‘Bendera za vyama soko la Mtwara marufuku’

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, mwishoni mwa wiki lilipitisha sheria ndogo ya uendeshaji wa masoko, ambapo limepiga marukufu upeperushaji wa bendera za vyama vya siasa katika maeneo ya masoko na atakayekiuka atakabiliwa na kifungo cha miezi 12 jela au faini ya Sh50,000.

Akiwasilisha rasimu hiyo kwa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Erinest Mwongi alisema sheria hiyo imelenga kudhibiti vurugu katika maeneo ya masoko ambazo husababishwa na mvutano wa kisiasa.

Alisema mbali na kuepusha hali hiyo, pia sheria hiyo itaondoa mgawanyiko wa kisiasa unaojionyesha kwa kila mfanyabishara kupeperusha bendera ya itikadi yake ya chama cha siasa na hivyo kusababisha maeneo ya masoko kugeuzwa kuwa vijiwe vya kisiasa.

Baraza hilo lilipitisha sheria hiyo, ambayo pia inazuia utoaji wa lugha ya matusi katika maeneo hayo na kutoa adhabu ya miezi 12 jela au kulipa faini ya isiyopungua Sh50,000.

Katika kikao hicho kilichoketi chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Suleimani Mtalika (Shilingi) pia kilipitisha sheria ndogo ya mazingira inayokataza utupaji wa taka ovyo, sanjari na utunzaji wa mazingira na sheria ndogo ya kilimo na usalama wa chakula.

Akichangia hoja hiyo, diwani wa Kata ya Vigaeni, Ali Nassoro (White) alishauri kutumia busara katika utekelezaji wa sheria hizo ili kuepusha mikanganyiko baina yao na wananchi.

“Leo tunapitisha sheria za mazingira, tukumbuke kuwa hakuna vifaa vyovyote vya kuwekea takataka, katika mazingira haya tusianze kutekeleza sheria kabla ya wajibu wetu, tuandae mazingira ya sheria hizi kutekelezeka” alisema White.
 
Sehemu nyingi huwa zinapepe bendera za chama pinzani kuliko tawala,watanzania wanaona aibu kupeperusha bendera ya chama tawala cos hakuna walichomfanyia ktk miaka 50 so sheria yao walenga bendera za chama pinzani ndizo tunazoziona sehemu mbalimbali nchi
 
Nadhani hii ni unconstitutional. naomba wanaseria wetu watueleze kama kuna kitu cha namna hiyo! Mwisho watasema watu hawaruhusiwi kuongea!
 
Nadhani hii ni unconstitutional. naomba wanaseria wetu watueleze kama kuna kitu cha namna hiyo! Mwisho watasema watu hawaruhusiwi kuongea!


hii ni kinyume na ibara ya 13(2) ya katiba, inasemaa 'ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake'

kifungu kidogo cha (5) cha ibara hiyohiyo kinatoa maana ya neno ubaguzi, 'maana yake ni kutimiza haja...kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila...maoni yao ya KISIASA...
 
madiwani vilaza, hawawazi kuwatumikia wananchi wao, akili zote zipo kunyanyasa wananchi tu.
 
vyama vya siasa vimesajiliwa kwa sheria ya nchi....

bendera za vyama pia ni sehemu yake.....

wataalamu wa sheria imekaaje hiyo?
 
Back
Top Bottom