SEAL Team 6
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 655
- 118
Kufuatia kifo cha Dictator Gaddafi serikali kupitia Waziri Membe itapeperusha bendera ya nchi nusu mlingoti. Hili jambo linanichanganya kidogo, ni kwa heshima gani aliyostahili Gaddafi kupewa hadi bendera ipepee nusu milngoti? Dunia nzima inajua kwamba Gaddafi alikuwa Dictator amehusika na mauaji ya watu kama siyo halaiki tena kwa kiburi tu.
Gaddafi huyo huyo alishirikiana na Dictator wa Uganda Amini kuvamia nchi yetu na Watanzania wengi waliuawa, sasa hapa kuna umuhimu gani wa serikali ya Tanzania kupeperusha bendera nusu mlingoti? Mbona wakati IDD AMINI alipokufa Tanzania hatukupeperusha bendera nusu mlingoti?
Inamaana ile misaada yake ya kujenga Miskit ndiyo imetufanya tuchukue maamuzi hayo? Kwa maana nyingine ni kwamba hata IDD AMINI kabla hajafa angejenga shule au Kanisa hapa Tanzania, siku ya kifo chake ingepeperusha bendera nusu mlingoti?
Kama ni suala la IMANI lingeachiwa viongozi wa dini ndiyo waeleze msimamo wao kuhusu uzuri na ubaya wa Gaddafi.
Gaddafi huyo huyo alikuwa ni mshirika wa Gaidi OSAMA BIN Laden, inakuwaje tunawashangilia watu hatari kama hawa. Tunachokiona hapa siyo sera za nchi bali ni SIASA KWA AJILI ya 2015, sasa huu ndiyo ujinga wa serikali yetu.
Serikali kukataa kuwatambua waasi inamaana inafanya maandalizi kwenda Libya kuwafurusha serikali ya mpito ya Lbya. Tujiulize tena au tumuulize Waziri membe nini kauli yake kuhusu MAZISHI ya GADDAFI kufanyika BAHARINI kama ilivyokuwa kwa OSAMA BINLaden???
Watanzania tunaliona hili kuwa maombolezo hayo ni maalumu kwa MAFISADI na Wenyeuchu wa Madaraka ( Wachakachuaji na wezi wa KURA)na wala hayawakilishi Watanzania wenye nia njema.