitihada za mara moja walizofanya kushusha mfumuko wa bei nchini, na pia kupandisha thamani ya shilingi ya Kitanzania. Katika miezi mitatu iliyopita mfumuko wa bei za vyakula umeteremka kutoka 27.8% mpaka 26.7% na inflation kwa ujumla (general inflation rate) imeshuka kutoka 19.8% mpaka 19.4%. Pia thamani ya shilingi ya Kitanzania imepanda. Kiwango cha kubadilisha dola 1 ya kimarekani kwa shilingi ya kitanzania ilikuwa 1900, leo hii ni 1598. Hongera Gavana Benno Ndulu kwa kazi nzuri. japokuwa nadhani huu ni mpango wa muda mfupi na tusiutegemee sana kama Taifa kuwa utadumu. Lengo likiwa kushusha mfumuko wa bei mpaka tarakimu moja kufikia June (ahadi ya BoT), kwa vyovyote vile inabidi muumize kichwa zaidi, na zaidi ya yote tuweke mipango ya muda mrefu ya kuimarisha uchumi wetu na hususani kupunguza imports. Je watafanikiwa, sijui, lakini ni matarajio na matamanio yetu kuwa watafika; tunawaombea dua. Wenzangu na mie wanashindwa kukuelewa ukiwapa hizi tarakimu, wao wanataka waone tu bei ya dagaa, maharage na sembe imeshuka maana wengi wao hata sukari haiwahusu sana. Je, tunaweza kukiri kuwa tumeshindwa kuzalisha misosi kiasi cha kutosha kushusha bei za chakula nchini? Ama tumeshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kusambaza chakula nchini kiasi kwamba watu wa nyanda za juu kusini wanakosa pa kuweka chakula ilhali Nzega wanakufa na njaa?
Mkuu Kigwangalla,
Ni lini exchange rate ya TShs/US$ ilifika shilingi 1900? Nimeangalia exchange rate ya kuanzia Januari 2009 mpaka juzi Ijumaa 22/3/2012, sikuona hiyo rate. Kwa kuhakikisha naomba angalia hapa: Bank of Tanzania: Financial Markets - Interbank Foreign Exchange Market (IFEM)
Data za IFEM ndio ambazo huwa zinatoa indicative exchange rate kwenye Bureaux de Change na mara nyingi ukiangalia selling rate ya BoT inaweza kukupa mwelekeo mzuri kwa kuongeza margin ya kama shilingi 100 kwenye selling rate.
Kwa hiyo credit yako ina walakini mkubwa sana. Ndio nilisema analysis yako umeiandika kimtazamo wa ki-CCM zaidi kuliko uhalisia wenyewe. Unataka kutuonyesha kwamba Prof. Ndullu amefanya kazi kubwa sana lakini hakuna kitu, bado tunacheza huko huko na hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila kukicha.