Benard Membe ni nani? Kuna anayemjua zaidi?

Mchaga 25

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
464
114
Huyu mtu anatajwa kuwa huenda akawa rais 2015 katika kujiaminisha kuwa ni mtu anaye faa hebu tuanze kukusanya maoni kutoka kona zote za nchi kwa wana JF wazalendo.
 
Hauweze wapi huo urais,islaeri wametutukana yeye kakaa kimya hakujibu chochote,huyu si atakua kilaza zaidi ya mkuu wa kaya.

Huyu ni Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa(Minister of foreign affairs and international relations)
 
Ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa sio uhusiano wa kimataifa.
 
Huyu mtu anatajwa kuwa huenda akawa rais 2015 katika kujiaminisha kuwa ni mtu anaye faa hebu tuanze kukusanya maoni kutoka kona zote za nchi kwa wana JF wazalendo.

Mhe. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, toka 2007 hadi sasa. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama tokea mwaka 2000 ambako akiwa Mbunge amekuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje. Amekuwa Mkuu wa Idara ya Siasa na Ushirikano wa Kimataifa ya CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tokea 2007 hadi 2011 Kamati Kuu ilipojiuzulu, na Mjumbe wa NEC tokea 2007 hadi sasa.

Nje ya siasa, Amefanya kazi katika Ofisi ya Rais hadi alipokwenda kugombea Ubunge mwaka 2000. Amekuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania Canada kati ya mwaka 1992 hadi 2000. Ana elimu ya Shahada ya Uzamili(Masters) kwenye masuakpla ya Uhusiano wa Kimataifa, International Law and Economics kutoka moja ya vyuo bora nchini Marekani cha John Hopkins University (School of Advance International Studies). Ni Mkristo Mkatoliki na ana Mke mmoja na watoto watatu.
 
Kabla muda wa uchaguzi kuanza yaani.2015 Ajitaidi aweamejenga barabara ya kutoka mtwara paka newala kwa kiwango cha rami kupitia nanyamba. tandahimba. mahuta. newala.kinyume na hapo.yy BENARD.na kina MKUCHIKA.kina GHASIA.sijui NJWAYO.kazi mnayo.kwanza kunaviongozi kusini madictetor.wanapendwa ikulu lakini wananchi hawawataki.hata uyo muindi aliekaa hapo mtwara saizi amewekwa na wazee wanao kwenda kuchukua kanzu na kubazi wakati wa ramadhani tunajua mtwara vijijini ndio usiseme ghasia ghasia tupu
 
Mwaka jana amewezesha mashekhe kutoka kata zote za jimbo lake la Mtama kwenda kuhiji Mecca, pia viongozi wa dini ya kikristo kwenda kuhiji Jerusalem
 
ni joka la mdimu mnafiki mkubwa anajipendekeza kupata huruma ya waumini wa kiislam kwa kusema kujiunga oic sio tatizo
 
Mhe. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, toka 2007 hadi sasa. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama tokea mwaka 2000 ambako akiwa Mbunge amekuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje. Amekuwa Mkuu wa Idara ya Siasa na Ushirikano wa Kimataifa ya CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tokea 2007 hadi 2011 Kamati Kuu ilipojiuzulu, na Mjumbe wa NEC tokea 2007 hadi sasa.

Nje ya siasa, Amefanya kazi katika Ofisi ya Rais hadi alipokwenda kugombea Ubunge mwaka 2000. Amekuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania Canada kati ya mwaka 1992 hadi 2000. Ana elimu ya Shahada ya Uzamili(Masters) kwenye masuakpla ya Uhusiano wa Kimataifa, International Law and Economics kutoka moja ya vyuo bora nchini Marekani cha John Hopkins University (School of Advance International Studies). Ni Mkristo Mkatoliki na ana Mke mmoja na watoto watatu.
........umeiacha kazi moja nafikiri ni kwa makusudi, maalum ulishaanza, wewe malizia tu na ile.
 
Maranyingi mtu akisoma USA hua anarudi akiwa controled and monitored with CIA. Ninamashaka na huyu broo... Huenda akawa kwenye plan C ya US kumuweka kama rais wao.

Hata hivyo, THE ISSUE HERE IS CCM, AND NOT THE MATTER OF CCM PESIDENTIAL CANDIDATE.
 
Ni waziri wa mambo ya nje na mbunge wa mtama mkoani Lindi. Amewahi kufanya kazi TISS
 
Naona kambi ya membe wamejiandaa sana kwa kujifanya kuuliza maswali ili waweze kutoa taarifa za membe. Cv yake bado sana wapambe wake.
 
Akiwa TISS yeye ndiye aliyefuatilia ile issue ya Mke wa Mzee Kitine kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa Mamilioni ! ni KACHERO mzuri sana lakini ninapata shida sana na utendaji wake katika siasa maana hizi TISS na SIASA haviendani kabisaaa !
 
Back
Top Bottom