Tatizo hapa Watanzania wengi hatujazoea kuwa na watu walio na uwezo wa kuzungumza vizuri ndio maana wengi mnakuwa mko impressed naye. Kwenye nchi zilizoendelea angekuwa anaonekana ni wa kawaida sana.
yeah ndiyo ukweli wenyewe na hatuwezi kujilaumu kwa hilo kwa kujilinganisha na wenzetu wa ulaya au marekani kwa sababu siyo viwango vyetu.Wewe chukulia kuna vinchi vya ulaya mashariki na vyenyewe bado ni masikini lakini ukifuatilia maendeleo yao ya elimu utaona walishaanza kuwa na universities tangia karne ya kumi na tatu au hata kabla wakati bongo ni karne ya 19 ama 20 ndipo walau watu walianza kwendakwenda shule kidogo.
Wanasema kujenga hoja ni kipaji lakini shule inasaidia sana.